KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 21 July 2012

Mbunge ahukumiwa kifungo au kulipa faini baada ya kukutinana na hatia
21/07/2012

Mbunge wa Maswa Mashariki, Sylvester Kasulumbai (CHADEMA), na kada wa chama hicho, Robert William, wamehukumiwa kifungo cha miezi saba jela au kulipa faini ya sh 250,000 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa mawili ya jinai.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Tabora, Thomas Simba, muda mfupi baada ya kumwachilia huru mbunge wa Viti Maalum wa chama hicho, Suzan Kiwanga, na mwanachama mwingine, Anwaryn Kashaga.

Kasulumbai na mwenzake walifungwa pingu na kupelekwa katika mahabusu ya mahakama kitendo ambacho kililalamikiwa na wakili Mbogolo kwamba ni cha udhalilishaji na uvunjaji wa haki za binadamu.

“Unakifurahia kitendo unachokifanya? Alisikika Kasulumbai akimuuliza askari polisi aliyemvika pingu mara baada ya hukumu hiyo kutolewa.

Akisoma hukumu ya kesi hiyo, hakimu Simba alisema kuwa hii ni sawa na kesi nyingine zinazowakabili watu wengine kwamba mbunge huyo atakwenda jela miezi mitatu kwa kutoa lugha ya matusi au kulipa faini ya sh 50,000.

Pia aliwahukumu washtakiwa hao kwenda jela miezi minne au kulipa faini ya sh 100,000 baada ya kuwatia hatiani kwa kosa la shambulio liletalo madhara mwilini.

Hakimu Simba vile vile aliwataka washtakiwa hao kumlipa fidia ya sh 2,000,000 mlalamikaji Fatuma Kimario, ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga.

Washtakiwa wote walilipa faini hiyo na kuachiliwa huru huku wakibaki kusubiri kulipa fidia hiyo ya sh milioni moja kila mmoja.

Awali upande wa mashtaka ulidai kuwa washtakiwa wote walitenda makosa hayo Septamba 15 mwaka jana, katika Kijiji cha Isakamaliwa wilaya ya Igunga.

Mara baada ya kuachiliwa huru, Kiwanga na Kashaga walitoka nje na kutimua mbio jambo lililowafanya watu waliokuwepo mahakamani hapo kuwashangaa.

Mapema wakili wa utetezi, Edson Mbogolo, aliiomba mahakama itoe adhabu ndogo kwa wateja wake kwa vile ni wakosaji wa mara ya kwanza na kwamba Kasulumbai (62) ana watoto 27 na wake watatu wanaomtegemea.

“Mahakama izingatie kwamba Kasulumbai ni mwakilishi wa wananchi na endapo akipewa adhabu ya kifungo, jimbo lake litakuwa wazi na hivyo litaigharimu serikali kuitisha upya uchaguzi,” alisema Mbogolo.

Makosa mengine yaliyokuwa yakiwakabili washtakiwa hao ni kumweka chini ya ulinzi isivyo halali kwa mujibu wa sheria Mkuu huyo wa Wilaya, huku kosa la nne ni wizi kutoka maungoni ambalo halikuweza kuthibitishwa na hivyo kufutwa na mahakama.

via gazeti la Tanzania Daima.


No comments:

Post a Comment