KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 29 January 2012

Urais CCM 2015 Ni Balaa ( GAZETI MWANANCHI)


KIGOGO AMWAGA MAMILIONI, ATUMA MAKADA MIKOANI KUMNYOSHEA NJIA
 Na Mwandishi Wetu
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionya wanachama wake kuacha ndoto za urais wa mwaka 2015, kauli hiyo sasa imeonekana kupuuzwa na kugeuka kichocheo cha kuongeza kasi ya kujipanga kwa baadhi ya makada wenye nia ya kusaka nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa taifa.
 
Hivi karibuni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, alionya kwamba chama hicho hakiko tayari kuendelea kuwakumbatia wanachama wake wanaunda makundi ndani ya chama, kwa lengo la kusaka umaarufu wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015
.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Nape alisisitiza kuwa endapo mwanachama yeyote atabainika kuvuruga mshikamano ndani ya chama kutokana na kigezo hicho, CCM haitasita kuchukua hatua kali dhidi yake. 
 
Pamoja na CCM kutoa onyo hilo kali, mbio za urais wa mwaka 2015 ndani ya chama hicho, zimeelezwa kuingia katika sura mpya baada ya mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo, kufanya kikao kizito jijini Arusha, kwa lengo la kuweka mikakati ya kujipanga na kuimarisha kambi yake.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wana CCM mjini Arusha, zinaeleza kuwa, kigogo huyo alifanya kikao chake wiki chache zilizopita katika moja ya majengo ya mfanyabiashara mmoja kutoka Kanda ya Ziwa, yaliyopo nje kidogo ya jiji.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa Serikali, pamoja na mambo mengine, kilifanya tathmini ya kina kujua maeneo ambayo mgombea huyo hakubaliki.
Chanzo chetu kilidokeza kwamba tathmini hiyo ilionyesha kuwa kada huyo hakubaliki sana katika mikoa ya Lindi , Mtwara pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, ukiwemo Mkoa wa Mara.
Kutokana na hali hiyo, ilikubaliwa kuwa fedha nyingi zitumike na watu mahiri wenye ushawishi, watumwe katika maeneo haya ili kuwalainisha baadhi ya viongozi wa CCM ambao wanaonekana kuwa mbali na mgombea huyo, na jambo hilo lifanyike haraka kabla ya kuanza kwa chaguzi mbalimbali ndani ya CCM mwaka huu. 

Kauli ya Nape 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoliuzwa kuhusiana na kikao hicho, alisema hana taarifa zozote lakini alionya kuwa endapo itathibitika kuwa kuna makada wa chama hicho wanafanya ‘rafu’ hizo, watachukuliwa hatua za kisheria za chama kwani huu si muda wa kufanya kampeni za urais. 

Aliwataka wanachama wa CCM kuipa nafasi  Serikali yao kutekeleza majukumu yake na ilani kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Awali, pia Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, aliwahi kukaririwa akisema kuwa wanaotarajia kutumia fedha kupata urais kupitia chama hicho wanajidaganya, ni bora watafute kazi nyingine za kufanya.


 Kikao cha mkakati 
Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho, zililidokeza Mwananchi Jumapili  kuwa makada watakaotumwa kuzunguka mikoani, baada kukamilisha kazi yao, watatakiwa  kurejesha ripoti itakayofanyiwa kazi, ili kundi hilo liweke mikakati zaidi ya kufanikisha lengo lake.
Inaelezwa kuwa hofu kuu ya kundi hilo, ni kutoka kwa baadhi ya makada wengine wa CCM, wanaotajwa kuonyesha nia ya kuwania nafasi ya urais, kukubalika zaidi ndani ya chama katika mikoa hiyo, ambapo baadhi yao  wanatoka huko.
Chanzo chetu kilidokeza pia kuwa mbali ya kuweka mikakati hiyo kabambe ya kuwania urais, pia wajumbe wa kikao hicho ‘kizito’, walifanyiwa sherehe kubwa ambapo nyama na vinywaji mbalimbali vilimwagwa kwa wingi, ndani ya majengo ya mfanyabiashara huyo, ambayo yamezungushiwa ukuta mrefu.
“Aisee! kikao kilikuwa kizito mno mikakati mizito imewekwa , jamaa yuko serious (makini) kuutaka urais, “alidokeza kada mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa tayari, makada waliotumwa kwenda mikoani ‘kumnyoshea njia’ mgombea huyo wa urais, hivi sasa wanavinjari kwenye maeneo hayo, wakiwa na fedha za kutosha na vitendea kazi vingine, yakiwemo magari ya uhakika.
Waliotumwa kufanya kazi hiyo, ni wenyeviti  wa baadhi ya mikoa ambao imeelezwa kuwa watatumia nafasi zao kufanya ushawishi huo kwa urahisi.
Ingawa hadi sasa hakuna kada ndani ya CCM ambaye ametangaza hadharani  kutaka kuwania urais, inadaiwa kwamba.... Soma zaidi; http://www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment