KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 29 January 2012

Rais Dk. Jakaya Kikwete akutana na mkuu wa Vodafone


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw.  Vittorio Colao katika Hoteli ya Sheraton Waldhuus, Mjini Davos, Uswisi, Viongozi hao wawili wanahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani unaofanyika mjini Davos na mazungumzo yao yaliangaza dhamira ya Vodafone ya kuongeza uwekezaji katika kusaidia ustawi wa jamii nchini na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio Colao mjini Davos, Uswisi.
Vodafone ndio wanahisa wakuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania.
Bw Colao ambae anahudhuria mkutano wa Uchumi wa Ulimwengu – WEF mjini Davos kama ilivyo kwa Rais Kikwete walipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo hayo katika hoteli ya Sheraton Waldhuus.
Mazungumzo hayo yaligusia mahusiano ya Vodafone na seriklai ya Tanzania na watu wake hususan katika uwekezaji katika jamii kusaidia kukuza,kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii nchini ikiwa ni utekelezaji wa azma na malengo makuu ya Vodafone ya kuchangia kubadili maisha ya watanzania.
Vodafone kupitia Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza kiasi kikubwa cha fedha kusaidia na kuunga mkono miradi mbalimbali ya kijamii nchini ikiwemo maeneo makuu matano ya Elimu, Afya, Kuinua vipato vya wanawake, Mazingira na Michezo ili kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo
Katika mazungumzo hayo mafupi Bw. Colao alimuhakikishia Rais Kikwete kwamba Vodafone itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya jamii Tanzania hususan katika maeneo ya afya na elimu ambayo yanauhusiano wa moja kwa moja na wa karibu katika kuiwezesha jamii kuondokana na changamoto ambazo zinaweza kuathiri maendeleo ya watu na hivyo kushindwa au kupunguza kasi ya kubadili maisha yao.

No comments:

Post a Comment