KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday 19 December 2011

Vodacom Yatoa Msaada Kwa Yatima


Meneja Mauzo wa Kampuni    ya Vodacom Kanda ya Kaskazini Bw. Jerome Munishi akimkabidhi Mkurugenzi    wa kituo cha watoto yatima cha Matonyak Bi. Emmy Ndeumo cha Mjini Arusha    zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha watoto kusherehekea vema    siku kuu ya Krismasi. Misaada hiyo iliyojumuisha vykula na vifaa vya    shule ilikabidhiwa jana ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Vodacom Share    and Care.
Mtoto Naseeb Juma wa kituo    cha watoto yatima cha Kibowa kilichopo eneo la Lemara mjini Arusha akipokea    kwa furaha zawadi ya Krismasi kutoka kwa Meneja Mauzo wa kampuni ya    Vodacom Kanda ya Kaskazini Bw. Jerome Munishi. Vodacom imetoa zawadi    mbalimballi kituoni hapo ikiwemo vyakula na vifaa vya shule ikiwa ni    sehemu ya kampeni ya share & care inayoendeshwa na Vodacom Desemba    ya kila mwaka.
Mfanyakazi wa Vodacom kanda    ya kaskazini Rehema Ndunguru akigawa viburudisho watoto wa  kituo    cha Matonyak cha mjini Arusha ikiwa ni sehemu zawadi mbalimbali za krismas    zilizotolewa kituoni hapo kupitia  kampeni ya Vodacom Share &    Care inayoendeshwa kila ifikapo Disemba. Vodacom imekabidhi misaada    mbalimbali kwa vituo sita vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira    magumu vya mjini Arusha jana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Kanda ya kaskazini wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na watoto pamoja na viongozi wa kituo cha yatima cha Matonyak cha mjini Arusha. Wafanyakazi hao walifika kituoni hapo jana kukabidhi zawadi mbalimbali za krismasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Vodacom Share & Care ambapo jumla ya vituo sita vya yatima vya mjini Arusha vilipatiwa misaada.

No comments:

Post a Comment