KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 4 October 2012


RAIS Jakaya Kikwete amewatumia salamu za rambirambi wakuu wa mikoa ya Mbeya na Shinyanga kutokana na ajali zilizotokea juzi katika mikoa hiyo kwa nyakati tofauti.


Katika salamu zake kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro kutokana na ajali iliyotokea katika Mlima Mbalizi, ambapo watu wapatao 11 wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine ishirini na moja (21) kujeruhiwa, Rais alitoa pole kwa ajali hiyo ambayo imesababisha msiba mkubwa mkoani humo.



Pia alitoa rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ali Nassoro Rufunga kuhusu ajali iliyotokea Kahama, ambapo watu watatu walifariki na wengine 23 kujeruhiwa.



Rais Kikwete ametuma salamu hizo akiwa anatarajia kuanza ziara ya kiserikali nchini Canada kuanzia jana hadi mwishoni mwa wiki hii baada ya kualikwa na Gavana Jenerali wa Canada, David Johnston.

Rais Kikwete akiongozana na Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson kuingia jumba la Rideau jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012
PICHA VIA IKULU

No comments:

Post a Comment