KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 1 October 2012


KATIBU Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Luteni Yusufu Makamba, amesema Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), ya  Chama Cha Mapinduzi (CCM) imefanya kazi nzuri kwa kuwa imesajiri supa timu ya kucheza ligi ya mwaka 2015.
 
Makamba ametabiri kuwa kazi nzuri iliyofanywa na NEC mjini Dodoma wiki iliyopita itakiwezesha chama hicho kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa rais na wabunge mwaka 2015.
 
Kauli hiyo aliitoa jijini  Dar es Salaam jana  wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuzindua kisima cha maji kinachomilikiwa na Kanisa la Anglikana Low Church Parishi ya  Ukonga Mazizini ambapo alialikwa kuwa mgeni rasmi.
 
“Nasema kama mwanachama wa CCM, lakini pia kama Katibu Mkuu Mstaafu wa chama, tumesajiri wachezaji wa super ligi ya mwaka 2015, wanaosema
CCM itakufa watakufa wao,”alitamba Makamba.
 
Aliongeza “Naamnini kuwa sisi tumesajiri vizuri, maana usajili ni mzuri, kila aliyesajiliwa akipata nafasi ya kushinda  afanye yale yanayotakiwa”.
Alisema katika uchaguzi huo wao walizingatia zaidi kuunda timu itayochochea ushindi mwaka 2015 na si vinginevyo.
 
Wakati huo huo Makamba alihimiza mshikamano miongoni mwa waamini wa kanisa hilo akionya kujiepusha na majungu na fitina kwa kuwa sasa tabia hiyo mbaya imejikita mpaka makanisani.
 
Alisema licha ya kuwepo maandiko yanayowataka waumini kutii mamlaka lakini wapo watu wanayapiga teke maandiko hayo na hivyo kuwadharau wapakwa mafuta wa Mungu hadi kufikia hatua ya kumvua kofia wakiwa madhabahuni.
 
“Siku hizi majungu na fitina vimeingia mpaka kanisani, maandiko yanasema kutii mamlaka lakini watu wanamvua kofia  hata askofu,” alisema Makamba.
 
Makamba alialikwa katika uzinduzi wa kisima hicho kilichogharimu zaidi ya sh. milioni 10 kutokana kanisa hilo kuthamini mchango wake.
 
Katibu wa Kanisa hilo Keneth Elia alisema Februari  26, mwaka huu Makamba alikuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa kisima hicho.
 
Alisema Makamba alichangia matanki mawili kila moja lina lenye ujazo wa lita 5000 na mabomba yaliyosaidia kusambaza maji hayo.

No comments:

Post a Comment