KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday, 6 September 2011

Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Korosho Nchini.


Mheshimiwa, Anna Margaret Abdallah
---

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa, Anna Margaret Abdallah (Mb) kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Korosho.

Sambamba na uteuzi huo, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe kwa mujibu wa Sheria ya Tasnia ya Korosho na 18 ya mwaka 2009, Kifungu cha nne (4) amewateua Wajumbe wengine Nane ili kuiongoza Bodi hiyo itakayosaidia kupeleka mbele sekta ndogo ya zao la Korosho.

Wajumbe wa Bodi hiyo ni kama ifuatavyo: Bwana Twahir Nzallawahe, Mtaalam wa Agronomia kutoka Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika; Bwana Muzamii Karamagi, Mwakilishi wa Wabanguaji wakubwa wa korosho na Bibi Tumpale S. Magehema, akiwa Mjumbe kutoka kundi la Wabanguaji wadogo wa Korosho.

Wajumbe wengine ni Bwana Madanga Allon, Mjumbe wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Pwani (CORECU), Bwana Yusuph S. Namila, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba Newala Cooperative Union (TANECU) na Dkt. Peter Massawe, Mtaalam na Mtafiti wa zao la Korosho kutoka Kituo cha Utafiti wa Zao la korosho Kanda ya Kusini, ARI – Naliendele.

Aidha, Waziri Maghembe amewateua pia Mheshimiwa Jerome Bwanausi, Mbunge wa Lindi, Profesa Haji Semboja, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; Bwana Hemed Mkali, Mkulima wa Korosho Mkoa wa Pwani na Bwana Mudhihir Mohammed Mudhihir Mbunge wa zamani wa Jimbo la Mchinga Mkoani Lindi. Uteuzi huo unaanza mara moja na utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,

Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,

Dar es Salaam,

Simu: 2861319; 0769-239946; 0718-128653

Tumsaidie Mzee Kipara

Hali ya Mzee Kipara (Fundi Said) kwa sasa.
 Pichaa Juu na Chini ni muigizaji mkongwe anayekwenda kwa jina la Mzee Kipara akiwa kwenye moja ya Maigizo Enzi Hizo
 Mzee Kipara akijaribu Kushuka kitandani juzi
--

Na Mwandishi Wetu
 
UNAMFAHAMU muigizaji mkongwe anayekwenda kwa jina la ‘Mzee Kipara?” Kama jibu ni ndiyo basi soma habari hii.

Mzee Kipara ambaye jina lake halisi ni Saidi Fundi (pichani) hivi sasa anasumbuliwa na miguu kukosa nguvu, tatizo ambalo endapo atapelekwa hospitali pengine linaweza kupata nafuu kama si kupona kabisa.

Kampuni ya Global Publishers inayochapisha Magazeti ya Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa, Ijumaa Wikienda na Championi imempa simu ya mkononi msanii huyo mkongwe, ambayo itamsaidia katika mawasiliano na wasamaria wema ambao tunawaomba mumchangie kwa njia yoyote hasa ya M-Pesa.

Simu hiyo ilikabidhiwa kwa mzee huyo wiki iliyopita na mmoja wa wahariri wa magazeti yetu, Mohammed Kuyunga, Kigogo Mbuyuni jijini Dar anakoishi.

Kuyunga alisema kuwa kampuni imeguswa na hali aliyonayo Mzee Kipara hivyo kupitia simu hiyo inaamini watu wengi walioguswa na maradhi yake wataweza kumsaidia kwa hali na mali.

“Hii simu tumempa pamoja na laini yenye namba 0753 92 34 54 ambayo imeunganiswa na huduma ya M-Pesa ili kuwa rahisi kwa watu kuweza kumtumia fedha,” alisema Kuyunga.
 N.B. Kutoa ni moyo na siyo utajiri, hivyo hima popote ulipo nchini, msaidie mzee huyu kwa kumtumia kiasi chochote utakachojaaliwa kwa njia ya M-PESA AU TIGO PESA, itamfikia mwenyewe moja kwa moja na unaweza kuongea nae kwanza. Elfu 2 utakayomtumia ina msaada mkubwa kwake na Mungu atakulipa - WEB MASTER.

Rais Jakay Kikwete Aizawadia NSSF Kwa Mchango Wake Katika Sekta Ya Ujenzi Nchini

 Rais Jakaya Kikwete akihutubia katika ufunguzi wa mkutano wa siku tatu unaojumuisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makandarasi uliofanyika Mlimai City Jijini Dar es salaam jana
Rais Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau akiwa mwenye furaha mara baada ya kukabidhiwa cheti na Rais Jakaya Kikwete kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi nchini
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau(Wa Pili Kushoto) akiwa wkenye mkutano huo jana jijini Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja Mara baada ya kufungua Mkutano wa wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makandarasi uliofanyika Mlimai City Jijini Dar es salaam jana
 
Na Alfred Ngotezi
 
Rais Jakaya Kikwete leo amemkabidhi Cheti Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dr. Ramadhani Dau kwa kutambua mchango mkubwa wa Mfuko huo katika sekta ya ujenzi hapa nchini.
 
Rais Kikwete ambaye alikuwa mgeni kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku tatu uliojumlisha wahandisi, Wabunifu majengo, Wakadiriaji na Makondrasi alitoa zawadi hiyo kwa niaba ya Bodi ya Wakondrasi.
 
Mkutano huo uliohudhuriwa na maelfu ya watu, kutoka nje na ndani, ulianza tarehe 5 na utakwisha tarehe 7 Septemba mwaka huu. Baadhi ya wajumbe walitoka Afrika Kusini, Zambia, Kenya na Malawi.
 
Akiongea kwenye hafla hiyo fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mjini Dar es Salaam, Rais aliwapongeza Wahandisi, Wabunifu Majengo, Wakadiriaji na Makondrasi walioandaa mkutano huo na kuwataka wajiunge pamoja ili waweze kupata uwezo mkubwa wa kufanya kazi.
 
Katika siku za karibuni NSSF imekuwa na miradi mikubwa ya ujenzi. Baadhi ya miradi hiyo ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, nyumba za Polisi Dar es Salaam na Zanzibar na nyumba za Jeshi huko Monduli Arusha. Hivi karibuni NSSF itaanza kujenga Daraja la Kigamboni.

Mgombea Ubunge Jimbo la igunga Kwa tiketi ya UMD

Mgombea ubunge kwa tiketi ya UMD, Ndegeya Lazaro akitoka kuchukua fomu ya kuwania nafasi hiyo kwa baiskeri katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Igunga, mkoani Tabora jana. Uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika jimboni humo hivi karibuni.Picha na Joseph Zablon.

Monday, 5 September 2011

Wabunge Wa CCM Wamtetea Rais Jakaya Kikwee

Mbunge wa Sumve (CCM,)Mheshimiwa Richard Ndasa,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti la Mwanahalisi toleo la wiki hii ambazo zilielezea hatua ya bunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais,  kufuatia sakata la  kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na kurudishwa tena kazini.  Kulia ni mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu.Habari na Picha na Mdau Victor Makinda
--
 
Akizungumzia habari iliyochapishwa na gazeti hilo,Mheshiniwa Ndasa alisema kuwa gazeti la Mwanahalisi limechapisha habari za kizushi na za uongo zenye lengo la kufitinisha Bunge na Rais.Aliongeza kusema kuwa wakati Jairo anarudishwa kazini na Katibu Mkuu, Luhanjo, Bungeni mjini Dododma hapakuwa na hatua yoyote ya wabunge kupanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kufuatia kuruhusiwa kwa Jairo kuendelea na kazi.

Akifafanua kuhusu uamuzi wao wa kutolea ufafanuzi na kukanusa habari hiyo, Ndasa alisema wao kama wabunge wa CCM, hawatopenda kuona kiongozi wa nchi anazushiwa habari zisizo na ukweli wowote. 

Akijibu swali kwa nini wao kama wabunge wajitokeze kukanusha taarifa hiyo ikiwa Ikulu ina kurugenzi ya Mawasiliano, Bunge linaongozwa na Spika, Pia yupo Waziri mkuu, ambaye ni kiongozi wa shughuli za serikali bungeni ambao kimsingi moja kati ya mamlaka hizo ndizo zilizotakiwa kufafanua au kukanusha habari hiyo, Ndasa alisema,  wao hawajatumwa na Ikulu wala mamalaka yoyote bali wametumwa na dhamira yao kama Watanzania

Kamati Teuli Iliyoundwa na Bunge Kuchunguza Sakata la Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg.David Jairo Yaanza Kazi Rasmi

Wajumbe wa Kamati Teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo ikiwa kwenye kikao chake leo jijini Dar es Salaam.Picha na Owen Mwandumbya-Bunge
---

Wajumbe wa Kamati Teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo kuchangisha pesa kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Wizara pamoja na hatua ya katibu Mkuu kiongozi kuitolea taarifa ya uchunguzi mbele ya waandishi wa Habari kabla ya kuwasilishwa Bungeni imeanza kukutana leo katika Ofisi ndogo ya Bunge chini ya uenyekiti wa Mhe. Injinia Ramo Makani (CCM), mbunge wa Tunduru Kaskazini,
.
kamati hiyo inayoundwa na mhe. Goesbert Blandes (CCM), Mbunge wa Karagwe, mhe. Mchungaji Israel Natse (Karatu-Chadema), mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF) na mhe. Martha Jachi Umbulla (CCM). Mbunge wa Viti Maalum, inafanya kazi kwa kuongozwa na hadidu tano za rejea ambazo ni:

kuchunguza utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilishwa kwa uwasilishaji wa Hotuba za bajeti za wizara bungeni na kwamba, hadidu hiyo ya kwanza itakuwa na vipengele vitatu. Vipengele hivyo ni pamoja na:
·kuchunguza uhalali wa utaratibu huo kisheria na kwa mujibu wa kanuni, iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika bajeti husika pamoja na matumizi halisi ya fedha zilizokusanywa.

Hadidu rejea ya pili ni kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni,

Hadidu rejea ya tatu ni kuchunguza mfumo wa Serikali kujibu hoja zinazotolewa bungeni na taratibu za kuarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa hoja hizo".
Hadidu rejea hiyo ya nne ina vipengele viwili ambavyo ni kuchunguzwa kwa usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa suala la Jairo na kubaini iwapo utaratibu huo umeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.

Hadidu ya rejea ya tano ni kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi huo.

Vodacom Tanzania yapata Mkurugenzi Mtendaji Mpya.


Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Vodacom Tanzania,Rene Meza
--

5 September 2011

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom leo imemtangaza Rene Meza kuwa Mkurugenzi Mtendaji mpya wa kampuni hiyo hapa nchini.

Rene ambae kwa sasa ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Bharti Airtel Kenya ana uzoefu mpana wa kimataifa katika sekta ya mawasiliano ya simu wa zaidi ya miaka kumi na miwili akiwa ameshafanya kazi barani Afrika, Asia na Larin-Amerika.

Akizungumzia uteuzi huo, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Johan Dennelind amesema:

“Tunayo furaha kubwa kwa Rene kujiunga nasi. Rene analeta uzoefu mpana kutoka nchi alizowahi kufanyia kazi ikiwemo Paraguay, Pakistan na Kenya na amewahi pia kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Millicom’s (Tigo) nchini Tanzania hivyo basi ni wazi majukumu yake mapya katika Vodacom hayatokuwa na ugumu na atayamudu ndani ya muda mfupi.”

Rene anachukua nafasi ya Dietlof Mare ambae ameomba kupangiwa kazi nyengine baada ya kuwa katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka minne na nusu na hilo linafanyika kama sehemu ya programu ya Vodacom ya maendeleo ya uongozi. Taarifa ya kazi mpya atakayopangiwa itatolewa baadae. 

“Napenda kumshukuru Dietlof,chini ya uongozi wake Vodacom Tanzania imepiga hatua kubwa, kwa sasa ni kampuni ya pili kwa ukubwa Afrika ikiwa na wateja zaidi ya milioni tisa ukiacha Vodacom Afrika Kusini. Amekuwa ni kiongozi wa kuhusudiwa na wengine, uendeshwaji wa huduma ya M-Pesa na nyengine zilizobuniwa na kusimamiwa nae zinaiweka Vodacom mahala pazuri kibiashara katika siku za usoni.”Alisema Dennelind.

Dennilend amesema Vodacom itautumia ujuzi wa Dietlof popote katika kundi la makampuni ya Vodacom.

Mwisho

Imetolewa na:
Mwamvita Makamba
Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano
Vodacom Tanzania
+255754704265
mmakamba@vodacom.co.tz

VODACOM MISS TANZANIA KUONDOKA NA GARI AINA YA JEEP MPYA YENYE THAMANI YA SHILINGI M.72


Meneja Masoko wa CFAO Motors Alfred Minja kulia na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania George Rwehumbiza wakifunua gari aina ya JEEP ambalo limetolewa kama zawadi ya Vodacom Miss Tanzania 2011 lenye thamani ya shilingi milioni 72 za kitanzania gari hilo limetengenezwa nchini Marekani. Hafla ya kuonyesha gari hilo la zawadi imefanyika asubuhi hii katika duka la kampuni ya CFAO Motors lililopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam, kulia anayeshuhudia tukio hilo ni mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.
Meneja Masoko wa CFAO Motors Alfred Minja katikati na Mkuu wa Udhamini na Masoko Vodacoma Tanzania George Rwehumbiza wakikabidhi funguo za gari lililotolewa na kampuni hiyo kama zawadi ya Vodacom Miss Tanzania kwa Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga
Warembo watakaoshindania taji la Vodacom Miss Tanzania wakiwa wamelizunguka gari ambalo lilmetolewa kama zwadi ya mshindi atakayeibuka siku hiyo.
Warembo wa Vodacom Miss Tanzania wakifurahia zawadi yao gari aina ya Jeep iliyotolewa na wadhamini wa shindano hilo CFAO Motors na Vodacom Tanzania.

Mgombea Ubunge Jimbo La Igunga-CCM Dk. Dalally Kafumu Achukua Fomu

MKURUGENZI wa Uchaguzi jimbo la Igunga Magayane Protace (kulia) akimkabidhi fomu za kuwania ubunge wa jimbo hilo, mgombea mteule wa CCM Dk. Dalally Kafumu , jana. Wengine ni Katibu wa CCM wilaya ya Igunga Neema Adamu na Msimamizi wa masuala ya uchaguzi wa CCM, Matson Chiz
MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba wakiwa katika huzuni kwenye hospitali ya wilaya ya Igunga ambako walisaidia kupeleka mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake, jana. Kulia ni ndugu wa mtoto huo.
MGOMBEA mteule wa CCM jimbo la Igunga Dk. Dalally Kafumu (kushoto) na Mratibu wa Uchaguzi wa CCM jimboni humo, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba wakimfariji Kulwa Mpina baada ya kufukisha kwenye chumba cha kuhifadhi maiti mwili wa mtoto Peter Ezekiel ambaye alifariki papo hapo baada ya kugongwa na lori la mizigo katika barabara ya Igunga-Singida akijarbu kuvuka barabara akiwa na mamia ya wananchi wa jimbo hilo waliokuwa wakimsubiri Kafumu na msafara wake, jana.Picha na Bashir Nkoromo

Dj Venture Afanya Kweli...


 Dj Mashuhuri Nchini Tanzania Dj Venture amefunga pingu za maishaa jana Jijini Dar es Salaam na Bibie Berna na kufwatiwa na sherehe ya nguvu iliyofanyika kwnye hoteli ya kimataifa ya Hyatt Regency Zamani Kilimanjaro Hotel Kempinsky.Picha Zote Zimefotolewa na Mdau Ahmed Michuzi

TASWIRA ZA MAHAFALI YA ST.THERESE OF LISIEUX KINDERGARTEN/PRIMARY SCHOOL

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita wa shule ya ST.Therese Lisieux iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam wakiongozwa na muongoza kwaya kuimba wimbo wa kuwaaga na kuwapongeza wahitimu wa kidato cha saba katika shule hiyo hapo jana.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la  pili wa shule ya ST.Therese Lisieux iliyopo Ukonga  jijini Dar es Salaam wakitoa heshima ikiwa ni ishara ya heshima ya kuwaaga  wahitimu wa kidato cha saba katika shule hiyo ilyofanyika mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya walimu wa Shule ya ST.Therese Lisieux iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam wakiwa kwenye hafla ya mahafali ya Saba (7) katika shule hiyo.
Baadhi ya wahitimu darasa la saba (7) katika shule ya ST.Therese Lisieux iliyopo Ukonga jijini Dar es Salaam wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Mjue Dr. Dalaly Peter Kafumu, Mgombea Ubunge Jimbo La Igunga Kwa Tiketi Ya CCM

JINA :Dk. Dalaly Peter Kafumu
 
KUZALIWA-Agosti 4, 1957        
 
MAHALI      
Kijiji cha Itumba, Tarafa ya Igunga Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
 
NDOA
              Nina mke  na watoto watano ambao kati yao watatu ni Madaktari wa binadamu, wengine wawili bado wanasomea Udaktari wa Binadamu na mmoja anasoma  Stashahada ya Ufamasia.
 
ELIMU
 *Shahada ya kwanza ya Madini- BSc (Geology)-1983
*Stashahada ya Elimu-PGD (Education)-1987
*Shahada ya Uzamili ya Madini-BSc (Geology)-1995
*Stashahada ya Utafutaji Madini-PGD (Mineral Exploration)-1991
* Sahahada ya Uzamivu ya Madini-Ph.D (Geology)-2000


UZOEFU CCM*
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa TANU (TYL) tawi la Itumba (1971-1972)
*Mjumbe wa Kamati ya Siasa na Halmashauri Kuu ya Tawi la CCM, Madini (1983-1992).
*Mjumbe wa Mkutno Mkuu wa Wilaya na mkoa wa Dodoma (1983-1992).
*Katibu wa Tawi la CCM, Madini Dodoma (1988-2011).
*Kada wa CCM (1988-2011).


UTUMISHI WA UMMA
*Kamishna wa Madini Tanzania (2006-2011)
*Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Nishati na Mdini (2004-2006)
*Mkuu wa Kitengo cha Uhamasishaji na Takwimu Wizara ya Nishati na Madini (2002-2004).
*Mtaalam Mwandamizi wa Madini (1993-2002)
*Mhadhiri Chuo cha Mdini Dodoma (1978-1992)
*Mtaalam wa Madini Wizara ya Nishati na Madini (1983-1987).


 TAALUMA
*Mtaalam Bingwa wa Madini Nchini.
*Mwanachama wa Chama Cha Wataalam wa Madini Tanzania na Afrika.
*Mjumbe wa (II)) Bodi  za Usajili wa Makandarasi (II) Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) na Chuo Kikuu    cha Dodoma (UDOM). 
 
  MCHANGO KWA TAIFA
*Mtaalam wa Madini (1983-1987)
Nilishiriki kwenye utafutaji wa madini na kugundua machimbo mengi ambayo sasa yanachimbwa na kuleta mapato, ajira na kukuza uchumi wa taifa.
 
*Mhadhiri wa Chuo cha Madini (1987-1992)
Nilifundisha mafundi sanifu katika fani ya madini, zaidi ya wahitimu 1,000 wanalitumikia taifa katika nafasi nyingi serikalini na kwenye sekta ya madini nchini.
 
*Mhadhiri wa Nje wa Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (2004-2006)
Nilifundisha masuala ya Jiolojia ya Mazingira na kuhitimisha wanafunzi zaidi ya 500 ambao sasa wanalitumikia taifa na katika sekta mbalimbali nchini.
 
*Kamishna wa Madini (2006-2011)
Nimesimamia marekebisho ya sheria ya Madini ya mwaka 1998 ili kupata sheria ya mwaka 2010. Sheria mpya inahakikisha kwamba:-
(i) Serikali na Wananchi wanashiriki zaidi katika uwekezaji madini kwa kupata hisa kwenye migodi.
(ii) Wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya migodi wanafidiwa vizuri, kujengewa makazi mazuri na kushiriki kwenye mradi husika.
 
(iii) Kampuni kulipa kodi na mrahaba kwa viwango vya juu zaidi.
 
(iv) Wachimbaji wadogo wanatengewa maeneo yao, kupewa leseni zenye muda mrefu ili waweze kupata mitaji kutoka kwenye taasisi za fedha;na
(v) Viwanda vya uongezaji thamani ya madini vinajengwa hapa nchini ili kuongeza ajira na kukuza uchuni; na
(vi)Madini ya vito (Almasi, Tanzanite, Ruby na mengineyo) yanachimbwa na Watanzania tu.


MCHANGO KWA IGUNGA
*Kamishna wa Madini (2006-2011)
(i) Nilisaidia wachimbaji wadogo nchi nzima kupata maeneo na viwanja kwa ajili ya uchimbaji madini.
 
Kwenye Wilaya ya Igunga nimewasaidia wachimbaji wadogo wa madini kuwapa leseni maeneo ya Bulangamilwa na Nanga.
(ii) Kuwapatia soko la dhahabu mjini Nzega na Dar es Salaam wachimbaji wadogo wa dhahabu wa wilaya ya Igunga.
 
(iii) Kuwashauri wachimbaji wadogo nchini na Igunga kuhusu umuhimu wa kufuata sheria na kanuni za madini ili wasidanganywe na watu wanaotumia sekta ya madini kutapeli na kuwaibia.
(v)Ofisi yangu kama Kamishna wa Madini ilikuwa wazi kwa wana Igunga wote kufika na kuopata ushauri, maelekezo na msaada waliohitaji.


HUDUMA KWA JAMII (2005-2011)
(i) kujenga Misikiti miwili katika Kata ya Itumba, kutoa vitabu vya rejea na kiada kwa shule kumi za sekondari wilaya ya Igunga:- Itimba, Igunga, Mwamashimba, Mwisi,Mwanzugi, Igurubi, Manshiku, Simbo na  Nanga.
 
(ii) Kufadhili vikundi vya kina mama, Kata ya Itumba, Kwaya za Madhehebu ya Kikristo Igunga mjini na Mwanzugi.
 
(iii) Nikiwa  mwanachama wa Igunga SACCOS nimekisaidia chama changu kwa ushauri wa kitaalam na kutoa ada na hisa na michango yangu kwa wakati.
(v) Nikiwa mlezi wa Vijana Kata za Mwamashimba na Itumba nilifadhili vifaa vya michezo (mipira, jezi na kombe) na kuendesha ligi ya mpira wa miguu katika kata hizo mwaka 2009-2010.
(vi) Nilitoa mchango wa sh. 800,000 kuchangia ujenzi wa visima virefu viwili Kata ya Itumbi.


HUDUMA KWA UMMA WA TANZANIA
*NikiwaMjumbe wa Bodi ya Makandarasi (2006-2011) nimesimamia kuandikisha makandarasi nchini wanaotoa huduma za ujenzi kwenye sekta ya barabara na majengo na nikiwa mjumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (2009-2011) nilishiriki katika usimamizi wa chuo hicho ili kutoa viajana wasomi bora wa kulitumikia Taifa la Tanzania.