KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday 31 May 2012


Serikali Yawaondoa Hofu Watalii Zanzibar



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALI

TAARIFA KWA UMMA

Tanzania ni Salama kwa Watalii

Kufuatia vitendo vya vurugu zilizozuka hivi karibuni katika maeneo kadhaa ya Mji wa
Zanzibar baada ya mitandao ya kimataifa imekuwa ikiripoti taarifa za kuwepo kwa hali
ya wasiwasi kwa watalii wanaotaka kuja kutembelea Visiwa hivyo.

Kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utalii, ningependa kuwahakikishia
wageni, ambao tayari wako nchini, na wale ambao wanajiandaa kuja, kuwa vurugu hizo
ambazo zimeshadhibitiwa na Serikali hazikuathiri utalii. Mjini Zanzibar pamoja na
maeneo ya vivutio vya utalii kote nchini.

Hadi hivi leo napotoa taarifa hii, amani imetawala Mji Mkongwe Zanzibar na hakuna
taarifa yoyote ya uharibifu wa maeneo ya vivutio vya utalii vya Zanzibar wala kuchomwa
kwa hoteli ama kudhulika kwa raia yeyote wa kigeni. Hivyo nasisitiza kuwa Zanzibar
nisehemu salama kwa watalii.

Vilevile, Siku chache kabla ya tukio la Zanzibar, kulikuwa na matukio manne ya watalii
kuporwa katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Uporaji huo ulitendwa na watu
waliokuwa kwenye magari au pikipiki ambao waliwapora watembea kwa miguu.

Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio
ya pekee na ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kupita na hatua
zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongoza usalam kwa wakazi na watalii.

Nachukua fursa hii kuwahakikishia wageni kwamba kila juhudi zimechukuliwa
kuhakikisha kuwa usalama wa watalii unadumishwa pamoja na faraja wakati
watakapotembelea Tanzania.

Daima tukumbuke kuwa, Tanzania ni kisiwa cha amani na nchi imenuia kudumisha sifa
hiyo nzuri.

Karibu Tanzania.

Mhe. Lazaro Nyalandu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
30 Mei, 2012

No comments:

Post a Comment