MANISPAA YA ILALA YAVUKA MALENGO YA UKUSANYAJI KODI
Meya amesema kuwa kwa ujumla ukusanyaji wa mapato katika mwaka huu imepanda kutoka 88% kwa mwaka 2010/2011 mpaka shilingi 17.1 bilioni zilizokusanywa kwa mwaka huu kiasi ambacho ni sawa na 99% ya mafanikio katika Malengo.
“Ongezeko hili limetokana na vyanzo vingi vya mapato kwa asilimia 102% ambayo ni sawa shilingi 2.25 bilioni kutoka katika mabango ya Matangazo yaliyopo Barabarani” amesema.
Ametaja Kitengo kingine kilichochangia kuongeza mapato kuwa ni Utoaji wa Leseni za Ujenzi kilichochangia Milioni 307 pamoja na Makusanyo ya Mapato kutoka kwenye kodi yaliyochangia shilingi 2.14 bilioni .
No comments:
Post a Comment