KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 3 August 2011

Makatibu Wakuu Wastaafu Waangwa

Katibu mkuu kiongozi Philemon Luhanjo(kulia) akimpa zawadi aliyekuwa katibu Mkuu ofisi ya Rais Ikulu, Michael Mwanda na mkewe wakati wa hafla ya kuwaaga makatibu wakuu wanne waliostaafu hivi karibuni katika hafla iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam jana jioni. Makatibu wakuu wengine walioagwa katika hafla hiyo ni pamoja na Andrew Nyumayo kutoka wizara ya Ulinzi, Bi Mariam Mwafisi Wizara ya Maendeleo ya jamii na Bi Ruth Mollel kutoka ofisi ya Makamu wa Rais.
Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo(watatu kushoto)akiwa katika picha ya pamoja na makatibu wakuu waliostaafu hivi karibuni katika hafla ya kuwaaga iliyofanyika katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam jana jioni.Wengine katika picha kutoka kushoto Michael Mwanda(ikulu),Bi.Ruth Mollel(Makamu wa Rais),Bi Mariam Mwafisi(Maendeleo ya jamii) na Andrew Nyumayo(Ulinzi).Picha na Freddy Maro-I

No comments:

Post a Comment