Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikaguwa Gwaride lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga wakati alipokuwa akiondoka uwanja wa ndege wa Fevereiro uliopo jijini Luanda, Angola leo Agosti 19, baada ya kumalizika kwa mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana Agosti 18.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maafikiano yaliyotokana kuhusu itifaki ya pamoja kwa nchi za SADC inayohusu udhibiti wa fedha chafu sambamba na katiba ya ushirikiano wa majeshi ya Polisi kwa nchi wanachama wa SADC yaliyoafikiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa SADC mjini Luanda Angola jana Agosti 18.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Mogan Changirai, walipokutana kwenye mkutano wa 31 wa Viongozi wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliomalizika jana Agosti 18, nchini Luanda Angola.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Maendeleo zilizopo kusini mwa afrika (SADC), wakiwa katika mkutano wa 31 wa Viongozi wa Jumuiya hiyo uliomalizika nchini Luanda Angola jana Agosti 18. Picha na Amour Nassor-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment