KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday, 7 August 2011

Chadema na maamuzi magumu; Shoka Moja, Madiwani Wake Watano wa Arusha wamefukuzwa!

KAMATI kuu ya CHADEMA inayokutana mjini Dodoma inasemekana imewatimua madiwani wake watano wa Arsuaha mjini kwa tuhuma za kushirikiana na chama tawala CCM.

Madiwani hao ni Naibu Meya na Diwani wa Kimandolu, Estomih Mallah, Diwani wa Elirai, John Bayo, Diwani wa Themi, Ruben Ngowi, Diwani wa Sekei, Crispin Tarimo, Diwani wa Kaloleni, Charles Mpanda na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed.

Habari zilizotufikia zinasema Madiwani hao wamefukuzwa saa sita usiku wa kuamkia leo, baada ya kuitunishia misuli Kamati Kuu hiyo ya CHADEMA kwa kukataa kuhojiwa mmoja baada ya mwingine na badala yake wakataka wahojiwe…
KAMATI kuu ya CHADEMA inayokutana mjini Dodoma inasemekana imewatimua madiwani wake watano wa Arsuaha mjini kwa tuhuma za kushirikiana na chama tawala CCM.

Madiwani hao ni Naibu Meya na Diwani wa Kimandolu, Estomih Mallah, Diwani wa Elirai, John Bayo, Diwani wa Themi, Ruben Ngowi, Diwani wa Sekei, Crispin Tarimo, Diwani wa Kaloleni, Charles Mpanda na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Mohamed.

Habari zilizotufikia zinasema Madiwani hao wamefukuzwa saa sita usiku wa kuamkia leo, baada ya kuitunishia misuli Kamati Kuu hiyo ya CHADEMA kwa kukataa kuhojiwa mmoja baada ya mwingine na badala yake wakataka wahojiwe kwa pamoja,la sivyo liwalo na liwe.

“Wamefukuzwa kwa kuonekana wamekula dili na CCM na kukubali muafaka hali ambayo uongozi wa Chadema uliwashushia tuhuma madiwani wake hao kwamba wamelamba rushwa”, kimesema chanzo chetu cha habari ndani ya kikao hicho.

Madiwani hao wamekana katakata shutuma hizo na kuomba ushahidi wa kuthibitisha hilo.

Awali Madiwani hao walisema wameamua kuingia muafaka na CCM kwa sababu ya uchu wao wa kutaka maendeleo zaidi katika jiji la Arusha badala ya mitafaruku isiyo na mwisho ambayo inachelewesha maendeleo.CHANZO: Global Publishers

No comments:

Post a Comment