KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday, 26 July 2011

Taswira Mbalimbali Kutoka Bungeni Mjini Dodoma

Waziri wa Katiba na Sheria Celina Kombani(kulia) na Mbunge wa viti Maalum(CHADEMA) Suzan Kiwanga (kushoto) wakimsikiliza Mbunge wa Maswa Magharibi (CHADEMA) John Shibuda nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Kahama, James Lembeli, kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Leo
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na ujumbe wa Shirika la Missada la Kimataifa la Japan (JICA) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) unaofuatilia Mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami za Babati - Dodoma na Tunduma Mangaka, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Leo.Kushoto ni Waziri wa Ujenzi John Magufuli.
Mbunge wa Jimbo la Nyang’hwale (CCM) (kushoto) Hussein Nassoro Amar akisalimiana na Patrick Grones (kulia) ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari St. Ignatius Collage ya Mjini London Nchini Uingereza nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma. Wanafunzi hao wako nchini kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ambapo leo wamepata fursa ya kutembelea Bunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na ujumbe wa Shirika la Missada la Kimataifa la Japan (JICA) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) unaofuatilia Mradi wa ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha lami za Babati - Dodoma na Tunduma Mangaka, kwenye ukumbi wa Mikutano wa Waziri Mkuu, Bungeni Mjini Dodoma Leo .Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, john Magufuli.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment