Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Prof.Jummanne Maghembe akiwasoma bajeti ya wizara hiyo leo mjini Dodoma.
Mbunge wa Kilwa Kusini kupitia chama cha CUF Selemani Bungara akichangia hoja kuhusiana na masuala ya kilimo katika jimbo lake mara baada ya waziri wa wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Jummanne Maghembe (hayupo pichani) kuwasilisha bujeti ya wizara hiyo leo bungeni mjini Dodoma .
Naibu waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Lucy Nkya(katikati),naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri (kulia) na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Benedict Ole-Nangoro (kushoto)wakijadili jambo leo wakati wa kikao cha bunge la bajeti kinachoendelea mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi(kushoto)akimsikiliza Naibu waziri wa Nishati na Madini Adam Malima (kulia)mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha asubuhi cha maswali na majibu katika bunge la 10 la mkutano wa bajeti kikao cha thelathini na mbili kinachoendelea mjini Dodoma.
Viongozi wa Tanzania Media Fund (TMF) wakifuatilia kwa umakini bajeti ya wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wakati waziri wa wizara hiyo Jummanne Maghembe(hayupo pichani) alipokuwa akiisoma leo bungeni mjini Dodoma. TMF kupitia mpango wao wa fellowship kwa mwaka huu imefadhili waandishi wa habari watano kwa ajili ya kuandika habari za uchunguzi kuhusu masuala ya kilimo vijijini kwa kipindi cha miezi sita.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Mkoa wa Magharibi Zanzibar Mjumbe Msuri Mjumbe(wan ne kulia)akiwa katika picha ya pamoja na wabunge wa CCM wa wilaya hiyo nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.Picha Zote na Anna Nkinda-Maelezo
No comments:
Post a Comment