Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Stadi(VETA),Emanueli Bukuku akiwa na gari aliyoiigundua ambayo haitumii mafuta. Gari hiyo inatumia mionzi ya Jua (Solara Power).Emanuel anasema alipata wazo hilo la kubadlishaja mfuo wa Gari kutoka kutumia mafuta na kutumia Solar Power kutokana na bei kubwa ya Mafuta inayopanda kila kukicha.Anasema imemchukua miaka miwili toka kubuni mpaka kukamilisha matengenezo.Akielezea kuhusu Gari hiyo jana kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara(Sabasaba)Emanuel anasema kuwa Gari hiyo inauwezo wa kutembea kilomita 100.Haina Injini.
Mwalimu Emanuel Bukuku, akimwelekeza Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye jinsi gari hiyo inavyozalisha nguvu za jua na uwezo wa kutembea.Nape alitembelea Maonesho ya Kimataifa ya Biashara jana kwenye Viwanja vya Mwalimu Nyerere na kufika katika Banda la VETA ndipo alipokutana na Mwalimu wa VETA na Mvumbuzi wa Gari isiyotumia Mafuta. Akizungumza baada ya Maelekezo hayo, Nape aliitaka serikali kuwekeza na kuwajali Wabunifu Wazalendo na kulinda ajira zao.Alisema kuwa kuna Vijana wenye uwezo mkubwa hapa nchini na Serikali haina haja ya kuajiri watu kutoka mataifa mengine ikiwa tuna hazina kubwa ya ujuzi, wabunifu na Wachapakazi hapa nyumbani. Nape alimpongeza Emanuel Bukuku kwa Ugunduzi huo ambao alisema kuwa ukiendelezwa utakuwa na tija kubwa kwa Taifa
Sehemu ya Nyuma ya Gari hiyo ambayo hufungwa vifaa kwa ajili na kuzalisha Nguvu za jua.Picha na Mdau Victor Makinda
No comments:
Post a Comment