KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday, 30 July 2011

Spika Anne Makinda Atembelea Ubalozi Wa Tanzania Nchini Uingereza

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda  akifurahia jinsi picha mbalimbali za Mabalozi wa Tanzania waliowahi kuhudumia Ubalozi wetu tangu Uhuru  nchini Uingereza zilivyopambwa katika ngazi za kuingia Ubalozini hapo mara baada ya kutembelea Ubalozi huo Leo. Anaemuongoza kuingia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza  Mhe. Chabaka Kilumanga.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda  akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza. Pembeni ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga aliyemkaribisha Mhe. Spika Ubalozini.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda  akizungumza na maafisa wa Ubalozi wetu Uingereza mara baada ya kuwatembelea
Mpigapicha hizi Owen Mwandumbya wa Bunge la Tanzania nae katika konooooooz na Naibu Spika wa Bunge la Uingerza  Mhe.Nigel Evance(Mb)(kushoto) pamoja na Mwenyekiti Mpya wa CPA Mhe Sir Alan Heselhurst (Mb)mara baada ya kumalizika rasmi kwa mkutano wa 57 wa CPA ambao ulifanyika London Uingereza kwa kukutanisha  Maspika, Maseneta na Wabunge zaidi ya 700 kutoka nchi 52 za Jumuiya ya Madola kujadili maswala mbalimbali yahusuyo uendeshaji wa Mabunge katika mabunge wanachama wa Jumuiya hiyo.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda  akiwa katika picha ya Pamoja na Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe. Chabaka Kilumanga pamoja na watumishi wote wa Ubalozi wetu nchini Uingereza mara baada ya kutembelea Ubalozi wetu Uingereza.

No comments:

Post a Comment