KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 7 July 2011

Kampuni Ya Bia Tanzania TBL Yaindua Kampeni Kabambe Ya Jivunie Utanzania

 Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akielezea umuhimu wa kampeni hiyo ya kuwahamasisha wananchi kuadhimisha sherehe hizo.
 Kaimu Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha na Uchumi, Geoffrey Msella (wa tatu kulia) akigongeana chupa za bia ya Kilimanjaro Premium Lager na baadhi ya viongozi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya 'Jivunie u Tanzania' jana katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam. Kampeni hiyo itakwenda sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Kutoka kushoto ni Meneja wa bia hiyo, George Kavishe, Mjumbe wa Bodi ya TBL, Ali Mwaimu, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Robin Goetzsche, Mkurugenzi wa Bodi, Alnold Kilewo, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja na Meneja Miradi Maalum wa kampuni hiyo, Emma Oriyo.
 Baadhi ya wanamuziki wakiwa miongoni mwa waalikwa katika uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Kanku Kelly, King Kiki,Ramadhan Waziri na Mabrouk Omar Mzee 'Njenje'.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.Picha na Mdau Richard Mwaikenda

No comments:

Post a Comment