KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 22 September 2011

Taswira Za Ziara Ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Huko mTarime

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akifungua kliniki ya mama na mtoto katika kituo cha afya cha kanisa Katoliki jimbo la Musoma cha Masanga wilayani Tarime. Alikuwa katika ziara ya mkoa huo Septemba 21,2011.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Sister Maria wakati alipowasili kwenye misheni ya Kanisa katoliki ya Masanga wilayani Tarime akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani Septemba 21,2011
Wasanii wa Tarime wakicheza ngoma maarufu ya Eritungu wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara katika Misheni ya kanisa Katoliki ya Masanga akiwa katika zaira ya mkoa wa Mara,Septemba 12,2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Sakata La Mkuu Wa Wilaya ya Igunga; Wanazuoni Wa Kiislamu Waivaa CHADEMA

Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimewekwa kitanzini baada ya Umoja wa Wanazuoni wa Kiislam Tanzania (HAY-AT) kutoa muda wa
siku tatu kwa viongozi wake wa taifa kulaani na kumuomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Bi. Fatma Kimario kwa kumvua sitara yake na kumdhalilisha.

Pia umoja huo umeonya kuwa iwapo CHADEMA hawatafanya hivyo wataandaa maandamano nchi nzima kutangaza chama hicho kuwa adui mkubwa wa dini hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Umoja huo, Bw. Sherally Sherally alisema kitendo kilichofanywa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA ni udhalilishaji kwa mwanamke wa kiislamu hivyo ni lazima viongozi wake wa juu walaani waliohusika na kuomba radhi.

Tayari watu watatu wakiwamo wabunge wawili wamefikishwa mahakamani mkoani Tabora wakituhumiwa kwa kumshambulia Bi. Kimario na kumwibia simu yake yenye thamani ya sh 400,000. Watuhumiwa hao waliachiwa juzi kwa dhamana hadi Agosti 10, mwaka huu.

Bw. Sherally alisema iwapo chama hicho kitapuuza agizo hilo kwa muda waliowapa umoja huo utapita nchi nzima kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo dhidi ya mwanamke.

"Tunalaani na kupinga kwa ukali kabisa kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa ni wafuasi na viongozi wa CHADEMA kumvua hijabu Bi. Kimario na kumuacha bila stara huko Igunga Septemba 15," alisema Bw. Sherally na kuongeza:

"Kitendo hiki kumvua hijabu Bi. Kimario, kumsukasuka na kumtolea maneno yasiyofaa ni kitendo kiovu sana mbele ya Mwenyezi Mungu, Waislam na Watanzania wote wapenda haki na amani na wanaojiheshimu," alisema.

Katika hatua nyingine Bw. Sherally alisema wamesikitishwa na kushitushwa na kukaa kimya kwa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na wanawake kwa kutolaani kitendo hicho cha mwanamke mwenzao kudhalilishwa kijinsia.

"Kuendelea kukaa kwao kimya kutatulazimisha kuwaona kuwa wanaafiki na ndumilakuwili," alisema.Chanzo Gazeti Majira.

Wednesday, 21 September 2011

DK. KAFUMU AHUTUBIA MKUTANO WA KAMPENI NYUMBANI KWAO ITUMBA


Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akimwombea kura mgobea ubunge wa jimbo la Igunga kwa tiketi ya Chama, Dk. Dalaly Kafumu, katika mkutano wa kamepni za CCM kumnadi mgombea wake katika Kata ya Itumba, kijiji cha Itumba alikozaliwa mgombea huyo wa CCM.
Watu wakiwa wamefurika katika mkutano ya kampeni uliofanyika Itumba kijijini kwa Dk. Kafumu.
Vijana wa Itumba wakiwa na picha ya Dk. Kafumu wakati wakiingia kwenye mkutano uliofanyika katika kata hiyo.
Maria Mgdalena, mke wa mgombea ubunge Igunga kwa tiketi ya CCM, Dk. Kafumu akiwapigia magoti wazee na vijana wa Kitaturu kumuombea kura mumewe.
Mratibu wa Kampeni za CCM, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Geofrey Kahindye (kulia) aliyehamia CCM katika mkutano wa Kampeni , Itumba.

Tuesday, 20 September 2011

MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AKUTANA NA MWAKILISHI WA KATIBU WA UMOJA WA MATAIFA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Marta Santos Pais, Mwakilishi maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na harakati za kutokomeza unyanyasaji wa watoto, wakati alipofika ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ripoti ya unyanyasaji wa watoto inayohusu hali ya Tanzania na inayotarajiwa kuwasilishwa rasmi hivi karibuni20 Septemba 2011.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais

Rais Jakaya Kikwete Atunukiwa Tuzo Nchini Marekani

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda Mh.Winston Baldwin Spencer  kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York Jumatatu usiku.
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi tuzo hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe baada ya kuipokea.Nyuma ya Mh. Membe ni Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue(kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Maajar
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa shukrani kwa kupewa tuzo hiyo. Marais Paul Kagame wa Rwanda, Abdoulaye Wade wa senegal na Mwai kibaki wa Kenya, pia walipokea tuzo kwa michango yao katika maendeleo ya nchi zao
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipewa shada ya maua kama pongezi kwa kupokea tuzo
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Dkt  Marion Bergam, Mkurugenzi wa miradi ya Health Care Projects ya Miracle Corners of the World katika mkutano wa kwanza wa kuhimiza hatua zichukukuliwe dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza,hususani ya kinywa.Serikali ya Tanzania ndiyo iliyodhamini mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha New York kitivo cha meno
 Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Dkt Asha Rose migiro kwenye hafla hiyo ya Roll Malaria
 Madaktari Bingwa kutoka Wizara ya Afya na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kugawa vipeperushi kwa wanaoingia mkutanoni
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa Makame Mnyaa Mbawala (kati), Waziri wa Maliasili na Utalii (shoto) pamoja na Mbunge wa Bukombe,Profesa Kulikoyela Kahidi wakiperuzi maandiko kuhusiana na mkutano huo wa kuhamasisha vita dhidi ya magonjwa ya kinywa
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa zanzibar Mh Juma Duni Haji (kati) na wasaidizi wake kwenye hafla hiyo
 Sehemu ya ujumbe wa Watanzania kutoka sekta ya utalii.kwa Habari na Picha Mbalimbali za Muendelezo wa Ziara ya Rais Jakaya Kikwete Nchini Marekani Endelea Kuperuzi

Ziara ya Dharura Ya Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika,Profesa Jumanne Maghembe

Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akinunua sukari ya kilombero katika Soko la Kipati, Mbagala Jijini Dar es Salaam Jana.Sukari hiyo ilikuwa ikiuzwa Shilingi 1,900 kwa kilo moja.
Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Profesa Jumanne Maghembe akipata maelezo kutoka kwa Bwana Harshid Chavda mwakilishi wa Kiwanda cha Sukari Kilombero kuhusu kiwango cha uzalishaji kwa siku na kiasi kinachouzwa kwa wasambazaji katika Mkoa wa Dar es Salaam kwa kila siku wakati Waziri alipofanya ziara ya dharura katika ofisi za kiwanda hicho,Gerezani Jijini Dar es Salaam.

Thursday, 15 September 2011

Wakuu wapya wa mikoa watangazwa

15th September 2011
  Wakuu wa wilaya 11 wapanda
  Sura mpya nne nazo zateuliwa
  Saba wastaafu, wanne kiporo
Rais Jakaya Kikwete, ameteua wakuu wa mikoa wapya 15, kati yao 11 wakiwa waliokuwa wakuu wa wilaya, wanne kutoka nje ya nafasi hizo, huku saba wakistaafu na wanne wakiachwa kwa maelezo kwamba, watabadilishwa vituo vya kazi.
Pia wakuu wa mikoa mipya minne ya Simiyu, Geita, Katavi na Njombe itakayoundwa baada ya taratibu kukamilika, watatangazwa baadaye.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Waziri Mkuu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, walioachwa, ambao watapangiwa vituo vingine vya kazi, ni Amina Mrisho aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani; Dk. James Msekela (Dodoma); Abeid Mwinyimusa (Tabora) na Daniel Ole Njoolay (Rukwa).
Waliostaafu ni Mohammed Babu (Kagera); Isidore Shirima (Arusha); Kanali Mstaafu Anatory Tarimo (Mtwara); John Mwakipesilem (Mbeya); Kanali Enos Mfuru (Mara); Brigedia Jenerali Dk. Yohana Balele (Shinyanga) na Meja Jenerali Mstaafu Said Kalembo (Tanga).
Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Singida amebaki kwenye kituo chake cha kazi wakati wakuu wa mikoa wengine wanne watapangiwa kazi nyingine.
Wakuu wa wilaya 11 waliopandishwa vyeo na kuwa wakuu wa mikoa, ni John Tupa ambaye anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara; Saidi Mwambungu (Ruvuma); Chiku Gallawa (Tanga); na Leonidas Gama (Kilimanjaro).
Wengine ni Dk. Rehema Nchimbi (Dodoma); Elaston Mbwillo (Manyara); Kanali Fabian Massawe (Kagera); na Fatma Mwassa (Tabora); Ali Nassoro Rufunga (Lindi); Mhandisi Ernest Welle Ndikillo (Mwanza) na Magesa Stanslaus Mulongo (Arusha).
Walioteuliwa nje ya nafasi hizo, ni Mhandisi Stella Manyanya (Rukwa) na aliyekuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza (Pwani).
Wengine ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera (Morogoro) na aliyekuwa Mbunge wa Kalambo (CCM-2005-2010), Ludovick Mwananzila (Shinyanga).
Waliobadilishwa vituo vya kazi, ni Abbas Kandoro anayekwenda Mbeya akitokea Mwanza; Said Mecki Sadiki anayekwenda Dar es Salaam akitokea Lindi na Dk. Christine Ishengoma anayekwenda Iringa akitokea Ruvuma.
Wengine ni Luteni Kanali Issa Machibya anayekwenda Kigoma akitokea Morogoro na Kanali Joseph Simbakalia anayekwenda Mtwara akitokea Kigoma.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakuu wote wa mikoa waliopo sasa, wameagizwa kuandaa Hati za Makabidhiano (Handing Over Notes) katika muda wa siku 14 kuanzia siku ya kuapishwa kwa wakuu wapya wa mikoa.
Taarifa hiyo pia ilieleza kuwa wakuu wa wilaya, ambao wamepandishwa vyeo kuwa wakuu wa mikoa, nao wanapaswa kufanya hivyo hivyo kwa ajili ya wakuu wa wilaya watakaopangiwa vituo vitakavyokuwa vimeachwa wazi kutokana na uteuzi wao.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakuu wa mikoa minne mipya na wakuu wa wilaya watakaoteuliwa baadaye, nao watatakiwa kuandaa Hati za Makabidhiano ndani ya siku 14 tangu kuapishwa.
“Makabidhiano hayo lazima yahusishe pia kutembelea kwa pamoja baadhi ya maeneo na miradi, ambayo ni muhimu kama sehemu ya makabidhiano yao,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa hiyo iliwataka wakuu wote wa mikoa walioteuliwa na wakuu wa mikoa minne mipya wakaoteuliwa pamoja na wakuu wote wa wilaya watakaoteuliwa baada ya zoezi kukamilika kuhudhuria mafunzo ya wiki tatu.
Mafunzo hayo yatatolewa kwenye Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, Dodoma kwa lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kiuongozi na kiutendaji.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa wakuu hao wapya wa mikoa wataapishwa kesho saa 4.00 asubuhi kwenye viwanja vya Ikulu, jijini Dar es Salaam.
CHANZO: NIPASHE

Wednesday, 14 September 2011

Mabadiliko ya Harambee Ubalozini Nchini Uingereza

Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika Jumuiya ya Watanzania nchini Uingereza TANZ- UK  inawaomba radhi wanajumuiya na watanzania wote kuwa shughuli za fund-RaƬsing zilizokuwa  zifanyike katika ubalozi wetu london siku ya jumamosi tarehe 17 septemba 2011 saa nane mchana zimeahirishwa. 

Taarifa zaidi zitawafikia hapo baadaye, tutawajulisha punde tu tutakapo pata habari kamili. Tafadhali mjulishe na mwenzako

ASANTENI
 MWENYEKITI, 
TANZ-UK

Balozi Wa Zambia Nchini Tanzania Apagawa na Ngoma Za Asili

Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mavis Lengalenga (kushoto) akicheza ngoma ya asili iliyokuwa ikitolewa na kikundi cha Sanaa cha Makanjani  kutoka nchini Zambia, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya  miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba  14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Zambia nchini Tanzania, Mavis Lengalenga(katikati) akicheza ngoma ya asili iliyokuwa ikitolewa na kikundi cha Sanaa cha Makanjani  kutoka nchini Zambia, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya  miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba  14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi Balozi wa Zambia nchini TanzaniaMavis Lengalenga, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango nchi yake katika ujenzi na maendeleo ya Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya  miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Mzee Nchimbi na mkewe wamepewa zawadi ya kusafiri na treni ya TAZARA bure katika kipindi chote cha maisha yao.
Kikundi cha Sanaa cha Makanjani kutoka nchi Zambia,  kikitoa burudani wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya  miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba  14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam.Picha Muhidin Sufiani

Viongozi na Wananchi Watembelea Makaburi Ya Wahanga Wa Meli Zanzibar

MAKABURI  ya Wahanga wa ajali meli katika Kijiji cha Kama nje kidogo ya mjini wa Zanzibar Wilaya ya Magharibi. ambayo yamezikwa jumla ya miili ya watu 46 wakiwemo Watoto 23 na watu wazima 23.  
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Pandu Ameir Kificho akiongoza na Ujumbe kutoka Arusha wa timu ya Wazee Sport Club ukiongozwa na Mwenyekiti wa timu hiyo Aatsa Atogho(kushoto), wakisoma dua katika makaburi ya wahanga wa ajali ya meli yaliyoko Kama Mkoa wa Mjini Magharibi.
MKUU wa wilaya ya Magharibi Unguja, Hassan Mussa Takrima, akitowa maelezo kwa Ujumbe wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Pius Msekwa na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mkama, walipotembelea eneo lilozikwa maiti wa ajali ya meli ya MV.Spice Kama wilaya ya Magharibi jana.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho  akiuongoza Ujumbe kutoka Arusha wa Timu ya Wazee Sport Club ukiwa na Mwenyekiti wa timu hiyo Aatsa Atogho, mwenye suti nyeusi wakizuru makaburi ya Wahanga wa ajali ya meli Kama.Picha Zote na Othman Mapara-Zanzibar

Tuesday, 13 September 2011

CUF WAZINDUA KAMPENI IGUNGA LEO HUKU WAKITOA UJUMBE MZITO KUHUSU TINDIKALI


" HATUMWAGII TINDIKALI KAMA WAO" moja wa wafuasi wa CUF akiwa na bango linalosomeka hivyo, wakati wa maandamano ya kumpokea Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya kumbukumbu ya Samora mjini Igunga mkoani Tabora. Wiki iliyopita mfuasi mmoja wa CCM alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana hata hivyo kumekuwepo kushutumiana kati ya vyama vya CCM na CHADEMA kuhusiana na tukio la kinyama lililotokea Jimboni Igunga.
Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba akiwa na mgombea Ubunge wa chama hicho Leopold Mahona kwenye mkokoteni wa punda na katika maandamano ya wanachama kwenda katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine mjini Igunga kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho.
Profesa Lipumba akizungumza jambo na mgombea ubunge wa chama cheke, Leopold Mahona.
."IGUNGA 'HATUTAKI VITA" mmoja wa wafuasi wa CUF (kushoto) akiwa na bango linalosomeka hivyo, wakati wa maandamano ya kumpokea Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ambaye baadaye alizindua kampeni za chama hicho katika viwanja vya kumbukumbu ya Samora mjini Igunga mkoani Tabora.
Mlinzi wa CUF (kulia) akiwa kazini wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho .

Kampeni Za CCM Zinaendelea igunga

Dokii, akiwajibika jukwaani.
Katibu wa Uchumi na Fedha waCCM Taifa, Mwigulu Nchemba, akipokelewa na wanachama wa CCM,alipowasili kijijini Nkinga leo mchana kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mdogo wa chama hicho.
Katibu wa Uchumi na Fedha waCCM Taifa, Mwigulu Nchemba, akihutubia wananchi wa kijiji cha Nkinga leo mchana katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Igunga. Akihutubia wananchi wa Nkinga, Nchemba aliwataka wakazi hao kumchagua mgombea wa CCM, Dr Dalali Kafumu, kuwa mbunge wao chama atokacho CCM, ndio chama pekee chenye sera  zinazotekelezeka. Aliwaasa wananchi wa Nkinga na Igunga kwa ujumla kutochagua wagombea wa vyama vya upinzania kwani vyama hivyo vipo kwa maslahi ya viongozi wake na sio kwa maslahi ya wananchi. "Ndugu zangu wana Nkinga, msithubutu kuchagua vyama vya upinzani, chagueni CCM kwa ajili ya mendeleo yenu. Chama cha CCM, ndicho chama pekee chenye sera zinazotekelezeka. Hawa wenzetu wapinzani hawa, hawana lolote. Vyama vyao ni porojo tupu. Vipo kwa maslahi ya viongozi tu na sio kwa maslahi ya wananchi wa Tanzania."
Katibu wa Uchumi na Fedha waCCM Taifa, Mwigulu Nchemba akimvisha bendera mwanachama mpya wa CCM, aliyejiunga kutoka chama cha CUF leo mchana katika mkutano wa kampeni wa kijijini Nkinga.
Hafsa Kazinja alikuwepo kutoa burudani kwa wanachama, wapenzi na mashabiki wa chama cha CCM.
Shabiki wa Chama Cha Mapinduzi akiwa kwenye Kampeni igunga.Picha Zote na Mdau Victor Makinda-igunga