KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday 6 January 2013

Rais Kikwete ahudhuria Sherehe za Kusimikwa Wakfu Askofu Dkt. Alex Seif Mkumbo wa KKKT Dayosisi ya Kati, aanza ziara ya Siku nne ya Mkoa wa Tabora.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Askofu mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo (mwenye fimbo) pamoja na viongozi wa kanisa hilo wakiongozwa na Askofu Mkuu Dkt Alex Gehaz Malasusa (kulia kwa Rais), Msaidizi mpya wa Dayosisi hiyo Mchungaji Syprian Yohana Hilinti (wa tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Kone na viongozi wengine katika sherehe ya Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013.
 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono na  kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt Alex Gehaz Malasusa baada ya kupokea kamba kama ishara ya kupokea zawadi ya ngombe toka kwa Dayosisi  hiyo huku  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo akishuhudia  katika sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na kiongozi wa kanisa la KKKT nchini  Dkt. Alex Gehaz Malasusa na  Askofu  mpya wa KKKT Dayosisi ya kati Dkt Alex Seif Mkumbo baada ya  sherehe ya  Kusimikwa Wakfu Askofu Mkumbo katika kanisa la KKKT la Singida Januari 6, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea ripoti ya mkoa wa Tabora toka kwa Mkuu wa Mkoa Mhe Fatma Mwassa huo aliyosomewa mara baada ya kuwasili kuanza ziara ya kikazi ya siku nne.(PICHA NA IKULU).

No comments:

Post a Comment