Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa akikata utepe wa uzinduzi wa maabara ya kisasa iliyogharimu milioni 49 ikiwa ni sehemu ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola  jana wilayani Uyui wakati  Waziri huyo alipotembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kushoto  ni Mbunge wa Jimbo Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar na wapili kutoka kushoto ni Kiongozi wa Mradi wa Vijiji vya Milenia wa Mbola Dkt Gerson Nyadzi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha(kulia) akitoa maelezo mafupi  jana wilayani Uyui mkoani Tabora kwa Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa(kushoto)  juu  ya mafanikio waliokwishapata katika utekelezaji malengo ya Milenia chini ya mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola. Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwenyekiti wa Halmashauri  ya Uyui Said Shaban Ntahondi.
Waziri wa Fedha Dkt William Mgimwa(kushoto) akiongea na viongozi wa vijiji 16 vinavyotekeleza  mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola  jana wilayani Uyui juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo. Katikati ni Mwnyekiti wa Halmashauri  ya Uyui Said Shaban Ntahondi na kulia ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilolangulu Ally Magoha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Uyui mkoani Tabora Said Shaban Ntahondi(kulia) akimwelezea  jana wilayani Uyui mkoani Tabora Waziri wa Fedha Dr. William Mgimwa (katikati) jinsi mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola ulivyosaidia kuboresha maisha ya wakazi wa eneo la mradi na hivyo kupunguza umaskini. Kushoto ni Mbunge wa Tabora Kaskazini Mamla Shafin  Suma.
Mbunge wa Tabora Kaskazini Mamlo Shafin Sumar (katikati) akimshukuru Waziri wa Fedha Dkt. William Mgimwa (kulia) jana wilayani Uyui kwa niaba ya wapiga kura wake kwa juhudi za serikali za kuidhinisha shilingi milioni 900 kwa ajili ya usambazaji wa umeme katika vijiji mbalimbali katika jimbo hilo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt Servacius Likwelile.
Viongozi na wananchi walioko katika mradi wa vijiji vya Milenia wa Mbola  wakimsikiliza jana wilayani Uyui juu Waziri wa fedha Dkt William Mgimwa(hayupo pichani) wakati akiwahimiza juu ya kuufanya mradi huo kuwa darasa endelevu kwa ajili ya vijiji vingine nchini kwenda kujifunza juu ya utekeleza wa malengo 8 ya Milenia . Waziri huyo alitembelea Wilaya hiyo kuona mradi wa mfano ulivyoboresha maisha ya wananchi katika vijiji 16 zinavyoteleza mradi huo.(PICHA na GCU – HAZINA).