KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 25 June 2011

Waziri Ashiriki Zoezi La Usafi Wa Mazingira . Written by haki | // 0 comments Wazir wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dk Terezya Huvisa akiangalia Uchafu Mtaa wa Toroli Chang'ombe Manispaa ya Temeke Mjini Dar es Salaam wakati aliposhiriki katika zoezi la usafi wa Mazingira Linalofanyika kila siku ya Kwanza ya Mwenzi ambalo ni agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dk Mohammed Gharib Bilali.Picha na Ali Meja Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 26 Police Arrest A Motorcyle Rider . Written by haki | // 0 comments A motorcycle rider (right) came under police arrest at the junction of Bibi Titi and Morogoro roads in Dar es Salaam on Saturday for infringing road traffic rules. Motorcycles commonly known as bodaboda have been cleared to transport passengers.Photo by Fadhili Akida Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 25 Wizara Ya Fedha Ni Ya Kwanza Kwa Ubora, Maadhimisho Ya Wiki Ya Utumishi Wa Umma . Written by haki | // 0 comments Mseamji Mkuu na Mkuu wa Mawasiliano Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingiaheri Mduma akiwa na Kombe la Ushindi wa nafasi ya Kwanza kwa Wizara zilizofanya vizuri katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma ambapo Wizara ya Fedha na Uchumi ilishinda nafasi hiyo. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dr Ally Mohamed Shein, akimkabidhi Kombe la Ushindi wa Wizara iliyofanyavizuri katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, Msemaji mkuu na Mkuu wa Mawasiliano wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingaheri Mduma jana kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Mseamji Mkuu na Mkuu wa Mawsiliano, Wizara ya Fedha na Uchumi, Ingiaheri Mduma, akiwa na Kombe la Ushindi. Kulia ni Waziri wa Nchi Menejiment ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, Kushoto ni Rais wa Zanzibar Dr Ally Mohamed Shein. Mwingine. Picha zote na Victor Makinda Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 25 Waziri Lukuvi Na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge Kutoka Dar es salaam . Written by haki | // 0 comments Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu Sera Uratibu na Bunge William Lukuvi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Msingi Bunge kutoka Dar es salaam nje ya ukumbi wa Bunge. Wanafunzi hao walikuwa bungeni Dodoma kujifunza masuala mbalimbali yanayofanywa na Bunge kufuatia mwaliko wa Spika.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 25 Lowassa ameshazungumza,Kikwete Lete Utamu Sasa Mambo Yazidi Kunoga! . Written by haki | // 0 comments Na Nova Kambota, Niliwahi kutabiri huko nyuma kuwa siku Lowassa atakapofungua mdomo wake na kuzungumza basi hali ya kisiasa ya nchi itabadilika ghafla naam! Lowassa jana sio tu amezungumza bali amezungumzia sehemu sahihi ambayo ndiyo haswa alipopaswa kuyasema aliyoyasema, nani kasema kuwa kuna baadhi ya watu hawajavutiwa na hatua hii ya lowassa? bilashaka kitendo cha lowassa kusimama upande wa wananchi kwa kuponda utendaji mbovu wa serikali huku akipandikiza moyo wa kujiamini kama taifa kwaa mfano kutumia pesa tulizonazo kutatua matatizo yetu huku akikazia kwaa kibwagaizo cha ….“tujenge reli ya kati, tupanue bandari Tanga, DSM, pesa tunazo, tumejenga UDOM kwa pesa zetu wenyewe” hali iliyofanya baadhi ya wabunge kumpigia makofi, hapa kuna siri kubwa ambayo inaturudisha kwenye swali lisilojibiwa la TATIZO NI LOWASSA AU URAIS 2015? sasa mimi nasema hivi Kikwete lete utamu sasa mambo yazidi kunoga! ila hii ni vita na hainaa macho lazima mmoja ashinde na mawingine ashindwe hivyo mwisho wa yote haya kuna mmoja atajeruhiwa tu kisiasa lakini ndiyo hivyo tena hakuna jinsi hii ni safari ya kuwaweka huru wote wawili JK na Lowassa kwani sasa kwa mbali naona wameanza sfari ndefu ya kuutafuta UKWELI. Na Novatus Kambota Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Ule Umeya Wa Arusha CCM na CHADEMA Walivyoweka Mambo Mswano . Written by haki | // 0 comments Meya wa Arusha,Gaudence Lyimo (katikati-CCM) akishikana mikono na Naibu Meya mpya, Estomih Malah (Kushoto-CHADEMA), kama ishara ya kupatana, baada ya makubaliano ya kufikiwa katika Kikao Maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Arusha, Estomih Changa'h. Meya Gaundence Lyimo CCM Naibu Meya Estomih Malah CHADEMA alipata kura 22 kati ya 25. 2 za HAPANA na Moja iliharibika Kamati Kamati ya Uchumi na Elimu: Bayo-CHADEMA Kamati ya Fedha: Lyimo- TLP Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Profesa Anna Tibaijuka Anamsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda . Written by haki | // 0 comments Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, Bungeni Mjini Dodoma Juni 24, 2011.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Rais Wa Zanzibar Dk Ali Shein Afungua Semina ya Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar . Written by haki | // 0 comments Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohamed Shein,akifungua semina ya Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,iliyoanza jana katika ukumbi wa Zazibar Beach Resort. Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Othman Masoud Othman,akitoa mada ya masuala ya sheria kwa Viongozi wa Serikali,wakati wa semina ya Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,iliyoanza jana katika ukumbi wa Zazibar Beach Resort. Baadhi ya Watendaji katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiwa katika Mkutano wa kujadili mambo mbali mbali ya kiutendaji katika sekta hizo,katika kuleta mabadiliko katika kazi za kila siku. Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Hapa Nyerere Anashambuliwa . Written by haki | // 4 comments Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni dikteta. Huu ni ukweli usiopingika. Alikuwa ni mtu ambaye hakuvumilia mawazo yake kupingwa, achilia mbali kukosolewa. Aliamini kuwa kila alichofanya na kufikiria kilikuwa sahihi na hakuna aliyeruhusiwa kukipinga. Oscar Kambona na Edwin Mtei ni mfano mzuri wa watu waliokuwa na mawazo mbadala ambao walikosana na “Baba wa Taifa”. Ilifikia wakati Nyerere alijiona kuwa na akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania na kwa bahati mbaya, Watanzania wengi waliamini hili. Matatizo mengi yanayoikumba Tanzania ni matokeo ya nchi kuendeshwa kwa miaka mingi kwa matakwa ya mtu mmoja. Pia Nyerere alikuwa ni mtu “arrogant”. Nakumbuka Nyerere akikataa kupeana mikono na Bob Marley katika sherehe za uhuru wa Zimbabwe mjini Harare mwaka 1980. Ubaguzi na udhalilishaji huu dhahiri alioufanya pale Uwanja wa Rufaro ulikuwa ni aibu kubwa kwa Tanzania. Alikataa pia kukutana na Muhammad Ali alipotembelea Tanzania mwaka 1979. Nyerere was the epitome of arrogance. Kujaribu kumweka Nyerere kundi moja na Nelson Mandela ni kushusha hadhi ya Mzee Madiba. Ni kumdhalilisha mmoja kati ya viongozi shupavu waliowahi kutokea duniani. Mandela ni mwanademokrasia halisi, tofauti na Nyerere ambaye alikuwa ni dikteta. Mandela alifungwa miaka 27 na makaburu, lakini alitoka jela akihubiri upendo, mshikamano na kusameheana. Hili lisingewezekana kwa Nyerere ambaye alikuwa ni mtu wa visasi na chuki. Wakati Nyerere alikataa kupeana mikono na Bob Marley na kukataa kuonana na Muhammad Ali, Mzee Mandela ameshakutana na idadi isiyohesabika ya wasanii na wanamichezo tangu alipotoka jela mwaka 1990. Mandela alikuwa Rais kwa miaka mitano tu kabla ya kustaafu na hata baada ya kustaafu hakuingilia mambo ya utawala kama alivyofanya Nyerere baada ya kuondoka madarakani mwaka 1985. Ilifikia wakati Nyerere alikuwa akiitisha mikutano na waandishi wa habari na kumtukana Rais Ali Hassan Mwinyi waziwazi. Nyerere alistaafu baada ya kuona Watanzania wamemchoka, lakini alitaka kuendelea kutawala akiwa nje ya Ikulu. Bado alikuwa na uchu wa madaraka. Alikuwa anataka mambo yaende anavyotaka yeye pamoja na kwamba alimkabidhi Mwinyi nchi iliyofilisika ambayo uchumi wake ulikuwa mfu na watu waliopoteza matumaini. Nyerere handed over to Mwinyi a failed state. Nani asiyekumbuka enzi za “bidhaa adimu”? Maggid nadhani unakumbuka enzi tulizokuwa tukioga kwa sabuni za mpapai na kupiga mswaki na jivu. Ni enzi ambazo tulikuwa tukivaa kandambili za ‘katambuga’ na kwenda nazo hadi katikati ya jiji bila mtu kukushangaa kwa kuwa wote tulikuwa tukizivaa. Tulikuwa tukipanga foleni masaa mengi katika jua kali kusubiri kuuziwa nusu kilo ya sukari. Hali ilikuwa hivi Dar es Salaam. Vijiji ilikuwa ni sawa na jehanam. Halafu ikaja enzi ya “wahujumu uchumi” ambapo watu waliteswa na kufungwa kwa kukutwa na dawa moja ya mswaki ya Colgate na vipande kadhaa vya sabuni ya kuogea. Hata huu ufisadi tunaouona sasa una mizizi yake katika utawala wa Nyerere. Nyerere alipiga marufuku biashara huria (free enterprise) na matokeo yake watu wakawa wanatumia rushwa kama njia ya mkato ya kujiongezea kipato. Ukienda NMC ilikuwa lazima uhonge ili upate sembe na mikate ya siha. Ukienda STC ulikuwa huwezi kupata mabati, redio au betri bila kumhonga mtu. Ni utamaduni ambao umeendelea kujengeka tangu enzi za Nyerere, ambaye tunaelezwa alikuwa akichukia rushwa. The fact is that Tanzania would have been much better off without Nyerere in the first place. His legacy is nothing to be proud of. Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Edward Lowassa Aunguruma Bungeni . Written by haki | // 0 comments Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Jimbo la Monduli Edward Lowassa akichangia bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya waziri leo.Pamoja na mambo mengine ameitaka serikali kufanya maamuzi magumu katika kutekeleza miradi mbalimbali kwa maendeleo ya wananchi.Picha na Aron Msigwa -MAELEZO. Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Rais Jakaya Kikwete Akutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la huduma za kujitolea za Wamarekani ikulu Jijini Dar es Salaam . Written by haki | // 0 comments Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Bwana Aaron Williams, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la huduma za kujitolea za Wamarekani (American Peace Corps)ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi wakati mkurugenzi huyo na ujumbe walipomtembelea na baadaye kufanya mazungumzo Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt, wakiweka saini katika ramani ya duania inayoonyesha sehemu mbali mbali duniani ambapo Shirika la huduma za kujitolea za Wamarekani(American Peace Corps volunteer) linatoa huduma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 tangu shirika hili lilipoanzishwa.Wengine katika picha aliyesimama kushoto ni Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo duniani, Bwana Aaron Wiliams, na kulia,a liyesimama ni Mkurugenzi wa shikika hilo nchini Bi.Andrea Wojnar Diagne. Shirika la Peace Corps lilianzishwa mnamo Tarehe moja Machi mwaka 1961 na aliyekuwa Rais wa Marekani hayati John F.Kennedy. Hapa nchini jumla ya wanachama 2100 wa shirika hilo walitoa huduma mbalimbali kuanzia mwaka 1961 katika sekta za Elimu, Utunzaji waMazingira na afya. Kwasasa jumla ya wanachama 140 wa shirika hilo wanafanya kazi za kujitolea katika sehemu mbalimbali nchini wakifundisha masomo ya Sayansi,Hesabu na lugha ya kiingereza.Picha na Freddy Maro-IKULU Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Idara ya Taifa ya Takwimu Yapokea Msaada Wa Magari Yenye Thamani Ya Tsh.Bilioni 1,109,502,196 . Written by haki | // 0 comments Mwakilishi wa UNFPA hapa nchini Dk.Julitta Onabanjo, akitoa hotuba fupi wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk.Albina Chuwa na Waziri waa Uchumi na Fedha, Mustafa Mkullo. Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, akikata utepe kuashiria uzinduzi wa magari hayo.Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk.Albina Chuwa na Mwakilishi wa UNFPA, Dk.Julitta Onabanjo.Picha na Mdau Richard Mwaikenda Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 SIGNING CEREMONY OF UNITED NATIONS DEVELOPMENT ASSISTANCE PLAN (UNDAP 2011-2015) IN DAR ES SALAAM... . Written by haki | // 0 comments UN Resident Coordinator Mr. Alberic Kacou discuss with some of the stake holders whose attended the Signing Ceremony of United Nation Development Assistance Plan(UNDAP 2011- 2015) held in Dar es Salaam. To the Right the Ambassador of Ireland Embassy Mr. Lorcan Fullam, next to him is Permanent Secretary Treasure Mr. Ramadhan Khijjah. The Director of International Labour Organisation (ILO) Mr. Alexio Musindo Mr.Emmanuel Kalenzi, the Representative for the United Nations Industrial Development Organisation (UNIDO). The head of Mission International Organisation for Migration (IOM) Mr. Par Liijert. The Representative of The United Nations Educational Scientific and Cultural Organisation (UNESCO) Ms. Vibeke Jensen Signing the UNDAP Agreement in Dar es Salaam. Ms. Dorothy Rozga, Representative of The United Nations Children’s Fund (UNICEF). The Permanent Secretary Treasure Mr. Ramadhan Khijjah (Centre), UN Resident Coordinator Mr. Alberic Kacou (to the Right) and The Ambassador of Ireland Mr. Lorcan Fullam (left) together Cheered the Agreement. Some of the Representatives and stake holders applaud in UNDAP Signing Ceremony UN Heads Agencies, funds and Programmes attentively listening to UN Resident Coordinator Mr. Alberic Kacou addressing the Signing Ceremony of United Nations Development Assistance Plan (UNDAP 2011-2015) in Dar es Salaam. Front Line (From Left to the Right) The Ambassador of Ireland Mr. Lorcan Fullam, The Permanent Secretary Treasure Mr. Ramadhan Khijjah and UN Resident Coordinator Mr. Alberic Kacou taking picture with Heads of UN Agencies after UNDAP Signing Ceremony.Photo By Zainul Mzige Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL AWEKA SAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA RAIS WA ZAMANI WA ZAMBIA . Written by haki | // 0 comments 1:- Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha aliyekuwa rais wa zamani wa Zambia, Frederick Chiluba, aliyefariki hivi karibuni. Makamu wa Rais alifika kuweka saini katika kitabu hicho kilichopo katika makazi ya Balozi wa Zambia nchini, jijini Dar es Salaam leo Juni 24. Picha na Amour Nassor-Ofisi Ya Makamu Wa Rais Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 FFU wa Ngoma Africa band Jukwaani 25.06 na 26.06.2011 . Written by haki | // 0 comments FFU wa Ngoma Africa band jukwaani ! Jumamosi 25.06.2011 Heidelberg na Jumapili 26.06.2011 Freudenstadt City, nchini Ujerumani Bendi ya maarufu ya mziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band" aka FFU yenye makao yake nchini ujerumani,inatarajiwa kupanda jukwaani siku ya jumamosi 26.06.2011 katika onyesho kambambe mjini Heidelberg,ujerumani.Pia siku ya jumapili 26.06.2011 Kikosi kazi hiko cha FFU wa Ngoma Africa band,kitaelekeza mashambulizi yake ya mziki katika oynesho lingine "Afrika Tage" mjini Freudenstadt,kusini mwa Ujerumani ambako mshike mshike wa pata shika ya nguo kuchanika ya washabiki na gwaride la mziki "bongo dansi" utakuwapo,Pia karandinga la FFU wa ngoma africa limeegesha hapa unaweza kuchungulia virungu na vya machozi ya mziki Hapa....>>>> Jipendelee kwa kujipa raha mwenyewe kwa kukongoli au bofya at www.ngoma-africa.com Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Pata Ufumbuzi na Elimu ya Afya . Written by haki | // 0 comments Katika kuhakikisha elimu ya Afya inamfikia mlengwa kiurahisi zaidi,timu nzima ya TanzMED,imefanya mabadiriko makubwa katika tovuti yake ya tanzmed.com, Hii ni hatua muhimu ambayo itamuwezesha mwanajamii wa Kitanzania; -Kuuliza maswali ya afya moja kwa moja kwa kutumia TanzMED Forums -Kuwasiliana na kufuatilia muendeleo(feedback) wa tatizo lako kwa kutumia mtinfo wa tiketi,Tuma tiketi -Kujumuika,kubadilishana mawazo,matukio,picha nk na wanajamii wa TanzMED -Tuma,tafuta au toa ushauri juu ya huduma mbalimbali za afya kwa kutumia Kitabu cha njano -Pata taarifa(Zenye uhusiano na afya) juu ya skolashipu,kazi,mishusho,blogs nk -Mafundisho ya mapishi,sayansi ya chakula,urembo na ushauri nasaha -Tuma maoni moja kwa moja juu ya masuala ya afya yanayokutatiza Jali Afya yako,Tembelea TanzMED Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Wizara ya Fedha Yalamba Tuzo Wiki Ya Utumishi Wa Umma . Written by haki | // 0 comments Baadhi ya wafanyakazi wa Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dar es salaam mara baada ya kushinda ushindi wa kwanza kwa Wizara na pia mshindi wa tatu kwa banda bora. Msemaji wa Wizara ya Fedha Ingiahedi Mduma akionyesha kikombe cha ushindi wa kwanza wa utoaji wa huduma nzuri wa Wizara wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yalimalizika Juni23,2011 Wengine ni Maafisa habari Eva Varerian na Richard Cheyo.Picha na Wizara ya Fedha Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 24 Ombi la Hussein Bashe Kwa Wabunge Wa CCM Kuhusu Posho . Written by haki | // 2 comments Hussein Bashe ------- Ombi Langu kwa wabunge wa chama changu, si kila jambo kulipinga swala la Posho (sitting allowance) hakuna sababu ya kulivalia njuga na kulazimisha kulipata,wabunge wanapata Mshahara,posho ya kuwa nje ya kituo ,posho ya ubunge FEDHA HIZI zinawatosha ukiangalia hotuba ya zito tunasema pato la mtanzania ni 770,000 lakini kuna asilimia 20% ambao wanashikilia 42% ya pato la taifa (32trillion) kati ya hizo wakati 20% ya masikini wa chini kabisa wanashikilia only 7% ya pato la Taifa. Kwa mtazamo wangu ikiwa sitting allowance ambayo kwa ujumla wake ikipunguzwa tuta save 900bn fedha hizi zikiamuliwa kupelekwa katika sekta ya ELIMU kuondoa kero ya waalimu kuishi madarasani kwa kuwajengea nyumba, kwa majirani,ama kuondoa kero ya Mabweni ktk shule za kata,ama kuondoa kero ya MAABARA katika shule za kata,ama kupelekwa katika sekta ya Afya , tutakuwa kama Taifa tutamaliza tatizo kubwa sana tutaipunguzia serekali na walipa kodi mzigo wa fedha ambazo haziendi katika shughuli za maendeleo,Niwaombe wasiitazame hoja imetoka kwa nani wa chama gani waipokee na kuiunga mkono Mtakuwa mmeitendea HAKI nchi yetu,na watanzania ambao mustakabali wa maisha yao katika miaka mitano ijayo upo mikononi mwa serekali ya CCM (cham chetu) hata kama kama mnaipata kwa mujibu wa sheria na kanuni fanyeni cost benefit analysis kwa kuliangalia taifa na si nyinyi peke yenu.kama taifa tutfaidika zaidi fedh hizi msipopokea na kuamua kama bunge zipelekwe katika shughuli za maendeleo. Wapo wabunge ambao wana jenga Hoja ya kwamba Posho hizo zinawasaidia ktk shughuli za Majimbo, inawezekana inaukweli,lakini kama MFUKO WA MAENDELEO WA JIMBO ,POSHO YA UBUNGE 5M,ALLOWANCE YA KUKAA NJE YA JIMBO 80,000,MSHAHARA 2M vyote hivi vimeshindwa kukusaidia kuhudumia Jimbo basi hata hiyo Posho haita weza,naamini mnatuongoza tutawaona si wabinafsi mkiunga mkono hili kwani mnachpata kwa maisha yenu kinawatosha. Itendeeni haki Nchii hii katika kipindi hiki ambachi ambacho maisha yanazidi kuwa magumu shilingi inashuka, kuna vijana wenzetu million 11 wanahitaji msaada waliopo mashuleni na vyuoni wanahitaji msaada wenu mtakuwa mmetenda haki sana kwa kusamehe hicho kidogo,nimuombe Mbunge wangu aunge Mkono kusamehe hiyo Posho 70,000 ni Tofali 350 za kuchoma kwa bei ya kule kwetu ,mara siku za vikao ,ni fedha nyingi tutapata mabweni, maabara,ama fedha hiyo utakuwa umesaidia vijana wengi kulipiwa ada ktk shule za Kata. Kwahiyo ni vizuri likaungwa mkono jambo hili ili kuisaida Nchi Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 23 Kuhusu Upatikanaji Wa Dawa Mseto . Written by haki | // 0 comments Katibu mkuu wa wizara ya Afya ustawi wa jamii Bi. Blandina Nyoni akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana jijini Dar es salaam juu ya upatikanaji wa dawa mseto za kutibu ugonjwa wa malaria kwa gharama nafuu katika sekta binafsi tanzania bara lengo kuu ni kuhakikisha kuwa wananchi wote hapa nchini wanapata tiba sahihi ya malaria kwa gharama nafuu.Picha na Philemon Solomon Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 23 Uhaba wa Madawati Nchini na Ubunifu Wa Madawati Ya Saruji . Written by haki | // 0 comments HIVI karibuni asasi ya kiraia ya Twaweza kupitia programu yake ya Uwazi,ilifanya utafiti katika jiji la Dar es Salaam na kubaini upungufu mkubwa wa madawati katika shule za serikali. Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo uliohusisha sampuli ya shule za msingi 40 katika manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni, karibu nusu ya shule hizo hazina madawati ya kutosha, hali inayowalazimu wanafunzi kukaa sakafuni. Na hata katika shule zilizo na madawati, wanafunzi wanalazimika kukaa watano katika dawati moja ambalo kimsingi linapaswa kukaliwa na wanafunzi wasiozidi watatu. “Katika takribani nusu ya shule(18 kati ya 40), hapakuwa na madawati ya kutosha kwa wanafunzi wote, wengi wanalazimika kukaa chini…..,” inasema sehemu ya ripoti ya utafiti. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ukosefu wa madawati ni tatizo kubwa katika Shule ya Msingi Kunduchi ambapo, robo tatu ya wanafunzi 1,931 katika shule hiyo hawana madawati. Pichani unaweza kuona ubunifu wa aina yake wa madawati ya saruji yaliyojengewa ndani ya darasa kama suluhisho la tatizo hilo. Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 23 Kuhusu Mkutano wa Tatu wa Afrika wa Kujadili Maendeleo ya Elimu Huria na Elimu Masafa . Written by haki | // 0 comments Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania(OUT),Profesa Tolly Mbwette(kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam , kuhusu maandalizi ya mkutano wa tatu wa Afrika wa kujadili maendeleo ya Elimu Huria na Elimu Masafa itakayoanza Julai 12-15, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Elifas Bisanda ambaye ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo hicho (Taaluma).Picha na Richard Mwaikenda Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 23 Mustapha Sabodo inaugurate a Well at Maweni School For the Deaf in Kigamboni . Written by haki | // 0 comments MR Mustapha Sabodo turns on a water tap to inaugurate a well at Maweni School for the deaf in Kigamboni, Dar es Salaam. Centre (in glasses) is the Director of Aqua Well Drilling, Mr Ismail Mohamed.Photo by Yusuf Badi Email This BlogThis! Share to Twitter Share to Facebook Share to Google Buzz Jun 23 MSIBA LEICESTER UINGEREZA...! . Written by haki | // 0 comments Marehemu Edgar Kileke Ndugu, Jamaa, na Marafiki, Watanzania wote; Kwa masikitiko makubwa tunawataarifu ya kwamba, tumepokea habari za msiba wa mwenzetu EDGAR KILEKE (KAKA DICK). Msiba umetokea leo huko Leicester Uingereza. Marehemu Edgar amefariki baada ya kuugua cancer ya Ini. Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kueleke anyumbani kwa mazishi inafanyika. Tunawaomba wote, kwa moyo wa upendo na utoaji, tusaidiane ili tukamilishe maandalizi haya na mwenzetu ili aweze kwenda kupumzishwa kwenye makao yake ya milele huko nyumbani Tanzania. Tunatanguliza shukurani za dhati kwa michango yenu. Wanaoweza kuwatembelea wafiwa na kutoa pole mnakaribishwa na msiba upo kwenye address hapo chini: 89 Stevenson Drive LE3 9AD Leicester Kwa maelezo ya ziada wasiliana na; Asaa Ali 07951644936 au Fauzia Musa 07943962628 Kama hutaweza kufika Leicester, unaweza kutuma mchango wako kwa: A A KAKOZI Account Num

No comments:

Post a Comment