KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 25 June 2011

Nyerere Anashambuliwa

Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni dikteta. Huu ni ukweli usiopingika. Alikuwa ni mtu ambaye hakuvumilia mawazo yake kupingwa, achilia mbali kukosolewa. Aliamini kuwa kila alichofanya na kufikiria kilikuwa sahihi na hakuna aliyeruhusiwa kukipinga. Oscar Kambona na Edwin Mtei ni mfano mzuri wa watu waliokuwa na mawazo mbadala ambao walikosana na “Baba wa Taifa”.

Ilifikia wakati Nyerere alijiona kuwa na akili kuliko mtu mwingine yeyote Tanzania na kwa bahati mbaya, Watanzania wengi waliamini hili. Matatizo mengi yanayoikumba Tanzania ni matokeo ya nchi kuendeshwa kwa miaka mingi kwa matakwa ya mtu mmoja.

Pia Nyerere alikuwa ni mtu “arrogant”. Nakumbuka Nyerere akikataa kupeana mikono na Bob Marley katika sherehe za uhuru wa Zimbabwe mjini Harare mwaka 1980. Ubaguzi na udhalilishaji huu dhahiri alioufanya pale Uwanja wa Rufaro ulikuwa ni aibu kubwa kwa Tanzania. Alikataa pia kukutana na Muhammad Ali alipotembelea Tanzania mwaka 1979. Nyerere was the epitome of arrogance.

Kujaribu kumweka Nyerere kundi moja na Nelson Mandela ni kushusha hadhi ya Mzee Madiba. Ni kumdhalilisha mmoja kati ya viongozi shupavu waliowahi kutokea duniani. Mandela ni mwanademokrasia halisi, tofauti na Nyerere ambaye alikuwa ni dikteta. Mandela alifungwa miaka 27 na makaburu, lakini alitoka jela akihubiri upendo, mshikamano na kusameheana. Hili lisingewezekana kwa Nyerere ambaye alikuwa ni mtu wa visasi na chuki. Wakati Nyerere alikataa kupeana mikono na Bob Marley na kukataa kuonana na Muhammad Ali, Mzee Mandela ameshakutana na idadi isiyohesabika ya wasanii na wanamichezo tangu alipotoka jela mwaka 1990.

Mandela alikuwa Rais kwa miaka mitano tu kabla ya kustaafu na hata baada ya kustaafu hakuingilia mambo ya utawala kama alivyofanya Nyerere baada ya kuondoka madarakani mwaka 1985. Ilifikia wakati Nyerere alikuwa akiitisha mikutano na waandishi wa habari na kumtukana Rais Ali Hassan Mwinyi waziwazi. Nyerere alistaafu baada ya kuona Watanzania wamemchoka, lakini alitaka kuendelea kutawala akiwa nje ya Ikulu. Bado alikuwa na uchu wa madaraka. Alikuwa anataka mambo yaende anavyotaka yeye pamoja na kwamba alimkabidhi Mwinyi nchi iliyofilisika ambayo uchumi wake ulikuwa mfu na watu waliopoteza matumaini. Nyerere handed over to Mwinyi a failed state.

Nani asiyekumbuka enzi za “bidhaa adimu”? Maggid nadhani unakumbuka enzi tulizokuwa tukioga kwa sabuni za mpapai na kupiga mswaki na jivu. Ni enzi ambazo tulikuwa tukivaa kandambili za ‘katambuga’ na kwenda nazo hadi katikati ya jiji bila mtu kukushangaa kwa kuwa wote tulikuwa tukizivaa. Tulikuwa tukipanga foleni masaa mengi katika jua kali kusubiri kuuziwa nusu kilo ya sukari. Hali ilikuwa hivi Dar es Salaam. Vijiji ilikuwa ni sawa na jehanam.

Halafu ikaja enzi ya “wahujumu uchumi” ambapo watu waliteswa na kufungwa kwa kukutwa na dawa moja ya mswaki ya Colgate na vipande kadhaa vya sabuni ya kuogea. Hata huu ufisadi tunaouona sasa una mizizi yake katika utawala wa Nyerere. Nyerere alipiga marufuku biashara huria (free enterprise) na matokeo yake watu wakawa wanatumia rushwa kama njia ya mkato ya kujiongezea kipato. Ukienda NMC ilikuwa lazima uhonge ili upate sembe na mikate ya siha. Ukienda STC ulikuwa huwezi kupata mabati, redio au betri bila kumhonga mtu. Ni utamaduni ambao umeendelea kujengeka tangu enzi za Nyerere, ambaye tunaelezwa alikuwa akichukia rushwa.

The fact is that Tanzania would have been much better off without Nyerere in the first place. His legacy is nothing to be proud of.

No comments:

Post a Comment