Rais Kikwete: Nasikia Dk.Slaa umekuwa ukinipiga chenga tusisalimiane?
Dk.Slaa:Mh,ulitaka vijana wako wa usalama wanikamate kwa kuvunja itifaki?
Naam,ni jana tu wote tumesikia habari za watu hawa wakubwa kukwepana na au kutosalimiana.Wengine wetu tulidhani ni mambo yalee ya uchaguzi. Ufafanuzi ukatolewa na wengi wetu tukadhani ni uongo wa wanasiasa.Leo picha hii halisi kabisa(siyo ya kutengenezwa) inaonyesha waheshimiwa hawa wakishikana mikono tena kwa tabasamu kuu.Ikiwa hili ni tabasamu la kweli litokalo moyoni au ni mambo ya kwetu kutabasamu ili ionekane vizuri wakati ndani ni chuki siyo rahisi kujua.Tunachojua ni kwamba viongozi hawa hawakujali maneno yaliyokuwepo kuhusu wao.Tunashawishika kudhani kuwa kuna jambo zito kabisa kati yao na kwa taarifa zilizoambatana na picha za ikulu inahusu mambo ya katiba.Je Wakati huu kutakuwa na maelewano kati ya serikali na CHADEMA? na je ni sahihi kwa chama kilichosema kilidanganywa mara ya kwanza na kutangaza kutoshiriki jambo hilo kama serikali italipeleka bila kuzingatia matakwa yao kurudi tena ikulu kwa mazungumzo hayohayo? nini kimebadilika mpaka wadhani kuwa wakati huu watasikilizwa? TUSUBIRI TUONE
Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar es salaam
No comments:
Post a Comment