KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday, 22 January 2012

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI WA CHIUMBATI , APOKEA KADI YA MWENYEKITI WA CHADEMA (W) NACHINGWEA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wakati alipotembelea mradi wa maji wa Chiumbati, Nachingwea, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana, januari 20.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Nachingwea, wakati alipokuwa akiondoka katika mradi wa maji wa Chiumbati jana, januari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment