Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa maziko. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Kiongozi wa Upinzani Bungeni Mh. Freeman Mbowe akitoa salam zake za pole kwa familia ndugu na jamaa wa Marehemu Regia Mtema. Picha Owen David
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali. Picha na Muhidini Sufiani wa OM
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa mare hemu katika shughuli zake za kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.
Viongozi mbalimbali wakitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Regia Mtema kutoka kulia ni Mama Tunu Pinda, Naibu Spika wa bunge Job Ndugai, Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta na Kiongozi wa upinzani Bungeni Freeman Mbowe.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Sadick Meck, Waziri wa Nchi Ofisi ya waziri Mkuu, sera Uratibu na Bunge Mhe. William Lukuvi pamoja na Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe wakimsubiri makamu wa Rais leo katika viwanja vya karimjee kuaga mwili wa Mbunge wa Chadema Viti Maalum Marehemu Regia Mtema aliyefariki kwa ajali ya gari Jumamosi tarehe 14, 2012 Picha na Owen David
Kutoka kulia ni Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitta, Mama Tunu Pinda mke wa Waziri Mkuu, Mwantumu Mahiza Mkuu wa mkoa wa Pwani na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai. Picha Owen David
Askari wa Bunge wakibeba Jeneza kuelekea mahala palipoandaliwa rasmi kwa ajili ya shughuli za kuaga.
Waombolezajio wakishuhudia mwili wa marehemu Regia Mtema wakati alipowasili kwenye viwanja vya Karimjee tayari kwa kuagwa leo.
No comments:
Post a Comment