Maelfu ya wananchi wa mji wa Ifakara wakiwa barabarani ambako walizuia ambulance iliyobeba mwili wa marehemu.Kwa mujibu wa wenyeji, haijawahi kushuhudiwa mapokezi kama haya katika msiba wowote ule katika historia ya mji huu.Mwenyekiti wa CHADEMA taifa alilazimika kuwaomba vijana kutulia kwani walikuwa wamejawa na jazba na taharuki.Baada ya mwili kuingizwa katika nyumba ya familia kwa muda, ulihamishiwa hospitali hadi baadaye utakapotolewa kwa ratiba nyingine.Msafara kutokea Dar es salaam uliwasili Ifakara saa 4 usiku na maandamano yaliuchelewesha kufika nyumbani kwa marehemu.wageni kutoka dar es salaam walifika ndani saa 5 usiku.Msafar kutoka Dar es salaam ulikuwa na magari yapatayo 60,ambayo mwandishi wa habari hii aliweza mwenyewe kuhesabu.Tutaendelea kuwahabarisha kutokea Ifakara.
No comments:
Post a Comment