KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Sunday, 29 January 2012

Liverpool 2 Manchester United 1: Kuyt strikes to bury United at bitter end

Last off the pitch was Jamie Carragher as the spontaneous chorus of You'll Never Walk Alone echoed around a glorious Anfield bathed in winter sunshine.

No matter that Carragher had been withdrawn after 63 minutes, long before the explosive winning goal was scored by Dirk Kuyt.
Dutch of class: Dirk Kuyt blasted Liverpool into the fifth round of the FA Cup
Dutch of class: Dirk Kuyt blasted Liverpool into the fifth round of the FA Cup

MATCH FACTS

Liverpool: Reina,Skrtel,Carragher (Kuyt 63),Agger,Kelly, Henderson,Gerrard (Bellamy 72),Jose Enrique, Downing, Carroll, Maxi (Adam 63) Subs Not Used: Doni ,Johnson, Coates, Shelvey.
Goals: Agger 21,Kuyt 88.
Man Utd: De Gea,Rafael Da Silva, Smalling, Evans, Evra, Scholes (Hernandez 76), Carrick, Giggs (Berbatov 90),Valencia, Welbeck, Park. Subs not used: Lindegaard, Ferdinand, Fabio Da Silva, Michael Keane, Pogba.
Goals: Park 39.
Booked: Rafael Da Silva.
Att: 43,952
Ref: Mark Halsey (Lancashire).
Last off the pitch was Jamie Carragher as the spontaneous chorus of You'll Never Walk Alone echoed around a glorious Anfield bathed in winter sunshine.

No matter that Carragher had been withdrawn after 63 minutes, long before the explosive winning goal was scored by Dirk Kuyt.

The veteran defender is the closest thing to the personification of Liverpool Football Club and yesterday was one of those days when that club could believe in itself again.

They have a Wembley date in the Carling Cup final to look forward to and now passage to the fifth round of the FA Cup. They may even start eyeing a double on Merseyside, and all this just a week after the abject capitulation at Bolton.

Yesterday, though, by the time Carragher had reached the tunnel, the fans' chants had changed from Anfield's traditional anthem to their playful song celebrating Luis Suarez.

That gave the impression that, for some, this fixture was seen as some kind of rematch of the FA disciplinary hearing which found Suarez guilty of racially abusing Patrice Evra at this ground in October and banned him for eight games, including this one.

Why else chant the name of a player who has made no contribution to the match?
It was, of course, inevitable that such a highly contentious issue would stalk this match.
First blood: Daniel Agger powered home from a corner to hand Liverpool the lead
First blood: Daniel Agger powered home from a corner to hand Liverpool the lead
First blood: Daniel Agger powered home from a corner to hand Liverpool the lead
First blood: Daniel Agger powered home from a corner to hand Liverpool the lead

 
It was, of course, inevitable that such a highly contentious issue would stalk this match.
Kenny Dalglish was right to point out that both clubs had done much to limit the vitriol in the run-up to the game; but he was wrong to suggest: 'Both sets of supporters were magnificent.'

It was not as bad as some feared but there were chants from the United end of 'racist b******' and 'self-pity city', while Evra, the injured party in all this, was booed throughout and traduced as a 'lying b******'.

Dalglish was incredulous when it was suggested he or anyone might be disappointed by that. 'Have you played football?' he asked. 'I've been booed.'

It is impossible to say whether the abuse affected Evra's game but he was badly out of position when, from Pepe Reina's goal-kick with two minutes remaining, Andy Carroll flicked the ball on for Kuyt, who was inside Evra and had a clear run at goal, to finish.
Goal time: David de Gea was questionably positioned for the opener
Goal time: David de Gea was questionably positioned for the opener

 
David de Gea, who had a miserable afternoon on his return to the United team, might have saved his team but was wrong-footed and beaten at the near post.

'I don't know how we lost it,' said Sir Alex Ferguson, who described defeat as a 'devastating blow'.

For Dalglish it was 'a fantastic effort' after the draining semi-final on Wednesday. And unlike last weekend, when he attacked his own side's commitment, yesterday he said: 'I can't speak highly enough of them.'

In truth, the result was an aberration in some respects, as for long periods United had controlled the game with Michael Carrick, Paul Scholes and Ryan Giggs unfazed in midfield.
Sideshow: Manchester United's Patrice Evra had to put up with jeers from the crowd
Sideshow: Manchester United's Patrice Evra had to put up with jeers from the crowd
Rafael had a superb game at right-back while Antonio Valencia was often dangerous, never more so than on 18 minutes when he went past a sprawling Maxi Rodriguez and crashed a shot against the post.

That was just prior to Liverpool's opening goal on 20 minutes. Steven Gerrard's driven corner required a strong presence but De Gea approached his task tentatively and collided with the immovable object that is Carroll.

No prizes for guessing who came off best. While De Gea was politely attempting to reach the ball, Daniel Agger rose to head firmly home.

Anfield roared but Liverpool retreated, dropping so deep that they were encamped on the edge of the penalty box, a tactic that might have been commendable had they been able to maintain concentration until half-time at least.

Striker: Park Ji-sung hauled Manchester United level before the break
Striker: Park Ji-sung hauled Manchester United level before the break
Level pegging: Park (obscured) fired United level before the break
But an opportunistic backheel from Valencia caught Jose Enrique dithering in the left-back position, a weakness the excellent Rafael pounced upon, winning the ball and racing to the byline to pull a smart ball back for Ji-Sung Park.

The Korean met it first time, driving into the near corner so quickly that Reina barely had time to react.
United continued the second half as they had finished the first - on top - but for all their possession there was precious little end product.

Carragher, playing in holding midfield, was effective in that respect but when he came off and Kuyt and, later, Craig Bellamy came on, Liverpool looked more dangerous than ever.

Watching on: Luis Suarez, serving his suspension for racially abusing Evra, was in the stands
Watching on: Luis Suarez, serving his suspension for racially abusing Evra, was in the stands
Carroll, in particular, came to life, thriving on the support and looking more confident, as he demonstrated in setting up the goal.

He might have added a third right on 90 minutes when his header at the far post crashed against the upright and Kuyt steered the ball wide from the rebound.

There will be no eulogies for Carroll yet, however.
Dalglish said he would receive a simple: 'Well done.'

Atmosphere: The Liverpool fans created a thunderous level of noise throughout the match
Atmosphere: The Liverpool fans created a thunderous level of noise throughout the match
Dalglish added: 'He's got to develop and he's got to work within a framework. And we'll be a lot more patient than many other people. I'm sure we'll get the rewards in the end.'

Yesterday, though, they got some immediate returns.

Urais CCM 2015 Ni Balaa ( GAZETI MWANANCHI)


KIGOGO AMWAGA MAMILIONI, ATUMA MAKADA MIKOANI KUMNYOSHEA NJIA
 Na Mwandishi Wetu
WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikionya wanachama wake kuacha ndoto za urais wa mwaka 2015, kauli hiyo sasa imeonekana kupuuzwa na kugeuka kichocheo cha kuongeza kasi ya kujipanga kwa baadhi ya makada wenye nia ya kusaka nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa taifa.
 
Hivi karibuni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye, alionya kwamba chama hicho hakiko tayari kuendelea kuwakumbatia wanachama wake wanaunda makundi ndani ya chama, kwa lengo la kusaka umaarufu wa kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2015
.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, Nape alisisitiza kuwa endapo mwanachama yeyote atabainika kuvuruga mshikamano ndani ya chama kutokana na kigezo hicho, CCM haitasita kuchukua hatua kali dhidi yake. 
 
Pamoja na CCM kutoa onyo hilo kali, mbio za urais wa mwaka 2015 ndani ya chama hicho, zimeelezwa kuingia katika sura mpya baada ya mmoja wa makada anayetajwa kuwania nafasi hiyo, kufanya kikao kizito jijini Arusha, kwa lengo la kuweka mikakati ya kujipanga na kuimarisha kambi yake.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na baadhi ya wana CCM mjini Arusha, zinaeleza kuwa, kigogo huyo alifanya kikao chake wiki chache zilizopita katika moja ya majengo ya mfanyabiashara mmoja kutoka Kanda ya Ziwa, yaliyopo nje kidogo ya jiji.
Kikao hicho kilichohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini, wakiwamo baadhi ya wenyeviti wa mikoa wa chama hicho na baadhi ya viongozi wa Serikali, pamoja na mambo mengine, kilifanya tathmini ya kina kujua maeneo ambayo mgombea huyo hakubaliki.
Chanzo chetu kilidokeza kwamba tathmini hiyo ilionyesha kuwa kada huyo hakubaliki sana katika mikoa ya Lindi , Mtwara pamoja na maeneo ya mikoa ya Kanda ya Ziwa, ukiwemo Mkoa wa Mara.
Kutokana na hali hiyo, ilikubaliwa kuwa fedha nyingi zitumike na watu mahiri wenye ushawishi, watumwe katika maeneo haya ili kuwalainisha baadhi ya viongozi wa CCM ambao wanaonekana kuwa mbali na mgombea huyo, na jambo hilo lifanyike haraka kabla ya kuanza kwa chaguzi mbalimbali ndani ya CCM mwaka huu. 

Kauli ya Nape 
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipoliuzwa kuhusiana na kikao hicho, alisema hana taarifa zozote lakini alionya kuwa endapo itathibitika kuwa kuna makada wa chama hicho wanafanya ‘rafu’ hizo, watachukuliwa hatua za kisheria za chama kwani huu si muda wa kufanya kampeni za urais. 

Aliwataka wanachama wa CCM kuipa nafasi  Serikali yao kutekeleza majukumu yake na ilani kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania.
Awali, pia Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi, aliwahi kukaririwa akisema kuwa wanaotarajia kutumia fedha kupata urais kupitia chama hicho wanajidaganya, ni bora watafute kazi nyingine za kufanya.


 Kikao cha mkakati 
Habari zaidi kutoka ndani ya kikao hicho, zililidokeza Mwananchi Jumapili  kuwa makada watakaotumwa kuzunguka mikoani, baada kukamilisha kazi yao, watatakiwa  kurejesha ripoti itakayofanyiwa kazi, ili kundi hilo liweke mikakati zaidi ya kufanikisha lengo lake.
Inaelezwa kuwa hofu kuu ya kundi hilo, ni kutoka kwa baadhi ya makada wengine wa CCM, wanaotajwa kuonyesha nia ya kuwania nafasi ya urais, kukubalika zaidi ndani ya chama katika mikoa hiyo, ambapo baadhi yao  wanatoka huko.
Chanzo chetu kilidokeza pia kuwa mbali ya kuweka mikakati hiyo kabambe ya kuwania urais, pia wajumbe wa kikao hicho ‘kizito’, walifanyiwa sherehe kubwa ambapo nyama na vinywaji mbalimbali vilimwagwa kwa wingi, ndani ya majengo ya mfanyabiashara huyo, ambayo yamezungushiwa ukuta mrefu.
“Aisee! kikao kilikuwa kizito mno mikakati mizito imewekwa , jamaa yuko serious (makini) kuutaka urais, “alidokeza kada mmoja aliyekuwa ndani ya kikao hicho kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa tayari, makada waliotumwa kwenda mikoani ‘kumnyoshea njia’ mgombea huyo wa urais, hivi sasa wanavinjari kwenye maeneo hayo, wakiwa na fedha za kutosha na vitendea kazi vingine, yakiwemo magari ya uhakika.
Waliotumwa kufanya kazi hiyo, ni wenyeviti  wa baadhi ya mikoa ambao imeelezwa kuwa watatumia nafasi zao kufanya ushawishi huo kwa urahisi.
Ingawa hadi sasa hakuna kada ndani ya CCM ambaye ametangaza hadharani  kutaka kuwania urais, inadaiwa kwamba.... Soma zaidi; http://www.mwananchi.co.tz

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AMALIZIA ZIARA YA MKOA WA TANGA, WILAYANI LUSHOTO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikagua jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto baada ya kuweka jiwe la Msingi katika jengo hilo lililopo Chakechake Lushoto jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Sophia Mjema

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia na kuwaaga wasanii waliokuwa wakitoa burudani, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga.
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mkulima wa Nyanya, Judith Munis, wa Kikundi cha Upendo Jegestal, kuhusu kilimo cha nyanya, wakati alipotembelea wakulima wa Kituo cha Habari na Mafunzo (Shamba Darasa) cha Jegestal-Lushoto, jana Januari 27, 2012, akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasalimia na kuwaaga wasanii waliokuwa wakitoa burudani, wakati akiondoka Chakechake baada ya kuweka jiwe la Msingi katika Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, jana Januari 27, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Tanga. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

RAIS DK. JAKAYA KIKWETE KATIKA MKUTANO WA (WORLD ECONOMIC FORUM) JIJINI DAVOS


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Bill and Melinda Gates Foundation Bw. Bill Gates wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Bw. Kevin Rudd wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo na Waziri Mkuu wa Thailand Bi. Yingluck Shinawatra wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Walmart Bw Doug Mc Millon
wakati wa Kongamano la Uchumi Duniani mjini Davos, Switzerland
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Madame Sadako Ogata, Rais wa Japan International Cooperative Agency mjini Davos
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Waziri Mkuu wa Kenya Mh Raila Odinga baada ya kufanya naye mazungumzo mjini Davos
Rais Jakay Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron mjini Davos, Uswisi

(PICHA NA IKULU)

Rais Dk. Jakaya Kikwete akutana na mkuu wa Vodafone


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw.  Vittorio Colao katika Hoteli ya Sheraton Waldhuus, Mjini Davos, Uswisi, Viongozi hao wawili wanahudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani unaofanyika mjini Davos na mazungumzo yao yaliangaza dhamira ya Vodafone ya kuongeza uwekezaji katika kusaidia ustawi wa jamii nchini na kuunga mkono juhudi za serikali ya Tanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na kufanya mazungumzo mafupi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vodafone Bw. Vittorio Colao mjini Davos, Uswisi.
Vodafone ndio wanahisa wakuu wa kampuni ya Vodacom Tanzania.
Bw Colao ambae anahudhuria mkutano wa Uchumi wa Ulimwengu – WEF mjini Davos kama ilivyo kwa Rais Kikwete walipata nafasi ya kukutana na kufanya mazungumzo hayo katika hoteli ya Sheraton Waldhuus.
Mazungumzo hayo yaligusia mahusiano ya Vodafone na seriklai ya Tanzania na watu wake hususan katika uwekezaji katika jamii kusaidia kukuza,kuimarisha na kuboresha huduma za kijamii nchini ikiwa ni utekelezaji wa azma na malengo makuu ya Vodafone ya kuchangia kubadili maisha ya watanzania.
Vodafone kupitia Vodacom Tanzania imekuwa ikiwekeza kiasi kikubwa cha fedha kusaidia na kuunga mkono miradi mbalimbali ya kijamii nchini ikiwemo maeneo makuu matano ya Elimu, Afya, Kuinua vipato vya wanawake, Mazingira na Michezo ili kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuwaletea wananchi maendeleo
Katika mazungumzo hayo mafupi Bw. Colao alimuhakikishia Rais Kikwete kwamba Vodafone itaendelea kuwekeza katika maendeleo ya jamii Tanzania hususan katika maeneo ya afya na elimu ambayo yanauhusiano wa moja kwa moja na wa karibu katika kuiwezesha jamii kuondokana na changamoto ambazo zinaweza kuathiri maendeleo ya watu na hivyo kushindwa au kupunguza kasi ya kubadili maisha yao.

Richmond kutikisa Bunge Mbunge wa Ubungo,John Mnyika


Mbunge wa Ubungo,John Mnyika
 NI HOJA BINAFSI ILIYOWASILISHWA NA JOHN MNYIKA WA UBUNGO

SAKATA la Richmond linatarajiwa kurudi upya bungeni baada ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika kuwasilisha hoja binafsi kuhusu utekelezaji wa Maazimio 13 yaliyobaki ya Bunge, juu ya mkataba baina ya Tanesco na kampuni hiyo ya kufua umeme wa dharura.Mnyika alisema jana katika taarifa yake kuwa lengo la hoja yake hiyo ni kutaka uamuzi wa Bunge la Tisa Mkutano wa 18 Februari, 2010 kufunga mjadala huo ubadilishwe ili hoja hiyo irudi upya bungeni.
“Niliwasilisha hoja hiyo Ofisi za Bunge Januari 25, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la 2007, Kanuni 54, (4) na 55 (1),” alisema Mnyika katika taarifa yake hiyo na kuongeza:
“Ikipokewa na kujadiliwa, hoja hiyo itaongeza msukumo wa utekelezaji wa maazimio ya Bunge na hivyo kuchangia katika mapitio ya mikataba yenye kuongeza bei ya umeme na kuweka mfumo wa kulihusisha Bunge katika maandalizi ya mikataba yenye maslahi kwa taifa.”
Februari 2010, Bunge lilifunga mjadala huo baada ya Serikali kutoa taarifa ya tatu ya utekelezaji wa mapendekezo yake. Taarifa hiyo ilitanguliwa na nyingine mbili zilizowasilishwa bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Agosti 28, 2008 na Februari 11, 2009.
Moja ya taarifa hizo ilikabidhiwa na kujadiliwa na Kamati, ambazo zililitaarifu Bunge kuwa utekelezaji wa Maazimio 10 kati ya 23 yaliyotolewa na Bunge, umefanyika hadi Februari 2009 na Maazimio 13 bado yalikuwahayajakamilika.
Baadhi ya maazimio ambayo utekelezaji wake haujakamilika ni Azimio Na. 3, ambalo liliagiza Mkataba kati ya Tanesco na Richmond Development Company LLC (uliorithiwa na Dowans Holdings S.A.) na mingine kati ya Tanesco na IPTL, Songas, Aggreko na Alstom Power Rentals, ipitiwe upya mapema kama mikataba ya madini ilivyopitiwa upya na Serikali.

“Iwapo Azimio hili lingetekelezwa kwa ukamilifu wake, gharama za uzalishaji Tanesco zingepungua na hivyo bei ya umeme isingepandishwa kwa kiwango kikubwa kama ilivyo sasa,” alisema Mnyika.

Maazimio mengine ambayo utekelezaji wake haujakamilika ni pamoja na lile lililotaka Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah awajibishwe kutokana na taasisi yake kushindwa kuona upungufu katika mchakato ulioipatia zabuni Richmond.

Azimio jingine ni lile lililotaka kuwajibishwa kwa watumishi wa umma akiwemo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, ambaye hata hivyo, hakuchukuliwa hatua yoyote hadi alipostaafu na kutowajibishwa kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika.

Katika sakata hilo, Serikali pia haijatekeleza azimio la kuwajibishwa kwa aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi badala yake ilieleza kuwa uchunguzi ulikuwa unaendelea dhidi yake.

“Hoja binafsi itakapojadiliwa bungeni itawezesha Bunge na wananchi kwa ujumla kupata taarifa ya utekelezaji wa maazimio hayo 13,” alisema Mnyika katika taarifa hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa Mnyika kuwasilisha hoja hiyo bungeni. Aprili 13, 2011 aliiwasilisha... “Hata hivyo, niliijibu Ofisi ya Bunge kupatiwa taarifa ya utekelezaji uliofanywa na Serikali baada ya Februari, 2010 bila kupatiwa majibu hivyo nimeiwasilisha tena ili hoja husika ijadiliwe.”

“Kwa muktadha huo, hoja binafsi husika itawezesha mjadala kuhusu uamuzi husika kufunguliwa na kutoa fursa kwa jambo hilo kufikiriwa tena ili kuwezesha hatua kamili kuchukuliwa juu ya maazimio 23 ya Bunge yaliyopitishwa Februari 15, 2008 katika Mkutano wa 10 wa Bunge la Tisa.”
Mnyika alihoji Serikali kutochukua hatua zozote hadi sasa wakati ililieleza Bunge kwamba vyombo vya dola vimekamilisha uchunguzi wake wa ndani ya nchi kuhusu suala hilo.
“Hata hivyo, zoezi lililoendelea toka Februari, 2010 ni kufanya uchunguzi wa nje ya nchi kwa kushirikiana na vyombo vya dola vya kimataifa ambapo, mmoja umemalizika bila hatua zozote kuchukuliwa kwa wahusika katika kashfa ambayo maazimio ya Bunge yalipitishwa zaidi ya miaka mitatu iliyopita hali ambayo inaweza kusababisha hata mashahidi na ushahidi kupotea,” alisema.
Mnyika pia alihoji sababu za kutoanza kutekelezwa ipasavyo kwa azimio la 13, lililotaka Serikali izihusishe Kamati za Kudumu za Bunge kwenye hatua za awali za maandalizi ya mikataba mikubwa ya muda mrefu ya kibiashara ili kuondokana na utaratibu uliopitwa na wakati kwamba mikataba ya kibiashara ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe.
Soma zaidi http://mwananchi.co.tz

Ban Ki Moon; " Migiro Ameomba Kupumzika"


NEWYORK, Marekani
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon amesema Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo,  Asha Rose Migiro ameomba mwenyewe kustaafu.Akizungumza na waandishi wa habari jana katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijiji New York, Marekani, Ki Moon alisema hata hivyo Dk Migiro ataendelea kuwapo kwenye ofisi za umoja huo, akiratibu shughuli mbalimbali hadi Juni mwaka huu.

 Alisema mbali na Dk Migiro, mwingine aliyeomba kuacha kuutumikia umoja huo ni Vijar Nambiar ambaye ni Mkuu wa  Ofisi yake.

 “ Kama mlivyotangaziwa mwishoni mwa mwaka jana kuhusu mabadiliko  yanayotarajiwa kufanyika katika nafasi za  watendaji waandamizi. Ningependa kuongezea na kuwajulisha kwamba, Naibu Katibu Mkuu,  Dk Migiro  na Vijar Nambiar wamewasilisha   kwangu maombi  yao ya kutaka kuachia nafasi zao  ili kuniruhusu  kuunda timu mpya ya  maofisa waandamizi nitakaofanya nao kazi katika  awamu  ya pili ya  uongozi wangu,” alisema Ki Moon.

 “Ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati  kabisa kwa  Naibu Katibu Mkuu, Dk Asha- Rozi Migiro,  kwa uamuzi wake huo, na kwa kazi nzuri na ushirikiano mkubwa na usio na shaka wala doa  alionipatia katika kipindi chote cha miaka mitano iliyopita akiwa msaidizi wangu wa karibu,” alisisitiza.  
Alisema Dk Migiro alimpa  ushirikiano mzuri mno na kumshauri kwa busara huku akijituma kwa uadilifu mkubwa katika kukabiliana na changamoto nyingi  zinazoukabili Umoja wa Mataifa.


Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa, aliyasema hayo baada ya  kuainisha mpango kazi na vipaumbele vyake katika miaka mitano ya muhula wa mwisho ya uongozi wake Kwa mujibu wa Ki Moon watendaji wengine watakaondoka ni wa Idara za Utawala, Maendeleo, Huduma za Mikutano,  Habari,  Ofisi ya Upokonyaji wa silaha,  na Mshauri wa Masuala ya Afrika.
 Wengine ni   wasimamizi  wa  Idara za Uchumi za Afrika na Ulaya,   waratibu wa  mifuko ya maendeleo na Idadi ya watu  UNDP na UNFPA.  Chanzo: MWANANCHI

Sunday, 22 January 2012

Rais Kikwete na Dk . Slaa


Rais Kikwete: Nasikia Dk.Slaa umekuwa ukinipiga chenga tusisalimiane? 
Dk.Slaa:Mh,ulitaka vijana wako wa usalama wanikamate kwa kuvunja itifaki?

Naam,ni jana tu wote tumesikia habari za watu hawa wakubwa kukwepana na au kutosalimiana.Wengine wetu tulidhani ni mambo yalee ya uchaguzi. Ufafanuzi ukatolewa na wengi wetu tukadhani ni uongo wa wanasiasa.Leo picha hii halisi kabisa(siyo ya kutengenezwa) inaonyesha waheshimiwa hawa wakishikana mikono tena kwa tabasamu kuu.Ikiwa hili ni tabasamu la kweli litokalo moyoni au ni mambo ya kwetu kutabasamu ili ionekane vizuri wakati ndani ni chuki siyo rahisi kujua.Tunachojua ni kwamba viongozi hawa hawakujali maneno yaliyokuwepo kuhusu wao.Tunashawishika kudhani kuwa kuna jambo zito kabisa kati yao na kwa taarifa zilizoambatana na picha za ikulu inahusu mambo ya katiba.Je Wakati huu kutakuwa na maelewano kati ya serikali na CHADEMA? na je ni sahihi kwa chama kilichosema kilidanganywa mara ya kwanza na kutangaza kutoshiriki jambo hilo kama serikali italipeleka bila kuzingatia matakwa yao kurudi tena ikulu kwa mazungumzo hayohayo? nini kimebadilika mpaka wadhani kuwa wakati huu watasikilizwa? TUSUBIRI TUONE
Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar es salaam

chadema na serikali waendelea na maongezi juu ya katiba,dk.slaa ahudhuria


 Rais Kikwete akimkaribisha Dk.Slaa na viongozi wa CHADEMA ikulu jana usiku kwa mazungumzo tena kuhusu suala la katiba
 Wanapitia makabrasha kifungu kwa kifungu
 Dk.Slaa akitoa ufafanuzi juu ya masuala ambayo chama chake kinaamini ni muhimu kuzingatiwa kwa maslahi ya wananchi
Maongezi yanaendelea, kifungu kwa kifungu.saa tatu walikaa katika vikundi kile cha CHADEMA na kile cha serikali kujadili misimamo na makubaliano, kisha kikao kiliendelea hadi saa 5:30 usiku.tunasubiri taarifa rasmi
Picha kutoka IKULU

CHADEMA YATEUA MGOMBEA JIMBO LA UZINI


             Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimemteua Ali Mbarouk Mshimba
kuwa mgombea wa Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kwa tiketi ya
CHADEMA katika Jimbo la Uzini.
Uteuzi huo umefanywa na Kamati Kuu ya chama taifa katika mkutano wake wa
kawaida uliofanyika Dar es salaam tarehe 20 Januari 2012 chini ya uenyekiti
wa Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara) Said Amour Arfi (Mb) na Katibu Mkuu Dr.
Wilbroad Slaa.
Maamuzi hayo yalipitishwa kwa kauli moja na kamati kuu ya chama taifa baada
ya kupokea taarifa ya mchakato wa uteuzi wa awali uliofanywa na ngazi
husika za CHADEMA Jimbo la Uzini iliyowasilishwa na Naibu Katibu Mkuu
(Zanzibar) Hamad Musa Yusuph.
Katika taarifa hiyo Kamati Kuu ya Chama Taifa ilielezwa kwamba uchukuaji
fomu za uteuzi wa ndani ya chama ulianza tarehe 15 Disemba 2011 na
kuhitimishwa tarehe 15 Januari 2012. Jumla ya wanachama watatu walichukua
fomu za kugombea.
Kura za maoni za uteuzi wa mgombea zilifanywa tarehe 17 Januari 2012,
ambapo Ali Mbarouk Mshimba alikubaliwa kwa kura zote 126 za wajumbe
waliohudhuria mkutano mkuu wa jimbo, kati ya wajumbe 130 waliopaswa
kuhudhuria kutoka katika shehia zote 13 za Jimbo la Uzini.
Mapendekezo hayo ya jimbo la Uzini ya kumteua Ali Mbarouk Mshimba
yaliridhiwa na kikao cha Kamati ya Utendaji ya Wilaya ya Kati
kilichofanyika tarehe 18 Januari 2012.
Ali Mbarouk Mshimba alizaliwa tarehe 10 Aprili 1966 katika Kijiji cha
Tunduni, Jimbo la Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Zanzibar. Ali
Mbarouk Mshimba ni Katibu wa CHADEMA wa Jimbo la Uzini na ni Mwalimu wa
Skuli Msingi Mchangani Chamba.
Ali Mbarouk Mshimba amesoma Shule ya Msingi Uzini mwaka 1977 mpaka 1984 na
Shule ya Sekondari ya Fidel Castro mwaka 1984 mpaka 1987 na baadaye kusoma
mafunzo ya ualimu ya miaka miwili katika ngazi na nyakati mbalimbali mwaka
2006 mpaka 2008 (Special Certificate in Teacher Education through Teachers
Advancement Program) yaliyoratibiwa na Wizara ya Elimu na Ufundi Stadi ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.



Imetolewa tarehe 21 Januari 2011 na:*

Dadi Kombo Maalim*

Afisa Mwandamizi wa Habari na Uenezi*

Ofisi ya Makao Makuu Zanzibar*

JK akutana na uongozi wa NCCR Mageuzi Ikulu jijini Dar es salaam leo



. Rais Jakaya Kikwete akipokea mapendekezo ya chama cha NCCR-MAGEUZI kuhusu mchakato wa Katiba toka kwa Mwenyekiti wa chama hicho Mh James Mbatia leo alipokutana na uongozi wa chama hicho Ikulu jijini Dar es salaam

  Mkuu wa Idara ya Katiba na Sheria wa Chama cha NCCR - Mageuzi, Dk. Sengondo Mvungi akisoma mapendekezo ya chama hicho juu ya mchakato wa katiba
 Rais Kikwete akiongea na uongozi wa NCCR-MAGEUZI
Akiwaaga baada ya picha ya pamoja
Picha na IKULU 

CHADEMA WAFUNGUA MSINGI TEGETA KATA YA KUNDUCHI


 Henry kilewo,katibu wa CHADEMA kinondoni kwenye ufunguzi wa msingi Tegeta
 Renatus Mrashani katibu wa mkoa wa Dar es salaam

 Msingi
 Wanachama
Diwani wa sinza CHADEMA

mh.jeremia sumari aagwa karimjee


 Mh. William Lukuvi akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali
 Mh.Freeman Mbowe akitoa salamu kwa niaba ya kambi rasmi ya upinzani
 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mh.Jeremiah Sumari
 Wageni waliofika kutoa heshima zao za mwisho wakiongozwa na Mh rais ndg Jakaya Kikwete
 Waliofika kutoa heshima ya mwisho

MAKAMU WA RAIS ATEMBELEA MRADI WA MAJI WA CHIUMBATI , APOKEA KADI YA MWENYEKITI WA CHADEMA (W) NACHINGWEA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananchi wakati alipotembelea mradi wa maji wa Chiumbati, Nachingwea, akiwa katika ziara yake ya Mkoa wa Lindi jana, januari 20.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi wa Nachingwea, wakati alipokuwa akiondoka katika mradi wa maji wa Chiumbati jana, januari 20, 2012. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyesha kadi ya CHADEMA baada ya kukabidhiwa na Hassan Mkope (kulia) aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Nachingwea, aliyeamua kujiengua na kujiunga na CCM. Makamu ameanza ziara yake katika Mkoa wa Lindi jana januari 20. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

maandamano ya wanafunzi waislamu yafanyika dar








Wanafunzi wa kiislamu shule za sekondari za Dar es salaam wameandamana jana kama walivyoahidi siku chache zilizopita kwenye vyombo vya habari.Maandamano yao yaliishia viwanja vya kidongo chekundu na waziri wa elimu Dk.shukuru kawambwa alikuwepo kuongea nao.