Meneja Mauzo wa Kampuni ya Vodacom Kanda ya Kaskazini Bw. Jerome Munishi akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima cha Matonyak Bi. Emmy Ndeumo cha Mjini Arusha zawadi mbalimbali kwa ajili ya kuwawezesha watoto kusherehekea vema siku kuu ya Krismasi. Misaada hiyo iliyojumuisha vykula na vifaa vya shule ilikabidhiwa jana ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Vodacom Share and Care.
Mtoto Naseeb Juma wa kituo cha watoto yatima cha Kibowa kilichopo eneo la Lemara mjini Arusha akipokea kwa furaha zawadi ya Krismasi kutoka kwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Vodacom Kanda ya Kaskazini Bw. Jerome Munishi. Vodacom imetoa zawadi mbalimballi kituoni hapo ikiwemo vyakula na vifaa vya shule ikiwa ni sehemu ya kampeni ya share & care inayoendeshwa na Vodacom Desemba ya kila mwaka.
Mfanyakazi wa Vodacom kanda ya kaskazini Rehema Ndunguru akigawa viburudisho watoto wa kituo cha Matonyak cha mjini Arusha ikiwa ni sehemu zawadi mbalimbali za krismas zilizotolewa kituoni hapo kupitia kampeni ya Vodacom Share & Care inayoendeshwa kila ifikapo Disemba. Vodacom imekabidhi misaada mbalimbali kwa vituo sita vya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu vya mjini Arusha jana.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom Kanda ya kaskazini wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu na watoto pamoja na viongozi wa kituo cha yatima cha Matonyak cha mjini Arusha. Wafanyakazi hao walifika kituoni hapo jana kukabidhi zawadi mbalimbali za krismasi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Vodacom Share & Care ambapo jumla ya vituo sita vya yatima vya mjini Arusha vilipatiwa misaada.
No comments:
Post a Comment