KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 19 December 2011

NBC Washeherekea Kumaliza Mwaka

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kushoto, mstari wa mbele) pamoja na mkewe, Noella Mafuru (nyuma yake) wakiwaongoza baadhi ya wafanyakazi na wenza wao katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (wa pili kulia) akisalimiana na Meneja wa Tawi la NBC Geita, Onael Mpeku katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na mkurugenzi huyo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni mke wa Mafuru, Noella na kulia ni Meneja wa NBC Kahama, Martin Mkanda.
Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Maharage Chande (kushoto) akibadilishana na mawazo na Mkuu wa Mauzo Kitengo cha Makampuni, Minnie Adolf Kibuta katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam.
Mshauri wa Habari wa NBC, Redemptus Masanja (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja, Mama Jane Dogani wakiselebuka pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC na wenza wao, katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam .
Meneja Chapa na Matangazo wa NBC, Arden Kitomari (katikati) akifanya vitu vyake pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa NBC, katika hafla ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Lawrence Mafuru (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa NBC na wenza wao, wakijimwaga ukumbini kusherehekea pati ya kumaliza mwaka iliyoandaliwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Lawrence Mafuru (hayupo pichani), jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment