KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Tuesday, 20 December 2011

JK Awaapisha Mabalozi Wapya Ikulu Dar

Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Phillip  Marmo, kuwa Balozi wa China, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Mabalozi wapya waliofia Ikulu Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete, wakisubiri kuapishwa.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Batilda Buriani,  kuwa Balozi wa Kenya, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Dkt. Deodorus Kamala, kuwa Balozi wa Ubelgiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Ally A. Saleh, kuwa Balozi wa Oman, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimwapisha, Shamim Nyanduga, kuwa Balozi wa Msumbiji, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika leo mchana Desemba 19, Ikulu Dar es Salaam.
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda (kuli) na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, wakizungumza jambo, baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kuwaapisha mabalozi wapya iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo, Desemba 19.
Rais Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Ushirikiano wa Kimataifa, Mahadhi Juma Maalim, wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wapya baada ya kuapishwa rasmi leo Ikulu Dar es Salaam.
Samim Nyanduga, akipongezwa na Mumewe, baada ya kuapishwa rasmi kuwa Balozi wa Msumbiji, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo. Nyuma yao ni wanafamilia wa Familia hiyo.

Picha Na Muhidin Sufiani - OMR

No comments:

Post a Comment