Daraja la Luhanga limekatika na watu wanapita katika maji yenye kimo cha kiunoni
Dar na foleni ya asubuhi.Hapa ni njia panda ya tabata segerea na foleni hii imeanzia Buguruni
Godoro limenasa kwenye mti.Limeletwa hapo na maji jana
Watu wakipata shida kutembea kwani maeneo mengi mitaani yamejaa maji
Ukuta wa shule ya msingi Gonzaga Luhanga umebomolewa na maji jana
Leo asubuhi Ubungo maziwa.Maduka,bucha na saloon vikiwa vimefungwa na maji yamejaa ndani
Mti mkubwa umeng'olewa na kuangukia nyumba hivyo kusababisha uharibifu mkubwa,Mabibo
Familia zikihangaika kumalizia usafi katika nyumba zao.Samani hizi hasa masofa yameharibiwa kabisa
Mabibo,nyumba zimeharibiwa na maji ya mto
Kigogo mwisho, baadhi ya vitu vya familia ambazo bado hazijapata ufumbuzi juu ya makazi yao
Mzee huyu anaendelea na usafi wa nyumba yake maeneo ya Luhanga
Luhanga, hapa watu wamelala usiku wanapaita camp baada ya kuwa wameshindwa kumaliza kutoa tope katika nyumba zao
Daraja la kigogo limekatika.vijana wameweka nguzo za umeme na wanatoza 500 kwa kila anayepita hapo.anayeogopa kuvuka mwenyewe wanamsaidia kuvuka kwa sh 1000.
Hapa vijana wakimsaidia dada kuvuka
Nyumba zaidi ya 4 zimeharibiwa kabisa maeneo ya kigogo darajani,wakazi wanajaribu kutoa mabaki ya matofali
Huyu bwana kaamua kuchukua tahadhari mapema.Anahama tabata dampo

DARAJA LA JANGWANI HALIPITIKI TENA , BARABARA YAFUNGWA
Hali ni mbaya katika barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ambapo kwa muda mrefu watu wamekuwa wakiishi hapo, japokuwa serikali imekuwa ikiwaambia hawatakiwa mkujenga katika eneo hilo kutokana na madhara yanayoweza kutokea endapo mvua zitanyesha,Lakini hali ndivyo ilivyo kwa sasa, ambapo katika eneo hilo maji yamefurika nyumba zinaelea kwenye maji na barabara hiyo imefunikwa na maji na kusababisha vyombo vya usalama kuifunga, hivyo kukata mawasiliano kati ya Kariakoo na mjini maeneo na Magomeni. Kutokana na nvua ambayo imenyesha siku mbili mfurulizo jijini Dar es salaam Watu ni wengi katika eneo hilo lakini pia kutokana na ubishi, kunawatu wamekuwa wakizolewa na maji kwa sababu ya kulazimisha kuvuka, wakati maji hayo yanaenda kwa kasi kubwa, baadhi ya watu wamekuwa wakiokolewa na vikosi vya uokoaji na wanapelekwa katika hospitali ya Muhimbili kwa matibabu zaidi, kama wanavyoonekana wakina mama hawa katika picha wakipelekwa kwenye gari baada ya kuokolewa kwenye maji.
Akina mama hawa wakilia baada ya kuokolewa kwenye maji hapa walikuwa wakielekea kupanda gari tayari kwa kuwapeleka hospitali ya muhimbili kwa uangalizi zaidi wa afya zao.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Slaa kushoto amekuwepo pia katika tukio hilo la uokoaji, hapa akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wanausalama.
Hapa ni mahali ambapo pamewekwa uzio ili kuzuia watu kuvuka ng'ambo yaani uapnde wa pili.Baadhi ya watu wakiokooa vitu vyao na kuviweka kando ya barabara ya Morogoro.
Hawa wajapan wanaofanya kazi katika kampuni ya Kajima yenye ofisi zake hapo Jangwani ambayo nayo imevamiwa na maji na kuharibu vitu mbalimbali huku maji yakiwazingira baadhi ya wafanyakazi ambao walikuwa wakiokolewa na vikosi wa uokozi.
Baadhi ya watu wamekuwa wakikimbilia kwenye mapaa ya nyumba kama nyumba zinavyoonekana zikiwa zimezama kabisa kwenye maji.
Eneo lote la Jangwani limebadilika na kuwa kama ziwa vile kutokana na mafuriko hayoTABATA DAMPO WAOMBOLEZA MVUA YA MAFURIKO
Maeneo ya tabata dampo,mto umefurika na watu wametoka majumbani kwani nyumba zimejaa maji.hali ni mbaya sana. Na sasa hivi saa moja usiku mvua imeanza kunyesha tena,Kila mtu ana wasiwasi.Tuombe dua Mungu apishe mbali mvua kama ya leo kanyesha usiku.
No comments:
Post a Comment