Vituo Ligi Ya Taifa Vyapangwa
Release No. 070
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mei 9, 2012
VITUO LIGI YA TAIFA VYAPANGWA
Kamati
ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imepanga
vituo vitatu vya Ligi ya Taifa inayoshirikisha mabingwa wa mikoa kwa
ajili ya ligi hiyo itakayoanza Mei 26 mwaka huu.
Kundi
A lenye mabingwa wa mikoa ya Iringa (Kurugenzi Mufindi), Lindi (Lindi
SC), Mbeya (Tenende FC), Morogoro (Mkamba Rangers), Mtwara (Ndanda SC),
Pwani (Super Star), Rukwa (Mpanda Stars) na Ruvuma (Mighty Elephant)
zitacheza mechi zake mjini Mtwara.
Mji
wa Kigoma utakuwa mwenyeji wa mabingwa wa mikoa ya Dodoma (CDA),
Kagera (Bandari FC), Kigoma (JKT Kanembwa), Mwanza (Pamba SC),
Shinyanga (Mwadui SC), Singida (Aston Villa) na Tabora (Majimaji).
Kundi
C lenye mabingwa wa mikoa ya Arusha (Flamingo SC), Dar es Salaam
(Ashanti United ya Ilala, Red Coast ya Kinondoni na Tessema FC ya
Temeke), Kilimanjaro (Forest FC), Manyara (Nangwa VTC), Mara (Polisi
Mara) na Tanga (Korogwe United) watachezea mechi zao mkoani Mara.
Mwisho
wa kuwasilisha fomu za usajili ni Mei 15 mwaka huu wakati kipindi cha
pingamizi ni kuanzia Mei 16 hadi 22 mwaka huu. Mei 23 mwaka huu Kamati
ya Mashindano ya TFF itakutana kupitia usajili huo. Wachezaji
wanaosajiliwa ni wale wale waliochezea timu hizo katika ligi ya mkoa.
Mei
14 mwaka huu ni mwisho kwa mikoa yenye pingamizi kwa mabingwa wao kuwa
wameshashughulikia rufani husika. Kamati ya Mashindano imeagiza kuwa
kwa mikoa itakayoshindwa kufanya hivyo mpaka baada ya tarehe hiyo
mabingwa wao hawatashiriki ligi hiyo.
Timu
tano zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.
Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi na washindwa wawili bora (best
losers) kutoka kundi A na C ambayo yana timu nane kila moja.
LIUNDA KUSIMAMIA MECHI LESOTHO
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua Leslie Liunda wa
Tanzania kuwa Kamishna wa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia 2014 Kanda
ya Afrika kati ya Lesotho na Sudan itakayochezwa jijini Maseru.
Mechi
hiyo ya kwanza ya raundi ya pili itachezwa kati ya Juni 1 na 3 mwaka
huu. Lesotho na Sudan ziko kundi D pamoja na Ghana na Zambia.
Naye
Hafidhi Ally ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
kuwa Kamishna wa mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Dynamos FC ya
Zimbabwe na Esperance Sportive ya Tunisia.
No comments:
Post a Comment