Tume Ya Kurekebisha Sheria Tanzania Yapitia Ripoti Ya Sheria Zinazosimamia Mfumo Wa Haki Za Madai
Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Buxton Chipeta akitoa ufafanuzi wakati wa mkutano wa kupitia Ripoti za Sheria zinazosimamia Mfumo wa Haki za Madai jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa Mkutano wakimsikiliza Jaji Mstaafu Chipeta
Na Munir Shemweta
Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania imeanza kupitia ripoti za Mapitio ya Sheria zinazisimamia mfumo wa haki za Madai kwa lengo la kufanya maboresho ya sheria hizo.
Katika Mapitio hayo Tume kwa kushirikiana na wadau ambao ni wakufunzi wa vyuo, Taasisi zinazotoa misaada ya kisheria, Wanasheria, Mawakili na Mahakimu kwa pamojaitapitia ripoti zilizofanyiwa kazi na Wataalamu washauri.
Katika mchakato huo Tume imegawa makundi manne yatakayopitia ripoti hiyo katika mikoa ya Mwanza ambapo kundi hilo linaongozwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Profesa Ibrahim Juma, Arusha Kamishna wa Tume Ester Manyesha, Mbeya Kamishna wa Tume Profesa Sufian Bukurura, Dodoma Kamishna Jaji Ernest Mwipopo na Dar es Salaam linaloongozwa na Jaji Mstaafu Praxon Chipeta..
No comments:
Post a Comment