Stars vs Malawi Hakuna Mbabe
Mpira umekwisha kama wanavyoonekana katika picha wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwenda mapumziko, Si Taifa Stars wala Malawi ambayo imepata goli, hata hivyo wamalawi wameshambulia mara nyingi katika lango la Taifa Stars katika kipindi cha kwanza, lakini uimara wa mabeki pamoja na Golikipa Juma Kaseja umesaidia Wamalawi hao kutopata goli , Taifa Stars yenyewe imefanya mashambulizi ya hatari mawili tu! hata hivyo haikuwa bahati yao ambapo mpaka mwisho wa mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0.
Wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars wakiingia uwanjani jioni hii kwa ajili ya kupasha mwili kabla ya mpambano wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Malawi The Flames
Wachezaji wa timu ya Malawi wakipasha mwili kabla ya kuingia uwanjani kukwaana na Taifa Stars jioni hii kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa Stars wakijifua kabla ya mpambano huo jioni hii.Timu ya Malawi iko safarini kuelekea nchini Uganda ambako itakipiga na timu ya Uganda Cranes.
Mpambano huo unafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment