map: tzaffairs.org
Utajiri wa Gesi Asilia tulio nao mpaka sasa haujawekwa wazi na Mamlaka husika na hasa Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania.
Ni vizuri wakawa wanauambia umma ili wenye nchi wajue.
Gesi ya Tanzania ambayo imegunduliwa na kutangazwa mpaka hivi sasa ni 19 trillion cubic feet (11 tcf za British Gas, 5.3 tcf za StatOil na 2.7 tcf za kampuni nyingine ndogo ndogo). Bei ya wastani ya Gesi Asilia iliyopo katika soko la Dunia kwa wakati huu ni USD 7 kwa kila 1,000 cubic feet (cf). Hata hivyo, JPMorgan walipofanya tathmini zao, imeonesha kuwa hifadhi ya British Gas ni takribani 60tcf na zile za StatOil ni takribani 25tcf.
Hivyo basi, utajiri wa Tanzania wa Gesi Asilia unakadiriwa kufikia 85tcf, na kwa kasi ya utafutaji inavyoendelea inakadiriwa kuwa mwaka 2014, Tanzania itakuwa inaongoza katika Afrika kwa utajiri wa Gesi na kuishinda Nigeria yenye 189tcf hivi sasa.
Kwa makadirio ya chini kwa viwango tajwa, thamani ya Gesi yote ya Tanzania iliyopo sasa ni Dola za Kimarekani Trilioni 6.
Utajiri uliotangazwa mpaka sasa ni wa visima vya Songosongo, Mkuranga, MnaziBay na visima vya kina kirefu vinavyoendeshwa na Kampuni za StatOil ya Norway na BG ya Uingereza.
Mpango kamambe wa Gesi, Sera na Sheria ya Gesi na Sheria ya Usimamizi wa wa Mapato ya Mafuta na Gesi ni masuala ya kumaliza sasa.
Tujipange kuhakikisha Uwazi na Uwajibikaji ili Utajiri huu ulete maendeleo ya WATU wa Tanzania. Kila mtu atimize wajibu wake sasa. Tusisubiri kulaumiana kama ilivyokuwa sekta ya Madini. Tuchukue hatua sasa kuweka sawa usimamizi wa sekta ndogo ya Mafuta na Gesi.
Sheria ya Usimamizi wa Mapato za Mafuta na Gesi ya Ghana (Petroleum Revenue Management Act 2011) ni nzuri sana. Waziri wa Fedha aliahidi kwenye 'letter of intent' kwa IMF kwamba tutatunga sheria kama hiyo ifikapo mwisho wa mwaka. Nadhani sheria hii inaandikwa kwa siri sana maana imekuwa kimya sana.
Sheria ya Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesi Asilia inapaswa kuwa wazi kuanzia matayarisho ya kuandikwa kwake mpaka katika utekelezaji wake. Uwazi na Uwajibikaji ni dhana muhimu sana katika kuhakikisha Taifa linafaidika na utajiri wa Mafuta na Gesi na Nchi kuepuka laana ya Mafuta (Oil Curse).
Chanzo cha taarifa ukurasa wa Zitto Kabwe wa facebook.

No comments:
Post a Comment