KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Thursday, 31 May 2012


Suits you, Mario! Italy striker Balotelli drops tracksuit to scrub up for team photo


we've got used to seeing Mario Balotelli adorned in some outrageous garments over the last couple of years, but he showed us this week that he can scrub up pretty well when he wants to.
Balotelli and the rest of the Italian squad were suited and booted on Wednesday before posing for their official Euro 2012 team photo in Coverciano, Tuscany, ahead of their departure for the tournament in Poland and Ukraine.
Suits you: Balotelli heads out for the team photo in Coverciano
Suits you: Balotelli heads out for the team photo in Coverciano
Suits you: Balotelli heads out for Italy's official team photo in Coverciano, Tuscany
Suits you: Balotelli heads out for the team photo in Coverciano
Azzurri boss Cesare Prandelli dropped the Manchester City striker from his squad earlier in the year, citing his volatile temperament, but the pair have reconciled their differences and Balotelli was named in the 23 this week - and will wear the No 9 shirt.
Outrageous: Balotelli has worn some bizarre outfits in the past
Outrageous: Balotelli has worn some bizarre outfits in the past
Outrageous: Balotelli has worn some bizarre outfits in the past
Outrageous Balotelli
Outrageous Balotelli
Balotelli made the headlines earlier this week as he warned he would 'kill' any fan who racially abused him at the tournament. The 21-year-old said: 'I will not accept racism at all. It's unacceptable. If someone throws a banana at me in the street, I will go to jail, because I will kill them.'
Ready to shine: Balotelli has been given the No 9 shirt for Euro 2012
Ready to shine: Balotelli has been given the No 9 shirt for Euro 2012
Ready to shine: Balotelli has been given the No 9 shirt for Euro 2012
Italy are drawn in Group C at the Championships, where they face world champions Spain on June 10, Croatia on June 14 and the Republic of Ireland on June 18.
Prandelli is adamant that Balotelli has cleaned up his act and that he is ready to lead the line for his country. He has certainly cleaned up his dress.

Wabunge Wa Chadema Waangwa Rasmi kwa Kuangalia Mechi Ya Kimataifa Kati Ya Brazil Na Marekani

Baaada ya kazi kubwa ya kuzindua na kuimarisha tawi la chadema Washington Dc Maryland na Virginia,Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Mhe. Peter  Msigwa na  Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu  Dogo janja, Usiku wa Jana Jumatano Mei 30,2011  waagwa rasmi kwa kuangalia mpambano wa kimataifa kati ya US na Brazil ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.
Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo  Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa.
Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani. 
Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo  Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
Forward wa United States Landon Donovan, akipandisha majeshi juu huku alidhibitiwa na Brazil defender Marcelo wa Brazi katika mpambano wa kirafiki.
Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la  kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar
Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao

Wabunge Wa Chadema Washuhudia Mechi Ya Brazil Dhidi Ya Marekani!

Kushoto Peter Msingwa na kulia ni Joshua Nassari

"Nape Ni Gamba"-Maige



na Ahmed Makongo, Kahama

KATIBU wa Itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye ametajwa kuwa gamba namba moja linalotakiwa kuvuliwa, kwa kile kilichodaiwa kutoa matamshi mengi ambayo yamekivunjia heshima na kukidhohofisha chama hicho.

Nape pia ameshutumiwa kwa kushindwa kwake kubuni mbinu za kuingiza wanachama na zaidi kupambana na wimbi la kuhama kwa viongozi, makada na wanachama wa CCM.

Shutuma hizo nzito zimetolewa na Mbunge wa Jimbo la Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Ezekiel Maige (CCM) jana wakati akizindua matawi mawili ya wakereketwa wa chama hicho ambao ni wajasiriamali, katika Kijiji cha Isaka wilayani hapa.

Maige alisema kuwa Nape amekuwa akitoa kauli ambazo si za msingi, zisizojenga bila kujua kuwa zinakidhohofisha chama hicho tawala.

Mbunge huyo ambaye amepata kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema kwa sasa kuna wimbi kubwa la wana CCM wanaohamia vyama vya upinzani, ambalo ilitegemewa kuwepo kwa juhudi za makusudi za kuzuia chini ya usimamizi wa katibu huyo wa itikadi na uendezi.

“Kitendo cha CCM kupoteza wanachama zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja mkoani Arusha na sehemu nyingine wanachama 3,000, kinashitua, na ilitegemewa Nape kusimama imara na kuhakikisha chama hakiendelei kupoteza wanachama wake, lakini ndio kwanza anasema hajali na eti hao ni makapi,” alisema kwa kushangaa.

Nape akihutubia vijana mjini Bukoba siku chache zilizopita, alidai kuwa hata kama wanachama wote watahama, yeye (Nape) atabaki peke yake na CCM haitakufa.

Alidai kuwa kasi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haiwezi kupuuzwa na kiongozi makini, na kuongeza kuwa zinahitajika busara na bidii za kuwapa moyo waliopo ili nao wasiondoke na si kuwasimanga.

“Jamani Nape anachokifanya sasa ndani ya chama mimi ninaweza kuamini kwamba anatumika na kukidhi matakwa ya waliomtuma na si manufaa ya chama.

“Ninalolisema hapa lisitafsiriwe kwamba nalilia uwaziri, hapana, ila ni uchungu nilionao kwa chama changu kuona kila siku tunavyopoteza idadi kubwa ya wanachama, tuliyemkabidhi jukumu la uenezi anasema hajali, sasa huyu si atupishe mapema kabla mambo hayajaharibika?”

Maige alimwomba Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja kutumia nafasi yake kuwashauri wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) kuchukua hatua za haraka dhidi ya Nape.

Wakati Maige akitoa maneno hayo mazito, Mgeja alikuwa ameinamisha kichwa chake chini, lakini mamia ya wana CCM pamoja na wananchi wengine walishangilia kwa nguvu.

Katika hatua nyingine, Maige aliwalaumu viongozi wa CCM katika ngazi ya wilaya na kata, ambao wamekuwa na tabia ya kutowatembelea wananchi na kusikiliza kero zao, wakisubiri mpaka viongozi wa kitaifa.

Alisema tabia hiyo ni moja ya vyanzo vya wananchi kuichukia CCM.

“Jamani inakuwaje kiongozi mwenezi wa CCM kata ama wilaya anakaa kimya kabisa, hakuna kazi yoyote ya uenezi anayoifanya, hata kama katika kata ama wilaya yake itakuwa imetembelewa na wapinzani na wakamwaga sumu, wao hawajibu, wanasubiri mbunge ama diwani aitishe mkutano na wao hujitokeza,” alisema.

Alisema ili kukabiliana na wimbi la mabadiliko, ni vizuri wana CCM wakakaa chini na kujipanga vizuri kwa kuwa kitu kimoja badala ya kugawanyika kutokana na maslahi binafsi.

Serikali Yawaondoa Hofu Watalii Zanzibar



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MALIASILI NA UTALI

TAARIFA KWA UMMA

Tanzania ni Salama kwa Watalii

Kufuatia vitendo vya vurugu zilizozuka hivi karibuni katika maeneo kadhaa ya Mji wa
Zanzibar baada ya mitandao ya kimataifa imekuwa ikiripoti taarifa za kuwepo kwa hali
ya wasiwasi kwa watalii wanaotaka kuja kutembelea Visiwa hivyo.

Kama Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Utalii, ningependa kuwahakikishia
wageni, ambao tayari wako nchini, na wale ambao wanajiandaa kuja, kuwa vurugu hizo
ambazo zimeshadhibitiwa na Serikali hazikuathiri utalii. Mjini Zanzibar pamoja na
maeneo ya vivutio vya utalii kote nchini.

Hadi hivi leo napotoa taarifa hii, amani imetawala Mji Mkongwe Zanzibar na hakuna
taarifa yoyote ya uharibifu wa maeneo ya vivutio vya utalii vya Zanzibar wala kuchomwa
kwa hoteli ama kudhulika kwa raia yeyote wa kigeni. Hivyo nasisitiza kuwa Zanzibar
nisehemu salama kwa watalii.

Vilevile, Siku chache kabla ya tukio la Zanzibar, kulikuwa na matukio manne ya watalii
kuporwa katika maeneo ya Masaki jijini Dar es Salaam. Uporaji huo ulitendwa na watu
waliokuwa kwenye magari au pikipiki ambao waliwapora watembea kwa miguu.

Serikali inawahakikishia wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio
ya pekee na ya kimataifa kuwa hayo yalikuwa matukio ya pekee na ya kupita na hatua
zimechukuliwa na Jeshi la Polisi kuongoza usalam kwa wakazi na watalii.

Nachukua fursa hii kuwahakikishia wageni kwamba kila juhudi zimechukuliwa
kuhakikisha kuwa usalama wa watalii unadumishwa pamoja na faraja wakati
watakapotembelea Tanzania.

Daima tukumbuke kuwa, Tanzania ni kisiwa cha amani na nchi imenuia kudumisha sifa
hiyo nzuri.

Karibu Tanzania.

Mhe. Lazaro Nyalandu
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
30 Mei, 2012

CCM Yatoa Ufafanuzi Hotuba Ya Zitto Marekani



KUHUSU MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Katika hotuba yake anadai kwamba mchakato wa Katiba Mpya unaoendelea
hivi sasa unatokana na shinikizo la CHADEMA, Asasi za kiraia na
viongozi wa dini.

UFAFANUZI
Huo ni upotoshaji mkubwa na wa wazi kabisa unaolenga kufuta historia
sahihi ya mchakato wa uandikaji au upatikanaji wa Katiba Mpya
unaoendelea hivi sasa.

Ni jambo lililo dhahiri kabisa kwamba mchakato wa Katiba Mpya ni
utekelezaji wa hotuba ya Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) aliyoitoa katika salamu za kuaga mwaka 2010 kukaribisha mwaka
2011 na baadaye katika sherehe za Chama Cha Mapinduzi kutimiza miaka
34 Mjini Dodoma. Hili ndilo chimbuko halisi la hoja ya Katiba Mpya.

Akitoa maamuzi hayo alisema Katiba iliyopo sasa ni nzuri, imetuvusha
salama miaka hamsini iliyopita, tukiwa wamoja, imetujengea umoja wa
Kitaifa. Lakini katika kipindi hicho hicho kumetokea mabadiliko mengi
duniani na hapa nchini ya kisayansi, kiteknolojia, kitamaduni, kisiasa
n.k. Hakuna shaka kwamba sasa tunahitaji Katiba Mpya itakayotuvusha
miaka mingine 50 ijayo. Jambo hili Zitto Kabwe kalinukuu kwenye hotuba
yake anaposema kuwa:-

“Tanzania tunayoitaka kwa miaka mingine hamsini ….” Mantiki hii ya
miaka mingine 50 inatokana na hotuba ya Mhe. Dr. Jakaya M. Kikwete sio
yeye.


KUHUSU UBADHIRIFU SERIKALINI


Katika hotuba yake amedai kuwa CHADEMA ndio viongozi waliobeba dhamana
ya mpito huu, kutoka Serikali ya kibadhirifu isiyojali watu mpaka
Taifa lenye demokrasia iliyokomaa na lenye maendeleo na ustawi wa watu
wake. (Developmental Democratic State).

UFAFANUZI
Kwanza CHADEMA haina “dhamana” ya uongozi wa nchi, mwenye dhamana ya
uongozi wa nchi ni Chama Cha Mapinduzi ambacho kina Rais ambaye ni
Mkuu wa nchi, Mkuu wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu. CHADEMA
wanachokitafuta ni Mob leadership ambayo ni fujo “Anarchy or law
lessness” kitu ambacho huwezi kukidhibiti hata ukishika madaraka
(mfano ni Libya, Mali, Algeria n.k.).

Mob leadership ni fujo kwa sababu ina watu ambao hawana sera ya pamoja
hawana wajibu wa kisheria, hawana maslahi ya kijamii na kidini,
wanadai haki bila wajibu.

Dhamana ya kuwafikisha watu katika Serikali ya kidemokrasia imo
mikononi mwa Serikali iliyopo madarakani. Matamshi yanayotolewa na
baadhi ya viongozi wa CHADEMA yanaonyesha dhahiri kuwa hawathamini
demokrasia ya nchi, umoja wa kitaifa wala amani na utulivu.




Mfano:-

Tamko la Mhe. Joshua Nassari la kumzuia Rais, Mkuu wa Nchi,
asikanyage Mikoa ya Kaskazini mwa Tanzania.




Tamko la Mhe. Kabwe la kudai kuwa Wazanzibar wameporwa mafuta na gesi.
Hata kwenye uchaguzi mdogo wa Mbeya vijijini mwaka 2009 CHADEMA
ilitamka kwamba Mhe. Ali Hassan Mwinyi Rais Mstaafu asikanyage Mbeya.

Tamko la Mhe. Wenje kuwa Mwanza inajitosheleza kuwa nchi kwa
rasilimali zake na hivyo kupendekeza serikali za majimbo ili Mwanza
ijiendeshe yenyewe.

Matamko haya hayawezi kutamkwa na kiongozi mmoja wa CHADEMA bila
ridhaa ya Chama ama sivyo wangekuwa wanachukuliwa hatua na Chama chao.

Kwa kuwa matamshi haya ni uhaini, uchochezi na ufashisti (ANARCHY).
Kauli hizi zinaweza kupelekea machafuko katika nchi, mgawanyiko,
ubaguzi, fujo na umwagaji damu, mambo ambayo yatamwathiri kila raia wa
Tanzania bila kujali Chama chake cha kisiasa.

Kwa hiyo, Chama Cha Mapinduzi ambacho kina dhamana ya uongozi wa nchi
hii kinalaani matamshi hayo na kinawataka viongozi wa vyama vya siasa
waache kutoa matamshi ya hovyo na hatari kwa mstakabali wa Taifa letu.
Chama Cha Mapinduzi kinaitaka Serikali kufuatilia matamshi haya kwa
kina na itoe taarifa kwa wananchi.

KUHUSU WATANZANIA KUTAKA UONGOZI MPYA
Katika utangulizi wa hotuba yake amedai kuwa “watanzania kuliko wakati
mwingine wowote katika historia ya nchi yetu wameamka na kutaka
mabadiliko ya kisiasa na hasa kutaka kabisa uongozi mpya wa nchi
kutoka Chama kingine tofauti na Chama kinachoongoza hivi sasa.”

UFAFANUZI
Chama kinachoongoza hivi sasa ni Chama Cha Mapinduzi “CCM”
unapozungumza kauli kama hii lazima uangalie na hali halisi ya Chama
chenyewe kama Taasisi.

Kwanza, Chama Cha Mapinduzi kina wanachama hai wengi ambao ni
watanzania kuliko CHADEMA.

Pili, Chama Cha Mapinduzi kina mashabiki na wapenzi wastaarabu ambao
ni watanzania wengi kuliko CHADEMA.

Tatu, Chama Cha Mapinduzi katika mfumo wake hakijapata ombwe la
uongozi, kina uongozi katika ngazi za Shina, Tawi, Kata, Jimbo,
Wilaya, Mkoa na Taifa na hao wote ni watanzania. Na kama kuna Chama
chenye heshima ya kuwasemea watanzania wote kila kona ni CCM sio Chama
kingine chochote.

Nne, katika uchaguzi wa ndani ya Chama wa mwaka 2012, watanzania
wameendelea kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi ndani ya
CCM. Mpaka sasa Mashina yamekwishafanya uchaguzi kwa asilimia 97.56.
Hao walioshiriki uchaguzi huo wa mashina ni watanzania.

Tano, katika chaguzi ndogo za Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji CCM
imeendelea kuongoza na wanaopiga kura nao ni wantanzania.

Sita, Chama Cha Mapinduzi tangu 2007 kimefanikiwa kufungua matawi yake
nje ya nchi maeneo mbalimbali mfano India, Uingereza na Marekani. Hao
ni watanzania waishio katika ulimwengu wa kwanza na wanaamini kuwa CCM
bado ni imara na hata Mhe. Rais alipoalikwa juzi kuhudhuria mkutano wa
G8 alikutana na wanachama wa CCM Tawi la Marekani. Kitendo cha Mhe.
Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kualikwa G8 ni heshima kubwa
kwa Chama Cha Mapinduzi na Taifa kwa kuwa kigezo cha kumwalika
kilikuwa ni demokrasia, utawala bora, amani na utulivu nchini vigezo
ambavyo vinavutia wawekezaji kutoka nje.

Kwa hiyo, hoja ya Mhe. Zitto ni Batili (futile) kwa sababu anatazama
kwa macho ya ubinafsi kwa lengo la kugombea Urais mwaka 2015.

Uongozi mpya kabisa wa nchi ni upi? Kwa kuwa uongozi wa nchi yoyote
huru na ya kidemokrasia unapatikana kwa utaratibu wa uchaguzi wa
kawaida unaozingatia Katiba na Sheria za nchi katika mazingira ya
uhuru na uwazi na vyama vyote vinashiriki. Afafanue maana ya uongozi
mpya kabisa na namna utakavyopatikana huku akijua kabisa kwamba vyama
vyote vya siasa vitakuwa na haki ya kushiriki uchaguzi. Lazima utapata
uongozi mchanganyiko kama ilivyo hivi sasa katika mfumo huu wa vyama
vingi.

KUHUSU SERA YA MADINI YA 2009 NA SHERIA YA MADINI YA 2010

Katika hotuba yake amedai kuwa Tanzania haina sera ya Gesi asili na
kwamba, sheria ya madini ya mwaka 2010 imetokana na shinikizo la
CHADEMA na Asasi za kiraia.

UFAFANUZI
Chama Cha Mapinduzi katika ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 ambayo
inapatikana katika website ya CCM www.ccm.or.tz katika ibara ya 55 ya
ilani imeeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini kwa
kipindi cha 2005/2010, ambayo ni pamoja na kukamilika kwa sera ya
madini ya 2009 na kupitishwa kwa sheria ya madini ya mwaka 2010.

Mhe. Kabwe mwaka 2009 alikuwa wapi kutoa mchango wake?

Hoja hii ni ya CCM yeye na Chama chake wameidandia kwa malengo ya
kibinafsi na sio maslahi ya nchi.


SUALA LA URAIA WA NCHI MBILI (DUAL CITIZENSHIP)

Mhe. Zitto anadai kwamba suala la uraia wa nchi mbili ni sera ya
CHADEMA.

UFAFANUZI
Suala la uraia wa nchi mbili limekuwa ni sera ya Chama Cha Mapinduzi
na limesimamiwa na Serikali yake, hususan Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe.

Katika hotuba ya bajeti ya 2011/2012 iliyotolewa na Mhe. Bernard Membe
Bungeni katika Bunge la Nne kikao cha 31 cha tarehe 22 Julai, 2011
alisema:-

“Ni dhamira ya Wizara yangu kuona suala la uraia wa nchi mbili
linazinduliwa sanjari na Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.”

Watanzania mnapaswa kujua jinsi Zitto Kabwe anavyoiba hoja kwa manufaa
binafsi alipowadanganya watanzania waishio nchini Marekani na dunia
kwa ujumla akisema:-
“CHADEMA inataka suala hili lifikie mwisho kwenye mjadala wa Katiba.”

Huo ni uwongo mkubwa na uzushi, kwa kuwa dhamira hiyo ni ya Serikali
ya CCM na ilishawasilishwa na Waziri mwenye dhamana Bungeni na yeye
akiwepo.

6. HALI YA UCHUMI WA NCHI
Amedai kuwa uchumi unaokuwa hivi sasa sio uchumi wa watanzania bali ni
uchumi wa watu wachache kwenye sekta chache kama madini, mawasiliano
na ujenzi; hivyo kupelekea watanzania wengi zaidi ya 15m kuishi chini
ya Tshs. 500 kwa siku, kutokuwa na uhakika wa kula na kukabiliwa na
mfumuko wa bei.

UFAFANUZI
Kwanza, takwimu zake sio za kitafiti kwani hazionyeshi chanzo. Pili
hazina ulinganisho wa hali ya maisha ya wananchi wa nchi
zinazotuzunguka ili uchungu alionao moyoni uonekane waziwazi kama ni
kweli au ni uzushi.

Mhe. Kabwe amepotosha kwa makusudi ya kulinda maslahi binafsi ya Urais
wa 2015 kwa kuwa haiingii akilini kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama
takwimu hizo yeye hajazisoma.

Kwa mujibu wa kitabu cha Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2010
kilichotolewa na Wizara ya Fedha kukuwa kwa sekta ya kilimo
kumeongezeka kwa 4.2% mwaka 2010 tofauti na asilimia 3.2% mwaka 2009.
Lakini katika taarifa yake anadai kuwa uchumi wa vijijini ambako ndiko
kwenye kilimo umekuwa kwa asilimia moja tu (flat lining).

Katika uchambuzi wake wa hali ngumu ya uchumi na mfumuko wa bei kama
angelinganisha na nchi jirani angegundua kuwa mfumuko wa bei kwa
Tanzania upo chini zaidi kwa asilimia 19 ukilinganisha na nchi
zinazotuzunguka ambao mfumuko ni mkubwa zaidi mfano Ethiopia ni 30%.

Katika hali halisi ya maisha ya watanzania wa vijijini chakula chao
hakitokani na pesa, wanakula vitu vingi ambavyo haviingii kwenye
takwimu za uchumi mfano, kuku, mayai, maziwa, mihogo, viazi vitamu,
nyama n.k. Hivyo vinaliwa bila kuingia kwenye mzunguko wa soko ndio
maana hakuna mtanzania anayekufa njaa. Lakini nchi jirani wanakufa
njaa na wanakimbia nchi zao kwa njaa. Mfumuko wa bei ni tatizo la
Dunia nzima sio Tanzania peke yake.

Huyu ni mgombea Urais wa aina gani ambaye si mkweli kwa nchi yake,
hasomi takwimu na anaropoka mambo ya ndani ya nchi hovyo hovyo
duniani.

7. SUALA LA FURSA YA ELIMU
Katika hotuba yake ameeleza kuwa “leo mtoto wa maskini Tanzania hapati
elimu anayopata mtoto wa mwenye uwezo.” Na kwamba Tanzania ijiandae
kupokea bomu litakaloletwa na kundi kubwa la vijana wasio na elimu
wala ujuzi.”

UFAFANUZI
Huo ni uwongo na uzushi unaolenga kutetea maslahi binafsi. Kwa kuwa
katika uchambuzi wake amejikita kwenye shule binafsi na sio shule za
serikali ambazo zipo katika vijiji vyote Tanzania, vinatoa elimu huru,
sawa na bila ubaguzi.

Serikali ya Tanzania imetoa fursa ya Elimu kwa kila mtoto wa Tanzania
tangu awali. Mpaka imefikia wakati hata mabinti wa kazi za ndani
(house girls) hawapatikani wote wapo mashuleni.

Kuthibitisha hilo mnamo tarehe 20/9/2010 Tanzania ilipata tuzo ya
utekelezaji mzuri wa miradi ya Elimu katika ngazi za awali, elimu ya
msingi na sekondari kutoka umoja wa mataifa. Waziri Mkuu Mizengo Pinda
alipokea Tuzo hizo Mjini New York.

Hivi huyu Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA anakuwa wapi asiyaone haya
mpaka kwenda kuwadanganya watanzania waishio Marekani huko huko
ilikotolewa Tuzo?

Serikali ya CCM imejenga Vyuo vya kutosha vinavyozalisha wasomi wa
kutosha na hata bomu tunalojiandaa kulikabili ni la vijana wasomi
ambao hawana ajira na sio vijana wasio na elimu kama anavyodai yeye.

IMETOLEWA NA TAWI LA CCM MAKAO MAKUU
DODOMA
28/05/2012

Monday, 28 May 2012


M4C Ya CHADEMA Ndani Ya Marekani

 Wantazania waishio DMV Nchini Marekani wakiwa katika uzinduzi wa tawi la chadema Washington  Dc
 Uongozi wa juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika uzinduzi rasmi watawi la Chadema Washington Dc  kwenye meza ya juu wa kwanza kushoto Libe Mwangombe, akifatiwa na Mhe. Peter Msigwa,  Mwenyekiti wa tawi Mhe. Kalley Pandukizi,  Mhe. Zitto Kabwe, na Mhe. Nassari Joshua, mkutano huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mirage Hall uliopo University Of Bld, Hysattsville, Maryland Nchini Marekani.
 Mhe. Zitto Kabwe akitoa hutba kuelezea mpango mzima wa mambo yanavyoendelea nchini Tanzania


Ziara Ya Waziri Kigoda Kiwanda Cha Urafiki

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Mh, Abdala kigoda akiongea na wajumbe pamoja na Viongozi wa kiwanda cha Urafiki jijini Dar es Salaam alipotembelea kiwanda hicho leo jijini Dar es Salaam ambapo aliziona changamoto nyingi zinazozikabili kiwanda hicho ikiwemo mishahara miidogo ya wafanyakazi na akaahidi kuzifanyia kazi.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Diwani wa kata ya Ubungo  jijini  Dr es Salaam Mh, Bonifas Jacob  akieleza changamoto zinazo wakabili wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na usimamiaji mbovu wa Kiwanda hicho mbele ya Waziri.
Baadhi ya wafanyakazi, Viongozi pamoja na wajumbe mbalimbali waliohudhuria kwenye ziara hiyo wakimsikiliza Mh, Waziri kwa umakini.
Naibu Meneja uchapishaji na utiaji rangi kwenye kanga Bw, Solomon Laban(kulia) akimuelekeza waziri namana mtambo huo wa utiaji Rangi unavyofanya kazi  akikagua baadhi ya Mitambo ndani ya kiwanda hicho.
Waziri akikagua uzalishaji wa kanga kiwandani hapo.
Mh. Waziri wa viwanda na Biashara akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kiwanda hicho baada ya kumaliza matembezi.

Rais Kikwete ahutubia Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya

Picture
Rais Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa mafunzo ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala na Wakuu wa Wilaya yanayoendelea katika ukumbi wa St. Gaspar, mjini Dodoma leo (Picha: Freddy Maro)

picha: Mkutano wa CHADEMA Mtwara leo Mei 28, 2012


 
Picture: CHADEMA Mtwara Mei 28, 2012
Sehemu ya maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara na vitongoji vyake, wakiwasikiliza viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika mkutano wa hadhara wa M4C (Movement For Change), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa. (Picha na Joseph Senga via Francis Dande)
Picture: CHADEMA Mtwara Mei 28, 2012
Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, akihutubia katika mkutano wa hadhara waM4C, kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara, leo. (Picha na Joseph Senga via Francis Dande)