KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 31 October 2012


RAIS KIKWETE AZINDUA UJENZI WA BARABARA YA KWA SADALA-MASAMA, WILAYANI HAI,LEO


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Hai Mhe Novatus Makunga katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa kuzindua jiwe la msingi  na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe L:eonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe wakikata utepe mojawapo ya magreda katika eneo la sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Miundombinu Mhe John Pombe Magufuli Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe Leonidas Gama na Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe Freeman Mbowe katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Kilimanjaro  baada ya  uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani hai leo.

 
 Rais Jakaya Kikwete akiangalia chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda cha kuzalisha Tangawizikimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mambakatika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 
Rais
Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi,
kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda wakati amkaribisha kufungua kiwanda cha kusindika Tangawizi.
 
 Rais Jakaya Kikwete akifungua rasmi kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda  na Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 
 Rais Jakaya Kikwete akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kushoto ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kimnachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda
 
 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi langop kuu la Kiwanda hicho.
 
 Rais Jakaya Kikwete akikagua uzalishaji wa Tangawizi mara baada kufungua rasmi kiwanda cha kusindika Tangawizi kinacho milikiwa na Ushirika wa wakulima wa Tangawaizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 
 Rais Jakaya Kikwete akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda (kushoto) juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela ambaye amefanikisha ujenzi wa kiwanda hicho kwa asilimia kubwa.
 
 Rais Jakaya Kikwete akioneshwa chupa ya tangawizi iliyotayari kuuzwa .Kushoto  ni Meneja wa Kiwanda cha Tangawizi, kinachomilikiwa na Umoja wa Walima Tangawizi Mamba, Mhandisi Aim Luvanda akimpa maelezo  juu ya shughuli za uzalishaji mara baada ya Rais Kikwete kufungua rasmi kiwanda hicho katika Kijiji cha Goha Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.
 
 
 Rais Kikwete akisalimina na wananchi wa rika mbalimbali waliofurika katika uiwanja wa michezo wa Goha kata ya Mamba Miamba kumsikiliza.
 
 Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi cheti cha shukrani Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecela kwa kufanikisha ujenzi wa Kiwanda cha kusindika tangawizi katika Kata ya Mamba Miamba Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro. Rais Kikwete alifungua kiwanda hicho juzi.
 
 Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango Malecelaakizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kabla ya Rais Kikwete kuhutubia hadhara hiyo.
 
Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia wakazi wa Kata ya mamba Miamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro juzi.

UN ADVICES TANZANIA ON WEALTH CREATION AND ECONOMIC EMPOWERMENT.

Deputy Country Director – UNDP Tanzania Titus Osundwa giving out a statement at the launch of the project on ‘United Nations support to the Strengthening of the Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture, for Innovative Business Support Services  where he said the implementation strategy of this project is anchored on the transfer of skills, incubation of SME’s and support through the interface and collaboration between big companies and SMEs.
Some of the representatives of International Organizations, Leaders and Members of the Business Community in Tanzania and Members of The Diplomatic Corporations  who attended the launch.
 

PINDA AHUDHURIA MAZISHI YA HOUSEKEEPER WA IKULU YA ARUSHA.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa Mtundza Ikulu ya Arusha (house keeper), Lucy Samillah katika ibada ya mazishiliyfanyika nyumbani kwa marehemu, Arsha Mjini.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka mchanga kwenye kaburi la Alikuwa mwanagalizi wa Ikulu ya Arusha (House Keeper), Lucy Samilaah katika mazishi yake yaliyofanyika, Arusha.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwejka shada la maua kwenye  kaburi la aliyekuwa mtunza Ikulu ya Arusha (House Keeper) Lucy Samillah  katika Mazishi yaliyofanyika Arusha, Oktoba 31,2012. (Picha na Ofisi ya Wazieri Mkuu).

DHAMIRA YA SAMSUNG NA IMANI KATIKA SOKO LA AFRIKA INAONEKANA DHAHIRI KUPITIA MIKAKATI YA SOKO LAO.

Samsung Senior Manager Bw.  Simon Kirithi akizungumza na waandishi wa habari katika duka la kampuni hiyo lililopo Quality Center jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumzia kuanza kwa Wiki ya Samsung Tanzania 2012 mnamo Oktoba 29 hadi Novemba 3 mwaka huu, na kusema wiki hiyo imelenga kujitolea katika maendeleo ya jamii, burudani na uvumbuzi wa teknolojia, ambapo watumiaji watapata nafasi ya kushiriki na kuona bidhaa na huduma za Samsung kwa vitendo.
Afisa wa Samsunga Ms. Tessa Calleb akikabidhi Aziz Kindamba wa Clouds zawadi ya kopmyuta ndogo ya mkononi baada ya kujishia katika bahati nasibu iliyoendeshwa kwa waandishi wa habari. 
Pichani Juu na Chini ni Afisa wa Samsunga Ms. Tessa Calleb akikabidhi zawadi mbali mbali kwa washindi wa bahati nasibu kwa waandishi wa habari.
Dhamira ya Samsung na imani katika soko la Afrika, inaonekana dhahiri kwa kupitia mikakati ya soko lao na kwa kushiriki kwao wenye miradi ya jamii ambayo imeacha hisia ya kudumu miongoni mwa watu.
Sasa kwa kuonyesha zaidi dhamira za malengo yao, Samsung inaadhimisha Wiki ya Samsung Tanzania kuanzia Oktoba 29 hadi Novemba 3 2012.
 Wakati Samsung inaendelea kupanua uwepo wake Afrika, nia yake si tu kushiriki katika shughuli nyingi za jamii inapofanyia kazi – bali kuwa zaidi kuliko tu kuwepo na pia kuchangia ipasavyo na kuleta mafanikio chanya kwenye jamii ambapo wateja wake huishi.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Samsung Electronics Afrika Mashariki Jong O Lee amesema “Sisi tunaelewa kwamba kuwa na mafanikio katika bara la Afrika si kuingia tu soko la Afrika bali inahitaji tabia ya ujasiriamali nakujitolea kusaidia kujenga soko na miundombinu inayoizunguka “.
”Sisi tunatengeneza bidhaa na programu za kipekee zinazoendana na mahitaji,  rasilimali na hali ya waafrika. Sisi tunatengenezaprogramu za waafrika ambazo zina uwezo na ubunifu wa kipekee unaowajengea watu wake kwa kutoa fursa/nafasi barani. Sisi tunatengeneza huduma zinazowalenga  waafrika na zinazopelekea moja kwa moja ukuaji wao .”
 Sambamba na hili, pamoja na umuhimu wa mafanikio na ushirikiano, pamoja na biashara zao za Afrika na ushirikiano wa sekta ya maendeleo, Samsung Electronics imeandaa Wiki ya Samsung Tanzania – wiki ambayo imelenga kujitolea katika maendeleo ya jamii, burudani na uvumbuzi wa teknolojia – ambapo watumiaji watapata nafasi ya kushiriki na kuona bidhaa na huduma za Samsung kwa vitendo.
Shughuli mbalimbali zimepangwa kwa ajili ya wateja kufurahia safu mbalimbali  za bidhaa za Samsungzinazopatikana kupitia matangazo ya ofa maalum zinazotolewakwenye maduka yote ya Samsung, kutakuwa na burudani ya maonyesho ya barabarani na katika vituo vya mauzo ili kuweza kulete bidhaa karibu na wananchi; pamoja na hayo ukinunua bidhaa za samsung kuna ofa nzuri  zinazo kuwezesha kuingia kwenye droo za bahati nasibu zilizo nzuri na za kusisimua.
 Pamoja na shughuli za kusisimua zilizopangwa kwenye wiki ya samsung za kuzunguka mji wa Dar , siku ya mwisho ya wiki mnamo tarehe 3 Novemba, Jumamosi pale Hoteli ya Golden Tulip Marquee, Toure Drive itakua ni siku ya maonyesho.
Samsung imepanga shughuli mbalimbali kwenye siku ya kuzoea Samsung kwa watumiaji kupata fursa ya kujaribu bidhaa mbalimbali za Samsung katika maonyesho, kutumia faida ya bei maalum inayotolewa, na pia kushiriki katika fani mbalimbali za burudani na shughuli za michezo na maonyesho kadhaa ya wasanii mbalimbali na kuwakaribisha wateja wote watakaohudhuria siku yamaonyesho ya Samsung.
Wiki ya Samsung imepangwa kufungwa rasmikwenye sherehe za vijana za ufukweni mwa bahari paleMbalamwezibeach iliyoko Mikocheni ‘B’ kwa Warioba ambapo kutakuwa na zawadi nyingi za kushindaniwa tarehe hiyo ya Novemba 3-Jumamosi kuanzia saa 11 jioni.
 Mbali na shughuli za maonyesho kwa watumiaji, Samsung pia itasaidia jamii kwa kutoa huduma za bure kwa matengenezo ya bidhaa za Samsung (kama vile notebook,kompyuta , kamera na simu za mkononi) na kuongeza uelewa kuhusu hatari za kutumiavifaa vya teknolojia bandia.
 Leealiendelea kusema; “Hii ni hatua ya kusisimua sana kwa Samsung kama kampuni ambayo hivi karibuni imepanuakiwango chake cha warantii kwa wateja wenye bidhaa zilizo na  (Visual Display), vifaa vyenye teknologia ya IT, Vifaa vya digitali, upigaji Digitali na bidhaa za ufumbuzi za Digital Air.
Wateja sasa kufurahia kiwango cha chini miezi 24 ya warantii kwenye bidhaa zote za Samsung, zilizonunuliwa kutoka 1 Mei 2012, na hakuna malipo ya ziada ya hii Kampeni ya Huduma za matangenezo ya bure inaturuhusu kuendelea kuonyesha dhamira hii.”
   “Samsung inasikiliza soko, inajenga ushirikiano na kweli inadhamiriakwa Afrika na watu wake na Wiki ya Samsung, pamoja na kampeni yetu ya Huduma ya matengenezo bure, hii ni mfano mmoja tu wa jinsi sisi tunavyofanikisha hili,” alihitimisha Lee.

Ni Kama Wanasema...!

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasin katika hafla ya ufunguzi rasmi  wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.
Reactions::

JK Azindua Barabara Ya Rombo- Tarakea

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaidiwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mbunge wa Rombo Mhe Joseph Selasini kukunjua pazia kama ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na washika dau wa miundombinu wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi wa barabara ya KM32 kutoka Mkuu Rombo hadi Tarakea leo Oktoba 30, 2012 kijijini Tarakea, wilaya ya Rombo mkoa wa Kilimanjaro ambako Rais Kikwete yuko katika ziara ya kikazi ya siku nne


 PICHA NA IKULU

Mama Tunu Pinda Azindua Maonyesho Ya Wanawake

Mke wa Waziri Mkuu Mana Tunu Pinda akitoa hotuba ya kufungua Maonyesho ya Wanawake Wajasiriamali (MOWE) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jana jijini Dar es Salaam ambapo amewahimiza wajasiriamali kujiunga katika ushirika ili iwe rahisi kusaidiwa kupata mikopo, kutafuta masoko, kupanga bei nzuri ya bidhaa zetu, kupata utaalam na teknolojia mpya. Kauli Mbiu ya ya Maonyesho hayo mwaka huu ni “Msichana Amka, Ujasiriamali ni Ajira”.
Mama Tunu Pinda akikata utepe kuzindua Mradi wa Uwezeshaji Kiuchumi wa Maendeleo ya Wanawake Wajasiriamali (WEDEE) Ulio chini ya Shirika la Kazi Duniani (WEDEE) wakati wa ufunguzi wa Maonyesho ya Wanawake wajasiriamali ya MOWE yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mama Tunu Pinda (katikati) katika picha ya pamoja baada ya kufungua maonyesho ya MOWE 2012


Vibanda vya maonyesho

Magazeti Leo Jumatano