KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Saturday 22 January 2011

MBUNGE Nyalandu akabidhi matrekta wakulima singida

Jumamosi, 22, January 2011
Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, akitoa maelekezo muda mfupi kabla kukabidhi matrekta 12 kwa wanachama wa Mtinko Saccos.







WANACHAMA 12 wa Mtinko Saccos ya Kijiji cha Mtinko, wilayani Singida, wamekopeshwa matrekta 12 yenye thamani ya zaidi ya Sh202 milioni.

Akizungumza kwenye kukabidhi matrekta hayo, Mwenyekiti wa Saccos hiyo, Elinywesia Sima, alisema lengo ni kuwezesha wanachama wao kuongeza kipato kwa kutumia nguvu kidogo kulima mashamba yao.

Matrekta hayo yalikabidhiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Lazaro Nyalandu.

Sima alisema kati ya matrekta manne makubwa, matano ni ya aina ya HP 20 na matatu ni aina ya Power tiller.
Alisema lengo la mkopo huo, ni kutekeleza azma ya Kilimo kwanza ili wakopaji waweze kujikwamua kiuchumi na kupunguza au kutokomeza kabisa umaskini.

“Wanachama hawa waliokopa matrekta, wameahidi kulima kilimo cha biashara ili waweze kuinua hali zao kiuchumi na kuwa na uhakika wa chakula kwa kipindi chote cha mwaka,” alisema huyo.

Alisema msukumo utaelekezwa zaidi kkwenye kilimo cha alizeti, zao ambalo lina soko la uhakika na litauzwa kwa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani.

Kwa mujibu wa mwenyekiti, Mtinko Saccos inafanya kazi kwenye vijiji 10; Mtinko, Minyenye, Ndughwira, Mughanga, Mpambaa, Malolo, Kijota, Nduu, Mitonto na Ikiwu.

Kwa upande wake, Nyalandu aliwataka wanachama hao kutumia vizuri  matrekti hayo kupanua kilimo chao.

No comments:

Post a Comment