Mbunge wa Sumve (CCM,)Mheshimiwa Richard Ndasa,akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari,(hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam, kuhusu habari iliyochapishwa na gazeti la Mwanahalisi toleo la wiki hii ambazo zilielezea hatua ya bunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais, kufuatia sakata la kusimamishwa kazi kwa aliyekuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo na kurudishwa tena kazini. Kulia ni mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu.Habari na Picha na Mdau Victor Makinda
--
Akizungumzia habari iliyochapishwa na gazeti hilo,Mheshiniwa Ndasa alisema kuwa gazeti la Mwanahalisi limechapisha habari za kizushi na za uongo zenye lengo la kufitinisha Bunge na Rais.Aliongeza kusema kuwa wakati Jairo anarudishwa kazini na Katibu Mkuu, Luhanjo, Bungeni mjini Dododma hapakuwa na hatua yoyote ya wabunge kupanga kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kufuatia kuruhusiwa kwa Jairo kuendelea na kazi.
Akifafanua kuhusu uamuzi wao wa kutolea ufafanuzi na kukanusa habari hiyo, Ndasa alisema wao kama wabunge wa CCM, hawatopenda kuona kiongozi wa nchi anazushiwa habari zisizo na ukweli wowote.
No comments:
Post a Comment