KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 5 September 2011

Kamati Teuli Iliyoundwa na Bunge Kuchunguza Sakata la Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg.David Jairo Yaanza Kazi Rasmi

Wajumbe wa Kamati Teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo ikiwa kwenye kikao chake leo jijini Dar es Salaam.Picha na Owen Mwandumbya-Bunge
---

Wajumbe wa Kamati Teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo kuchangisha pesa kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya Wizara pamoja na hatua ya katibu Mkuu kiongozi kuitolea taarifa ya uchunguzi mbele ya waandishi wa Habari kabla ya kuwasilishwa Bungeni imeanza kukutana leo katika Ofisi ndogo ya Bunge chini ya uenyekiti wa Mhe. Injinia Ramo Makani (CCM), mbunge wa Tunduru Kaskazini,
.
kamati hiyo inayoundwa na mhe. Goesbert Blandes (CCM), Mbunge wa Karagwe, mhe. Mchungaji Israel Natse (Karatu-Chadema), mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF) na mhe. Martha Jachi Umbulla (CCM). Mbunge wa Viti Maalum, inafanya kazi kwa kuongozwa na hadidu tano za rejea ambazo ni:

kuchunguza utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilishwa kwa uwasilishaji wa Hotuba za bajeti za wizara bungeni na kwamba, hadidu hiyo ya kwanza itakuwa na vipengele vitatu. Vipengele hivyo ni pamoja na:
·kuchunguza uhalali wa utaratibu huo kisheria na kwa mujibu wa kanuni, iwapo fedha hizo huwa zinakasimiwa katika bajeti husika pamoja na matumizi halisi ya fedha zilizokusanywa.

Hadidu rejea ya pili ni kupitia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu uchunguzi alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini kuchangisha fedha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni,

Hadidu rejea ya tatu ni kuchunguza mfumo wa Serikali kujibu hoja zinazotolewa bungeni na taratibu za kuarifu Bunge matokeo ya utekelezaji wa hoja hizo".
Hadidu rejea hiyo ya nne ina vipengele viwili ambavyo ni kuchunguzwa kwa usahihi wa utaratibu uliotumiwa na Katibu Mkuu Kiongozi kwa suala la Jairo na kubaini iwapo utaratibu huo umeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.

Hadidu ya rejea ya tano ni kuangalia nafasi ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi huo.

No comments:

Post a Comment