Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa tuzo na Waziri Mkuu wa Antigua and Barbuda Mh.Winston Baldwin Spencer kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya afya, teknolojia na maendeleo kwenye hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na taasisi ya South-South katika hoteli ya Waldorf Astoria jijini New York Jumatatu usiku.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiikabidhi tuzo hiyo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe baada ya kuipokea.Nyuma ya Mh. Membe ni Balozi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa Mh Ombeni Sefue(kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh Mwanaidi Maajar
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa shukrani kwa kupewa tuzo hiyo. Marais Paul Kagame wa Rwanda, Abdoulaye Wade wa senegal na Mwai kibaki wa Kenya, pia walipokea tuzo kwa michango yao katika maendeleo ya nchi zao
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipewa shada ya maua kama pongezi kwa kupokea tuzo
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Dkt Marion Bergam, Mkurugenzi wa miradi ya Health Care Projects ya Miracle Corners of the World katika mkutano wa kwanza wa kuhimiza hatua zichukukuliwe dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza,hususani ya kinywa.Serikali ya Tanzania ndiyo iliyodhamini mkutano huo uliofanyika Chuo Kikuu cha New York kitivo cha meno
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Dkt Asha Rose migiro kwenye hafla hiyo ya Roll Malaria
Madaktari Bingwa kutoka Wizara ya Afya na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakisubiri kugawa vipeperushi kwa wanaoingia mkutanoni
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Profesa Makame Mnyaa Mbawala (kati), Waziri wa Maliasili na Utalii (shoto) pamoja na Mbunge wa Bukombe,Profesa Kulikoyela Kahidi wakiperuzi maandiko kuhusiana na mkutano huo wa kuhamasisha vita dhidi ya magonjwa ya kinywa
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wa zanzibar Mh Juma Duni Haji (kati) na wasaidizi wake kwenye hafla hiyo
Sehemu ya ujumbe wa Watanzania kutoka sekta ya utalii.kwa Habari na Picha Mbalimbali za Muendelezo wa Ziara ya Rais Jakaya Kikwete Nchini Marekani Endelea Kuperuzi
No comments:
Post a Comment