Watu 242 wameuawa mkoani hapa kwa imani za kishirikina katika kipindi cha januari 2010 hadi juni mwaka huu.
Kamanda wa Polisi wa mkoani Shinyanga, Diwani Athumani, aliwambia wadau wa ulinzi shirikishi kuwa matukio hayo yamekithiri hasa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu.
Akitoa taarifa yake mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dk. Yohana Balele, na wadau wa jeshi hilo mkoani hapa, Kamanda huyo alisema katika kipindi cha Januari hadi Desemba 2010, watu waliouawa kwa imani hizo ni 63.
Kamanda huyo aliongeza kuwa katika kipindi cha kuanzia Juanuri hadi Juni mwaka huu, watu 36 waliuawa ikilinganishwa na watu 18 mwaka 2010 ambao ni ongezeko la watu 18 na sawa na asilimia 100 ya ongezeko la mauaji ya aina hiyo.Alisema watu 45 waliuawa katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ikilinganishwa na watu 29 waliouawa katika kipindi kama hicho mwaka 2010 na kuwepo kwa ongezeko la watu 16 sawa na asilimia 55.
Kutokana na hali hiyo, alisema jeshi hilo limejipanga na kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa mauaji hayo yanapungua kama si kukoma kwa kutumia moja ya mbinu zake za kuielimisha jamii na kuihamasisha kuacha mauaji hayo.
Kwa upande wake, Balele, alikemea tabia ya wakazi wa Mkoa wa Shinyanga ya kujichukulia sheria mkononi na kuwaua watu wasiokuwa na hatia.
Takwimu za mauaji hayo zinaonyesha kuwa Wilaya ya Bariadi ndiyo inayongoza kwa mauaji ikifuatiwa na Bukombe na Kahama huku Maswa na Manispaa ya Shinyanga zikiwa na idadi ndogo.
Hongera kaka mambo yako nayaona,tupo pamoja katika kuielimisha jamii yetu.Malampaka moja nasi tu wa moja.
ReplyDeleteKaka nimeikubali blog yako kwa mwendo huu malampaka lazima ielimike
ReplyDelete