KARIBUNI
Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.
Sunday, 27 May 2012
Kutoka Facebook: Nape Asema; " Inatosha!"
"INATOSHA!! Mmewadanganya sana watu, utadhani wakivaa magwanda matatizo yao na ya nchi yanakwisha!! Mnatafuta biashara ya magwanda yenu!! Karibuni nazindua operation ya VUA GWANDA NA GAMBA VAA UZALENDO!! kinachopungua kwetu, Afrika na Dunia nzima ni UZALENDO, sasa tunakwenda kuwavua magwanda na magamba na KUWAVISHA UZALENDO na ndo DAWA INAYOHITAJIKA DUNIANI LEO. Stay tuned!!!! Soon operation hii itaanza tufute uongo!"- Nape Nnauye
CHADEMA Wafunga Barabara Kwa Saa 2 Baada Ya Mkutano
Wananchi wakitembea kwa mtindo wa maandamano kutoka eneo la mkutano jangwani kuelekea ofisi za CHADEMA kinondoni.
Mh.Mbowe na Mnyika wakiwa wamesimama kwenye gari wakati wa matembezi wakitoka kwenye mkutano
Godbless Lema akiwa juu ya gari huku akishangiliwa na vijana jioni baada ya mkutano
Mbowe akiwatania wanachama ofini kinondoni baada ya wananchi kuanza kudai chama kimfukuze John Shibuda.Alikuwa akijifanya hasikii wanachosema na hapa anajaribu kuwasikiliza zaidi.hata hivyo Mbowe aliwaondoa wasiwasi na kusisitiza kuwa chama kinao utaratibu wa kushughulika na viongozi wanaokiuka maadili ya chama na kuwaomba wawaamini kama viongozi kuwa wanaouwezo wa kulishughulikia jambo hilo na mengine
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akiwaaga wananchi waliokuwa wamefurika makao makuu ya chama kinondoni walikofika wakitokea jangwani usiku huu
Sehemu ya umati uliowasindikiza viongozi wa chadema toka jangwani hadi kinondoni.wamesambaa yapata saa 2 usiku.
Viongozi wa chadema wakifurahia kadi nyingi za CCM zilizorudishwa leo jioni kwenye mkutano
Sugu akimwaga mistari.

Stars vs Malawi Hakuna Mbabe
Mpira umekwisha kama wanavyoonekana katika picha wachezaji wa Taifa Stars wakitoka nje ya uwanja kwenda mapumziko, Si Taifa Stars wala Malawi ambayo imepata goli, hata hivyo wamalawi wameshambulia mara nyingi katika lango la Taifa Stars katika kipindi cha kwanza, lakini uimara wa mabeki pamoja na Golikipa Juma Kaseja umesaidia Wamalawi hao kutopata goli , Taifa Stars yenyewe imefanya mashambulizi ya hatari mawili tu! hata hivyo haikuwa bahati yao ambapo mpaka mwisho wa mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya 0-0.
Wachezaji wa timu ya taifa Taifa Stars wakiingia uwanjani jioni hii kwa ajili ya kupasha mwili kabla ya mpambano wake wa kirafiki na timu ya taifa ya Malawi The Flames
Wachezaji wa timu ya Malawi wakipasha mwili kabla ya kuingia uwanjani kukwaana na Taifa Stars jioni hii kwenye uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa akiba wa timu ya Taifa Stars wakijifua kabla ya mpambano huo jioni hii.Timu ya Malawi iko safarini kuelekea nchini Uganda ambako itakipiga na timu ya Uganda Cranes.
Mpambano huo unafanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Wednesday, 23 May 2012
Makao Makuu Ya Benki Ya Azania Kuhamia Mawasiliano Towers
UONGOZI wa benki ya Azania umeridhia uhamisho wa makao makuu ya benki hiyo kutoka Masdo House, mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam kwenda jengo la Mawasiliano Towers iliyopo mkabala na barabara ya Sam Nujoma kuanzia Jumatatu wiki ijayo kwa lengo la kuwatumikia wateja wa benki hiyo katika mazingira yenye nafasi ya kutosha.
Hata hivyo, tawi la Masdo litaendelea kuwahudumia wateja waliopo katikati ya Jiji huko makao makuu mapya ya benki hiyo yaliyopo Mawasiliano Towers yakitoa huduma za kibenki kwa maeneo yaliyopo karibu na Ubungo, Mwenge ,Sinza na mengineyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa benki hiyo kwa vyombo vya habari jana, benki ya Azania itaendelea na mpango wake wa kujiimarisha zaidi kwa kuendelea kufungua matawi zaidi nchini ikiwa na lengo la kusogeza huduma za kifedha karibu na watu na pia kuhakikisha usalama kwa pesa zao.
Kupitia taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo Charles Singili alisema benki yake ipo mbioni kufungua tawi jingine jipya katika Wilaya ya Geita na maeneo mengine yakiwemo Lamadi, Katoro na Kagongwa ifikapo mwisho wa mwezi ujao, hatua ambayo itasaidia kuimarisha uwepo wa benki hiyo katika kanda ya ziwa.
"Tunatarajia kufungua matawi mengine zaidi nchi nzima ifikapo mwisho wa mwaka huuambayo yatasaidia benki yetu kuwa kitovu cha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati nchini.

“Tangu benki ifunguliwe mwaka 1995, benki imekuwa haraka hali ambayo imesababisha mali za kampuni kufikia shilingi bilioni 190 mwishoni mwa mwaka 2011,” alisema Singili.
Singili aliongeza kuwa benki yake imelenga zaidi katika kutoa huduma za kibenki za kipekee kwa bei nafuu ukiilinganisha na mabenki mengine.
“Nawahakikishia kwamba tutaendelea kutoa huduma za kipekee zinazokidhi mahitaji ya kila mteja wetu kwa upekee wake. Katika miezi sita iliyopita benki imejikita katika mpango madhubuti wa kujitanua kwa kufungua matawi matatu katika maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam, Arusha mjini katika barabara ya Wapare na mtaa wa sokoni jijini Moshi,” alisema.
"Ninawaomba wateja wa benki ya Azania wa sasa na umma kwa ujumla kuendelea kupata huduma mbalimbali za kibenki na huduma zinazotolewa na benki hii ya Kitanzania yenye mafanikio," alisema.
Benki ya Azania iliaanzishwa mwaka 1995 kama Adili Bancorp Limited baada ya Serikali kuruhusu mfumo wa uchumi wa soko huria na kwa sasa benki hiyo ina wanahisa wakuu wakiwa pamoja na mashirika ya serikali yakiwemo, National Social Security Fund (NSSF) 34.8%, Parastatal Pensions Fund (PPF) 30.1%, Public Service Pensions Fund (PSPF) 17.2%, Local Authorities Pensions Fund (LAPF) 14.2%, na mengine.
Tanzania Yadhamilia kuwepo Kuweka Mazingira Ya Upatikanaji Wa Msaada Wa Kisheria
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Dk. Alberic Kacou akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP.
Dk. Kacou amesema warsha hii ya Msaada wa Kisheria ni hatua nyingine katika kuelekea kuondoa vikwazo katika uwezeshaji wa Kisheria na kupatikana kwa haki kitu ambacho kimeathiri kwa kiwango kikubwa bara hili katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya watu, mali, Uraia, huduma za kijamii na kukosekana kwa fursa za maendeleo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki
Dk. Kacou amesema warsha hii ya Msaada wa Kisheria ni hatua nyingine katika kuelekea kuondoa vikwazo katika uwezeshaji wa Kisheria na kupatikana kwa haki kitu ambacho kimeathiri kwa kiwango kikubwa bara hili katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na maisha ya watu, mali, Uraia, huduma za kijamii na kukosekana kwa fursa za maendeleo. Kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki na kushoto ni mmoja wa maafisa wa makao makuu ya UNDP New York Shelley Inglis.
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angela Kairuki akisoma hotuba wakati akifungua rasmi warsha ya Mpango wa Msaada wa Kisheria Barani Afrika iliyoandaliwa na UNDP na kuhudhuriwa na wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji Tanzania.
Katia ufunguzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam Mh. Kairuki amesema Serikali ya Tanzania imefanya jitihada mbalimbali za kuboresha huduma za misaada ya Kisheria haswa kwa watu ambao ni vigumu kuupata msaada huo, ambao wengi wao wanaishi katika maeneo ya vijijini.
Kauli mbiu ya Warsha hiyo ni " Taking Forward Legal Aid Programming in Africa: Experiences and Lessons in Policy and Programming".
Baadhi ya wadau wa masuala ya sheria kutoka mataifa mbalimbali barani Afrika wakiwemo wenyeji Tanzania wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mh. Angela Kairuki.
Kamati Ya PAC Kutembelea Waathirika Wa Mabomu Mbagala Kuu
Wajumbe wa kamati ya PAC wakiwa kwenye mkutano wa utoaji taarifa ya maafa ya Mabomu Mbagala chini ya Mwenyekiti John Cheyo
Wakiangalia orodha ya malipo ya waathirika wa mabomu ya Mbagala
Muathirika Mzee Steven Gimongi (shoto) akitoa maelezo alivyoathirika wakati wa mabomu mbele ya Mk wa Kamati ya ( PAC )John Cheyo
Mwenyekiti wa( PAC) John Cheyo (koti) ,MP wa Kigamboni Dk. Faustin Ndugulile (kaunda) pamoja na baadhi ya wajumbe wa PAC na watenda
Mbunge wa Kigamboni Dr. Faustin Ndugulile (kaunda suti) akiwasikiliza baadhi ya waathirika wa mabomu huko Mbagala Kuu.
Tigo Waanzisha Promosheni Ya Xtreme Pack
Meneja wa Huduma za malipo ya kabla Tigo Bw, Suleiman Bushagama akizungumza na waandishi wa habari leo hii makao makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam, katika uzinduzi wa promosheni mpya ya iitwayo Xtreme Pack ambapo mteja wa tigo anaweza kutuma meseji mbili za kulipia na kupata meseji tano za bure kwenda mitandao yote nchini.
Kwakupiga *148*01# au kutumaneno XTREME kwenda namba 15509, wateja wa huduma yakulipia kabla watafurahia huduma za thamani ambazo ni pamoja na dakika 15 za muda wa maongezi zitakazowawezesha kupiga simu Tigo kwa Tigo, sms 100, 50 MB kwa ajili ya kuperuzi facebook, kutumia mtandao, E-mail pamoja na Twitter,vyote hivyo kwagharama ya Tsh 450 nakuokoa sh 4,600! Pia tigo itatuma ujumbe mfupi wa maneno bure kwa wateja wao, kuwataarifu juu ya ukomo wa matumizi ya vifurushi vyao na kuwaruhusu kujiunga tena kama watahitaji.
Promosheni hiyo inaanza kutumika rasmi kesho kushoto ni Titus Kafuma meneja wa Tigo internet na kulia ni Alice Maro Msemaji wa Tigo, Naye afisa mahusiano wa Tigo Bi Alice Maro alisema kuwa wanatafuta njia thabiti ya kuhakikisha kuwa wateja wao wanapata huduma zinazoendana na thamani ya pesa zao.
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE)
Mmoja wa waandishi wa habari Omary Katanga kutoka Redio one akiuliza swali kwenye mkutano huo pamoja na waandishi wa habari wengine wanaoonekana nyuma yake.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kwenye uzinduzi huo wa Xtreme Pack ya Tigo.
Subscribe to:
Posts (Atom)