KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Monday, 18 February 2013

WanaCCM Gongo la Mboto wampongeza Jerry Silaa kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.

Baadhi ya  kinamama wa Gongo la Mboto ambao ni wananchama wa CCM wakiwasili kwenye Uwanja  uliopo karibu na reli Gongo la Mboto katika mkutano wa hadhara wa kumpongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Jerry Silaa baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. (Picha na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Mstahiki Meya Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akisalimiana na waendesha Boda boda wa Gongo la Mboto waliofika kumlaki akitokea mjini Dodoma.
Msafara wa waendesha Boda boda ukimsindikiza Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa kwenye viwanja vya Gongo la Mboto alipoandaliwa sherehe ya kumpongeza iliyoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
Watoto waliokuwa pembezoni mwa barabara wakimpungua kwa furaha Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa alipokuwa akipita na msafara wake.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya viongozi wa CCM wakimlaki Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa katika Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto alipopita kutia baraka ofisi hizo akielekea kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akitia saini kitabu cha wageni cha Ofisi za CCM kata ya Gongo la Mboto.
Waendesha boda boda wa Gongo la Mboto wakitia mbwembwe katika mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa aliyeteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Msafara wa Jerry Silaa ukiwasili uwanjani hapo kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Gongo la Mboto.
Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akipunga mkono kwa wananchi, WanaCCM waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza kuchaguliwa nafasi nyeti ya Chama cha Mapinduzi.
Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM taifa Jerry Silaa akivishwa skafu ya chama mara baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Gongo la Mboto.
Jerry Silaa akivishwa lubega ya kimasai baada ya kuwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana Gongo la Mboto jijini Dar.
Pichani juu na chini ni Baadhi WanaCCM wa kata ya Gongo la Mboto wakimpongeza Jerry Silaa baada ya kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM Taifa wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza katika viwanja vya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya umati wa wakazi wa Gongo la Mboto wakubwa kwa wadogo waliohudhuria mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Wanenguaji wa Mashujaa Band wakicheza staili ya Boda boda na Wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara.
“UTU UZIMA DAWA KWA RAHA ZETU”…Rappa wa Bendi ya Mashujaa akicheza sambamba na kinamama wa Kata ya Gongo la Mboto wakati wa sherehe za kumpongeza Jerry Silaa zilizoenda sambamba na mkutano wa hadhara.
Jukwaa kuu la viongozi mbalimbali wa chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki katika mkutano wa hadhara uliofanyika mwishoni mwa wiki Gongo la Mboto jijini Dar.
Katibu Mwenezi wa CCM Mtwara Bw. Haroun Maarifa akitoa salamu kwa wana CCM wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Wana CCM wa Gongo la Mboto wakitia manjonjo kwenye mkutano huo.
Mbunge wa Ukonga Mh. Eugene Mwaiposi akizungumza na wananchi wa Gongo la Mboto wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ya maendeleo ya Wakazi wa jimbo lake yanayopangwa kufanywa na Serikali kwa manufaa ya wakazi wa maeneo hayo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa akizungumza machache na wananchi wa kata ya Gongo la Mboto kabla ya kumkaribisha Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa kuhutubia wananchi katika mkutano huo.
 Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa Jerry Silaa akisindikizwa Jukwaani kwa staili ya aina yake ya kufagiliwa njia na WanaCCM waliokuwa wakibiringika mpaka kwenye ngazi za jukwaa. Anayemsindikiza ni Diwani wa Kata ya Tabata Hajati Mtumwa Mohamedi.
“Karibuni kwenye Chama chenye mshikamano na Sera za Ukweli” ndiyo maneno ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa wakati akigawa kadi  kwa Wanachama wapya wa Gongo la Mboto walipoamua kujiunga baada ya kukolewa na sera za CCM wakati wa mkutano huo.
Zoezi la ugawaji kadi kwa wanachama wapya likiendelea. Kulia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abillahi Mlewa.
Pichani juu na chini ni Wanachama wapya wa CCM wakila kiapo mbele ya Mjumbe wa kamati kuu na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa na viongozi mbalimbali wa Chama wakati wa mkutano wa hadhara ulioenda sambamba na sherehe za kumpongeza Jerry Silaa.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Gongo la Mboto Mh. Jerry Silaa akizungumza na wananchi wa Kata yake ya Gongo la Mboto ambapo amewasihi viongozi wa CCM ngazi za Chini kuhakikisha wanafuatilia na kutafutia ufumbuzi  kero zinazo wakabili watu wanaowazunguka.
Mstahiki Meya ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na wana CCM kwa ujumla kufuatia kuteuliwa na Mh.rais kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na kusema ofisi za chama zinatakiwa kuwa wazi kuanzia ngazi ya kata mpaka mkoa ili wananchi waweze kufika kutoa kero zao.
Aidha amewataka viongozi wenzake kufanyakazi kwa ushirikiano na uadilifu, na kuwa wale viongozi wachache wasio waadilifu watashughulikiwa kikamilifu ili kuleta ufanisi ndani ya chama.
Baadhi ya wananchi wa Gongo la Mboto wakichukua taswira ya Diwani wao Jerry Silaa wakati wa mkutano wa hadhara.
Mmoja wachekeshaji katika mikutano ya CCM wanaofahamika kama Aki na Ukwa akimwombea Dua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa mara baada ya kuzungumza na wana CCM wa Gongo la Mboto.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na wananchi wa Gongo la Mboto mara baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Jerry Silaa akisalimiana na mmoja wa watoto waliohudhuria kwenye mkutano wa hadhara.
“Asante kwa kuonyesha upendo…Mume wa mtu mie” ndivyo anavyoonekana kusema Mh. Jerry Silaa akimwambia mwana CCM mkereketwa aliyekwenda kumfuta jasho kwa kutumia Khanga yake.

Baba Mtakatifu aanza wiki ya kufunga na kutoonekana hadharani.

Baba Mtakatifu Benedict wa 16 ameanza wiki yake ya mafungo ya kiroho ambapo atakuwa haonekani hadharani kwa wiki nzima ikiwa ni mwanzo wa safari yake ya kuelekea kuachia rasmi uongozi wa kanisa Katoliki na kusema kuwa ana matumaini ibada zake zitakuwa na mafanikio.
 Baba mtakatatifu atabakia Vatican na baadhi ya wasaidizi wake wa karibu kwa ajili ya ibada za awali za sikukuu ya Pasaka na atapata mapumziko mafupi kila siku kwa ajili ya kuonana na katibu wake Georg Gaenswein, ili kuyashughulikia masuala ya dharura ya kanisa.
 Baada ya wiki nzima ya ibada, Baba Mtakatifu atakutana na rais wa Italia, Giorgio Napolitano, tarehe 23 Februari kushiriki ibada ya Jumapili yake ya mwisho ifikapo tarehe 24 mwezi huu na kuzungumza hadharani kwa mara ya mwisho mbele ya waumini wapatao 10,000.
Kiongozi huyo wa kanisa Katoliki duniani ataachia uongozi rasmi tarehe 28 mwezi huu na inasemakana kuwa Waziri wa Utamaduni wa Vatican Kadinali Gianfranco Ravasi ndiye anayeonekana mtu mwenye nafasi kubwa ya kuchukua nafasi yake kwa muda mfupi au mrefu.

Rais Kikwete aomboleza kifo cha Padre Evarist Mushi aliyepigwa risasi visiwani Zanzibar.

Gari liliacha uelekeo na kugonga nyumba baada ya Padre Mushi kupigwa risasi (Picha na Francis Dande).
Gari alimokuwa Padre Mushi (Picha na Francis Dande).
(Picha na Othman Maulid Othman-Shirika la Magazeti ya Serikali Zanzibar).

Waziri Dkt Nchimbi (wa pili kushoto) akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mohamed Aboud na maafisa wengine walipotembelea eneo la tukio jana. (Picha na Francis Dande).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki  mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushi na kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.