KARIBUNI

Pata habari za kila siku, burudani,matangazo, na mengineyo mengi pia unaweza kuacha maoni yako kuhusu tovuti hii.

Wednesday, 27 June 2012


Matukio mbali mbali hospitali ya Muhimbili leo

Madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam wakimpakia kwenye Gari Daktari Mwenzao aliepatwa na Mkasa wa Kutekwa Nyara na watu wasiojulikana na ambao walimjeruhi vibaya sana,Dk. Steven Ulimboka aliepatwa na mkasa huo usiku wa kuamkia leo huko katika msitu wa Mabwepande,jijini Dar
Wanahabari wakihangaika kupata picha ya Dk. Steven Ulimboka alieinginzwa kwenye gari hiyo tayari kwa kupelekwa kwenye Taasisi ya Mifupa (MOI) kwa matibabu zaidi.
Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakiisukuma gari iliyokuwa imempaki Dk. Stevan Ulimboka.
Madaktari na Wauguzi wa Muhimbili wakiwa wamesimama huku wakizungumzia hali iliyompaka mwenzao.

Wanahabari wakitafuta taswira.
hakuna kazi iliyokuwa ikifanyika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati Dk. Ulimboka akifikishwa hospitalini hapo.









No comments:

Post a Comment