SUMATRA Yatoa Msaada Wa Vifaa Vya Milioni 2.2 Hospitali Ya Mwananyamala Na Moi
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra),Ahmad Kilima (kulia), akimkabidhi vifaa mbalimbali na madawa Mganga Mkuu Mfawidhiwa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani kwa ajili ya wagonjwa wa haospitali hiyo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Msaada huo umetolewa na Sumatra kwa ajili ya kuwafariji wagonjwa wa Hospitali hiyo wakati wa siku hizi za sikukuu
Maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), wakiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ahmad Kilima (wa sita kulia), pamoja na
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani (Aliyeshikana mikono na Mgurugenzi huyo), wakiwa na vifaa mbalimbali na dawa
vyenye thamani ya sh.milioni 2.2 kabla ya kuwakabidhi wagonjwa wa Hospitali hiyo ikiwa ni kuwafariji katika kipindi hiki cha sikuukuu za mwisho wa mwaka.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani (Aliyeshikana mikono na Mgurugenzi huyo), wakiwa na vifaa mbalimbali na dawa
vyenye thamani ya sh.milioni 2.2 kabla ya kuwakabidhi wagonjwa wa Hospitali hiyo ikiwa ni kuwafariji katika kipindi hiki cha sikuukuu za mwisho wa mwaka.
Ofisa Habari wa Sumatra Daud Mziray akigawa vifaa hivyo kwa wagomjwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), Ahmad Kilima akigawa vitu hivyo kwa akina mama waliopo wodi ya wazazi.
Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mwananyamala Sophinias Ngonyani, akiwaelekeza jambo maofisa wa Sumtra na Kaimu Mkurugenzi baada ya kuwasili
hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa msaada huo.
Na: Dotto Mwaibale
MAMLAKA ya Udhibiti wa Usafiri
wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra), imetoa vitu mbalimbali vyenye thamani
ya sh.milioni 2,200,000 kwa wagonjwa waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa
(MOI) na Hospitali za Mwanayamala ikiwa ni kuwafariji katika kipindi
hiki cha sikukuu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi
zawadi hizo mwishoni mwa wiki Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Ahmad
Kilima alisema Sumatra imechukua hatua hiyo kwa lengo la kuwafariji
wagonjwa hao.
“Tumetumia fursa hii ya sikuku
kushirikiana na Hospitali hizo katika kuchangia na kutoa msaada wa vifaa
na madawa kwa akina mama waliopo wodi za wazazi kuwafariji” alisema
Kilima.
Alisema hatua hiyo ni kuonesha
Mamlaka kujiona inawajibu wa kuwa fanya akina mama hao ambao wapo
hospitalini hapo kujisikia kuwa nao ni sehemu ya watanzania wengine
ambao wako katika harakati za kujenga Taifa wakiwa na Afya njema katika
kipindi hiki cha mwisho wa mwaka wa 2012.
Alilisema walilazimika kwenye
Taasisi ya Mifupa (MOI), kwa kuwa kuna majeruhi wanaotokana na ajali za
vyombo vya moto ambao ni wadau wao wakubwa.
“Majeruhi wa ajali kwa namna
moja ni wadau wetu kwa sababu ya vyombo walivyotumia wakati wakipata
ajali ndio maana tukaguswa kuja kuwafariji kwa kuwapa zawadi” alisema
Kilima
Kilima alivitaja vifaa hivyo
pamoja na madawa kuwa ni dawa aina ya Fefol kwa ajili ya kuongeza damu
akina mama wajawazito 100, pamba za kujihifadhi akina mama na Kanga.
Vitu vingine ni sabuni detal kwa
ajili ya watoto, detal ya maji, nepi, mafuta ya kupaka watoto wadogo,
juice, nguo za watoto wachanga, sabuni za kufulia nguop na Toilet papers
No comments:
Post a Comment