Katika kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 49 ya Mapinduzi Dkt. Shein azindua Bohari kuu ya dawa Visiwani Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein
akifungua rasmini Bohari ya dawa iliopo maruhubi mjini Unguja ikiwa ni
shamra shamra ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hii
ni moja ya sehemu ya ndani ya Bohari la dawa lililopo maruhubi mjini
Unguja lililozinduliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza
la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein
akimuuliza swali msambazaji dawa na vifaa tiba Bi Husna Maulid huko
katika Bohari kuu ya madawa maruhubi mjini Unguja ikiwa ni shamra shamra
ya sherehe za miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Hili
Ndio Bohari la madawa lililopo Maruhubi mjini Unguja lililozinduliwa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed
Shein .
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein
akitoa hutuba yake ya uzinduzi wa Bohari la Madawa lililopo maruhubi
mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Mfamasia mkuu wa kwanza baada mapinduzi huko katika
Bohari la madawa lililopo maruhubi mjini Zanzibar.(Picha zote na Makame Mshenga – Maelezo Zanzibar).
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzíbar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amesema uzinduzi wa Bohari kuu ya Dawa utaiwezesha Serikali ya Mapinduzi
Zanzíbar kupanga bajeti yake vyema ya dawa na kusaidia utoaji wa huduma
za afya kwa ubora wa hali ya juu.
Rais
shein ameyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Bohari Kuu ya Dawa
iliyopo Maruhubi mjini Zanzibar ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za
kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi Zanzibar.
Amesema
Bohari hiyo ya kisasa ni matunda ya kujivunia ya Mapinduzi ya Zanzibar
ambayo kwa hakika italeta tija katika upatikanaji wa dawa na uimarisha
wa afya za wananchi.
Dkt.
Shein ameelezea matumaini yake kwa sekta ya afya kupitia Bohari hiyo na
kwamba anaamini baada ya miaka mitatu Zanzibar itakuwa haipeleki tena
Wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
Aidha
Dkt. Shein amewataka watumishi wa Serikali kubadilika kiutendaji
kulingana na kasi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wa Bohari
hiyo kuitunza vyema ili iendelee kutoa huduma kama inavyotakiwa.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Afya Sira Ubwa amesema Bohari hiyo
itaboresha utoaji wa huduma kwa uhakika kutokana na ubora wa vifaa na
mitambo ya kisasa ambapo wataalamu wataweza kubaini mahitaji ya Dawa
zinazohitajika katika kila Hospitali za Unguja na Pemba.
Kwa
upande wao Mabalozi wa Marekani na Denmark wameelezea kufurahishwa kwao
na juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha afya
ya Wananchi hasa katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Malaria na Ukimwi.
Aidha
wameahidi kuendelea kutoa mashirikiano kwa Serikali hasa katika huduma
za Afya kwa Mama na Watoto, Elimu,Mapambano dhidi ya magonjwa ya
maambukizi pamoja na uzazi wa mpango.
Bohari
hiyo iliyojengwa na Serikali ya Mapinduzi kwa msaada wa Shirika la
USAID na NIDA inaelezewa kuwa ya tatu duniani katika viwango vya ubora
ambapo jumla ya Dolla za Kimarekani Milion 1.2 zimetumika kukamilisha
ujenzi wake.
No comments:
Post a Comment