Rais Kikwete kuzindua Miradi ya Barabara Tabora.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa
miradi ya barabara na daraja katika mkoa wa Tabora kuanzia tarehe 7
Januari 2013.
Pamoja
na shughuli nyingine, Jumatatu tarehe 7 Januari 2013 akiwa mkoani humo,
Mhe. Rais kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya uzinduzi wa ujenzi wa
Daraja la Mbutu liloko Wilayani Igunga.
Jumanne tarehe 8 Januari 2013, Mhe. Rais ataweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi kwa lami wa barabara
1.Nzega – Puge,
2. Puge – Tabora,
3.Tabora – Ndono na
4.Tabora – Nyahua
Siku ya Jumatano ya tarehe 9 Januari 2013 Mheshimiwa Rais ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Ndono hadi Urambo.
Uzinduzi
wa miradi hii ni sehemu ya utekelezaji wa azma ya Serikali ya
kuhakikisha kuwa makao makuu ya mikoa yote yanaunganishwa kwa barabara
za lami. Miradi hii ni mafanikio makubwa katika sekta ya usafirishaji
na itatoa chachu kubwa kwa uchumi wa mkoa wa Tabora na Taifa kwa
ujumla. Aidha, miradi hii itasaidia sana katika kuimarisha Usafiri wa
barabara kati ya Tabora na mikoa ya Kigoma, Shinyanga, Singida na
Dodoma.
Taarifa hii imetolewa na;
Balozi Herbert E. Mrango
Katibu Mkuu
No comments:
Post a Comment