Miraji Mrisho Kikwete ateuliwa kuwa “Makamu wa Rais” wa IBF/Afrika maendeleo ya vijana.
Bw. Miraji Mrisho Kikwete.
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa Africa (IBF/Africa) limemteua bwana Miraji Mrisho
Kikwete kuwa Makamu wa Rais anayeshughulikia maendeleo ya vijana katika
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati. Uteuzi wa Miraji
unaanza January mwaka mpya 2013.
Katika
kumteua Miraji, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na
Mashariki ya Kati bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Miraji ana uwezo wa
kuwahamasisha na kuwaunganisha vijana katika shughuli za maendeleo.
Aliendelea
kusema kuwa Miraji atakuwa anawahamashisha vijana, kuwaunganisha,
kuwajengea uwezo wa kimaendeleo yatakayoratibiwa na IBF.
Aidha,
Rais huyo alisema kuwa Miraji atakuwa anabuni njia mbalimbali za
kuwaunganisha vijana wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati ili
waweze kufaidika na miradi ya IBF ambayo inalenga kwenye elimu, kujenga
vipaji pamoja na kuwaunganisha kwenye biashara ya utalii wa michezo.
Katika
mkutano wake wa mwaka uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la
Hawaii, nchini Marekani hivi karibuni IBF iliupokea mradi wa “Utalii wa
Michezo” uliobuniwa na kuwakilisshwa na Rais wa IBF katika bara la
Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtazania Onesmo Ngowi.
Lengo
kuu la mradi huu ni kulifanya bara la Afrika hususan Tanzania kuwa
kitovu kikuu cha “Utalii Michezo” hivyo kujenga uchumi imara. Nchi za
Tanzania na Ghana ziliteuliwa kuwa nchi za mfano kwenye mradi huu.
Katika
mradi huu, IBF itatumia mtandao walionao katika nchi zaidi ya 203
duniani kuhamasisha wanachama wake na famlia zao, wapenzi pamoja na
marafiki zao kuja Afrika/Tanzania kutalii pamoja na kuwekeza katika
miradi mbalimbali.
Uteuzi
wa Miraji utasaidia kuwaunganisha vijana ili waweze kuchangia na
kufaidika na biashara ya utalii kwenye mradi huu umefanywa wakati
muafaka.
Miraji
ambaye ni Mjasiliamali amejipambanua katika maendeleo ya jamii na ana
mchango mkubwa sana katika kuendeleza vijana nchini Tanzania.
Rais
Ngowi alimwelezea Miraji kama tegemeo ambalo vijana wanalihitaji kwani
wanahitaji uhamasishaji wa hali ya juu na Miraji ana uwezo wa kufanya
kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa kwani alishawahi kuifanya kwa kipindi
kitefu.
Miraji
Mrisho Kikwete ni msomi wa chuo kikuu cha nchini Oman ambako amesomea
elimu ya utawala wa biashara ambayo ndiyo lengo kuu la uteuzi wake. Ana
haiba ya kupendwa na vijana pamoja na uwezo wa kujichanganya nao.
No comments:
Post a Comment