Serikali ya Kongo na waasi wa M23 warejea katika meza ya mazungumzo mjini Kampala.
Serikali ya Kongo na waasi wa kundi la M23 wameendelea tena na mazungumzo ya kutaka kutatua mgogoro unaendelea Mashariki mwa Kongo.
Mazungumzo hayo yanayoendeshwa na waziri wa Ulinzi wa Uganda Dkt. Crispus Kiyonga yameanza hapo jana mjini Kampala nchini Uganda.
Nia kuu ya mazungumzo hayo ni kutafuta suluhisho kwa njia ya amani la mgogoro unaofukuta katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini.
Awamu ya kwanza ya mazungumzo baina ya serikali ya Kongo na waasi wa M23 ilianza Disemba 7 2012 lakini yakasitishwa mnamo Disemba 18 kwa ajili ya sikukuu ya Christimas.
No comments:
Post a Comment